Mrejesho: Kikao cha kutoa mitaji kwa watoto wa mstaafu

Nejad Rocket

JF-Expert Member
Jul 5, 2017
298
197
Habari za asubuhi wana Jf.Jana usiku nilishirikishwa kikao cha familia ya Mzee mmoja mstaafu mwalimu wa shule ya msingi wilaya ya Muheza Tanga.

Huyu mzee ni msambaa amepata milioni 77 ana watoto 6 wanne wa kiume wawili wa kike.Ni rafiki yangu sana ndo mana kanikaribisha kwenye kikao baada ya kumshauri mambo kadhaa Kwa watoto wake.

Baada ya kufungua kikao aliwaambia lengo la kuwaita kuwa ni kuwapa mitaji kwakuwa wote hawakubahatika kuajiriwa isipokuwa mmoja wa kiume ambae ni mwalimu pia.

Akawapa fursa kila mmoja aeleze anataka kufanya biashara kilimo au chochote.Kila mmoja alieleza lengo lake Kwa ufasaha kabisa na baba yao akawaahidi atawapa kila mmoja mtaji wa milioni tatu kila mmoja.

Bila hiana mzee akatoa bulungutu alikuwa ameziandaa bila ya kuwaambia akanikabidhi niwape alikuwa kazibana M3 kila bunda.Watoto walifurahi kupita maelezo.
Akawapa neno kuwa pesa alizowapa si za kuchezea kununua nguo mawigi madela na starehe nyinginezo.

Akamalizia Kwa kuwaambia kuwa atakaye chezea pesa hizo asifikiri atapata nyingine hivyo wawe makini sana.Waliahidi kuwa makini katika malengo yao.

Funzo.Laiti wazazi wote wangelikuwa kama huyu mzee mstaafu basi tisingeshuhudia shida mtaani Kwa baadhi ya familia za wastaafu.Ruhusa kutoa maoni yenu members.
 
Huyo mzee nae kilaza..hizo ni pesa zake za kujikimu mpaka kufa..akiwapa watoto wata tapanya hawana uchungu Nazo..yaelekea Mzee hakuwasomesha ..so sad! atakufa kifo cha masikitiko sana!
 
Huyo mzee angekua na akili angewakopesha kwa riba, wangetia akili na kufanyia kazi kibiashara hizo pesa, hao watu wa waja leo warudi leo, wanaenda kuolea au kuchezeshea ngoma hizo pesa.
 
Huyo mzee nae kilaza..hizo ni pesa zake za kujikimu mpaka kufa..akiwapa watoto wata tapanya hawana uchungu Nazo..yaelekea Mzee hakuwasomesha ..so sad! atakufa kifo cha masikitiko sana!

IMG_3010.jpg

Hii picha ni ya yule Ex KGB aliyelishwa Polonium na watu wa Putin kule London? Au nimemfananisha?
 
Yah ni jambo jema sana alilofanya huyo mzee.na kwa huko Tanga itafaa kwa hiyo pesa wakanunua au kukodi vitivo wakafanya kilimo,ni mtaji tosha ktk sekta hiyo ila kwengine inaweza kuwa ndogo kidogo ikawasumbua akili.
 
Back
Top Bottom