Mrejesho: I need A Girl : Where are you Cute Girl blessed with Inner & Outer Beauty?!!.

Sawa......ol the best! Ila mkihitaji wanakamat nipo hapa mkuu! Najitolea kwa kamat ya chakula na vinywaj
 
Man, I'm just as cool as an ice cube!
The problem is you take life too serious!
Take a chill pill and relax, no hard feelings!
hater is spoken! nothing is too serious in life and love!
 
Sawa kiongozi... Hongera kwa kumpata mwandan wako ila ungetutajia id yake ili tuache kumuibukia pm
 
Wasalaam Alekyum! , Shalom! na Amani Ya Bwana! Iwe Nanyi Nyote wana JF-Love Connect.

Kwanza kabisa katika uzi huu nataka kuandika kwa kiswahili fasaha kabisa ili kila kiumbe kitambaacho katika ardhi ya ulimwengu huu kinielewe. Lakini ieleweke sijaja hapa kuhubiri Injili bali tu kuwapa mrejesho wa Habari Njema ambayo imekuwa raha yangu sasa na maisha ya badae.


Ifahamike hapa majuzi kati niliweka uzi ambao ulizua utata mwingi sana hapa jukwaani yaani kwa kiiingereza ' a more controversial thread' ambao ulikuwa na kichwa cha habari ' I need a Girl: Where are you cute girl blessed with inner & outer beauty?. Katika kupitia mawazo ya wadau wengi katika komenti zenu kuna ambao kikawaida wao ni 'hater' tu watu kama hawa huwa hawana jema kwao ( yaani huwa wanapinga ama kuponda chochote tu bila sababu za msingi), kuna watu wa nguvu pia walitoa mawazo yao hawa huwa nawaita watu wakiroho safi ( watu wa namna hii huwa wanamtakia mtu heri nakumtia moyo kwa lolote lile ambalo mtu anaazimia kufanya). Pia kuna watu ambao mimi huwaita ni much-know ingawa kiukweli watu wa namna hii huwa wanajifanya kujua sana zaidi ingawa kiuhalisia hawajua lolote, hawa hujifanya kukosoa ama kujifanya kurekebisha utadhani wao ndo wanajua kuliko mtoa uzi. Kiufupi kundi hili la watu ni sawa na aina ya watu ambao unawaalika kwenye shughuli yako halafu wanakupangia chakula cha kula!. Nashukuru hii ni thinking diversity - au kwa kiswahili mgawanyiko wa fikra na mawazo ambao ndio unatupa umoja wetu wana JF-Love Connect.

Sasa bana nisiwachoshe, nimeona niwape mrejesho wa uzi huo ambao kuna watu waliponda sana sana mara oh nimeandika kwa kiingereza ntaambulia patupu wengine walijifanya walimu wa English kwenye uzi wangu, wengine waliibuka nakunipa kashfa za uongo kuwa nimewadhalilisha wasichana kwa uzi ule kwa kusema sikuona mwanamke wa vigezo vyangu basi ilimradi ikawa kukurukukara tu kwenye uzi ule mtu anatupia komenti yake anavyojisikia kama vile unavyoamka asubuhi nakuamua kuvaa nguo uipendayo. Bana mdau wenu nilichukulia poa tu mawazo yote na wengine niliweza kuwapa shit live pale ilipobidi maana falsafa yangu ni moja tu kwamba jinsi utavyokuja kwangu ndivyo nami ntakupokea.


Haya tuendelee, unajua niliibuka jukwaani hapa kwa uzi huo nikiwa natafuta mwandani, mtoto ambae anaweza niongezea sababu za kuishi duniani hapa. Lahaula bana katika ile kukata tamaa mdau wenu si unajua majukumu so huwa naingia kwa kuibia ibia huku mara paap nikaona text imeingia kunako inbox, kiuhalisia nyingi zinaingia ila hii niliichukulia tofauti na kiukweli hisia zangu zilipelekea sawa. Ulikua ni ujumbe wa mrembo ambae kwa kipindi hiki kifupi tulichojuana kupitia jukwaa hili naona kama tumejuana miaka na miaka kwa jinsi tulivyo-click pamoja. Basi tukabadilisha hili na lile siku za mbeleni tukabadilishana namba tukawa tunawatsapika nakufanya regular calls. Ebana nani alowaambia JF-Love Connect hakuna watoto waliobarikiwa kila kitu?! kuanzia uzuri wa sura, tabia, umbo?!. Kama alowaambia hivyo ama kufikiria hivyo anajidanganya, kwani kama wanavyosema uzuri sio sura wala maumbile bali uzuri tabia basi mimi nawaambia kupitia ule uzi wangu nimempata mtoto mzuri hatari kisura umbo na tabia, zaidi anatoka nyumbani kabisa kanda ya kaskazini. Kwa muda mfupi tuliokaa pamoja kuwasiliana nakukutana live kiukweli nimeona kama nimeshushiwa ngekewa maana ana kila kitu nilichokuwa nahitaji kwa mwanamke awe nacho. Kwanza, ni mzuri balaaa kimuonekano tu, pili ni mcheshi sana na muelewa ingawa kwa sasa yuko chuo kikuu kimoja hivi anasoma ila anaonekana ni binti ambaye anajua anachokifanya, mkarimu mwenye malengo. Kifupi kila mmoja wetu anakaa nakufikiria nakusema kuwa ingawa kama tulianza kama utani hivi tukidhani haiwezekani lakini kwa hatua tuliyofikia nadhani tutasonga mbali sana.

Nawashukuru wote mlionesha nia njema yakunitakia mema, nakushukuru pia bebe wangu, sijui nikutaje?! hapana itakuwa si hekima, ila najua unasoma huu uzi, nakushukuru sana (mama mchungaji)kama jinsi navyokuita kwa jina la utani kwa kuchukua hatua nakunielewa, nnachokuahidi ni kuwa nitakupa penzi ambalo hujawahi pata na hutojuta kunifahamu. Kama tulivyoongea mpaka kufikia mwezi December tutatangaza nia nyumbani kwa wazazi. Nakushukuru kwa kunifanya chaguo lako nakuvutiwa na mimi pia maana hiyo nayo ni Karisma.

Pia nalishukuru jukwaa hili la JF-Love Connect kwa kuweza kufanya yasiyowezekana, kuniunganisha na binti ambae sikuwaza kumpata humu jukwaani. Ujumbe wangu kwa wengine ni kuwa hakuna linaloshindikana chini ya jua. Kila mtu ana fungu lake haijalishi jinsi fungu hilo linavyokuja ama kupokelewa. Maisha ni popote, unaweza pata mwenza popote pale, tena kwa teknolojia ilivyoongezeka hivyo hata kiteknolojia kama hivi watu tunakutana. Halafu kama mtaani watu walivyo ndivyo hivyo hivyo JF Love Connect watu wapo, kuna watu wa aina zote cha muhimu ni kuwa na malengo nakuomba Mungu akuongoze pia kwani huwezi muomba Samaki akukupa Nyoka.

Nawasilisha!
Wish u all the best.. Msimegane sasa, sex hadi ndoa okay..?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom