cha1509
JF-Expert Member
- Jul 6, 2018
- 258
- 402
Jembe halimtupi mkulima. Huu msemo umetamalaki sana hapa kwetu Tz, lakini mara kadhaa huwa unakuwaga na ukweli ndani yake.
Msimu wa 2018/19 nilijaribu kulima mpunga Bahi hekari 5, japo nilikodi hekari 12 na kuzitifua zote kwa trekta, ila nikakumbana na ukame wakati napandikiza. Nilifanikiwa kupandikiza mashamba matano tu maji yakawa yameisha. Hivyo, nikawa sina jinsi.
Si haba katika heka hizo tano nimeweza kurudisha mbegu, nimepata magunia 54, yenye ujazo wa debe saba saba (7,7). Kiukweli nashukuru sana Mungu kwan mwaka huu ulikuwa na changamoto sana. Wengine hawakuweza kuvuna kabisa hata lita moja.
Nimezidi kujifunza mengi katika kilimo, ndugu zangu. Wakati mimi nimepata vigunia 54, kuna mtu kapata migunia 400, na mwingine migunia 600, hivyo ukiwa kupanda uhakika wa kupiga pesa kupitia kilimo INAWEZEKANA.
Nimeona si haba niwaletee mrejesho wananzengo kwani kuna baadhi ya wanaJF walitaka mrejesho mara baada ya kutoka shambani.
Picha hizi hapa