Mrejesho: Je, ulishiriki shindano la “JF Stories of Change?” Kuwa karibu na PM yako

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
4,991
Ule wakati wa Washindi wa Shindano la Stories of Change kujulikana umewadia. Muda wowote kuanzia sasa jopo la majaji baada ya kupitia, kuchambua maandiko na kujiridhisha na maamuzi yao, litakabidhi maandiko yaliyofanikiwa kushinda kwa timu ya uratibu wa shindano.

Washiriki wote wa Shindano la Stories of Change wanatakiwa kuangalia kwenye jumbe zao za faragha za Jamii Forums (PM) ili kuona endapo wametumiwa ujumbe kutoka akaunti Rasmi ya Jamii Forums (hakikisha ni akaunti hii na si vinginevyo) kwa kusudi la kupata mawasiliano yao.

Hivyo, kama ulishiriki, au unamjua Mtu aliyeshiriki Shindano hili, mfikishie ujumbe huu muhimu.

Zingatia: Ni muhimu kutoa Ushirikiano (PM) kama ilivyo kwenye Vigezo na Masharti ya Shindano hili. Kama haujapokea Ujumbe wowote, jua kura zako za Majaji hazikutosha.

Timu nzima ya JamiiForums inakushukuru Wewe uliyetenga muda wako kushiriki kuandika, kusoma na hata kupiga kura Jukwaani. Mwisho wa Shindano hili, ni Mwanzo wa Shindano lingine hivyo kaa Mkao wa Kushinda.

Asanteni.

Zaidi, soma:
1. Shindano: Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (Stories of Change)

2. Mshindi wa Shindano la Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija ( JF Stories of Change) kujulikana Ijumaa tarehe 15 Oktoba, 2021
 
Waandaaji basi walau mngewaambia Washiriki ya kuwa kutokushinda haimaanishi waliandika utumbo
 
Nilishinda aisee kwa ID yangu ile nyingine, nawashukuru waandaaji na nawasihi washiriki wenzangu msikate tamaa.

Ujumbe:

Milioni 3 taaaamuu.
 
Back
Top Bottom