sheikh yasin
Member
- Aug 6, 2015
- 61
- 45
Wadau hamjambo?
Niliwahi kuweka habari ya kuhusu Hela za matunzo ya mtoto wanakula na mwanaume mwingine
Ni wiki ya Tatu sasa nipo hapa Dar kushughulikia mgogoro ulioibuka kati yangu na mzazi mwenzangu kuhusu matunzo na haki za huyu mtoto wetu kwa ujumla.Ikumbukwe kwamba nilisitisha huduma zote za ki utu kwa mama na mtoto tangu mwezi January baada ya kuthibitisha pasipo shaka kuwa pesa za matunzo nilizokua natuma zinamnufaisha pia mpenzi wa huyu mzazi mwenzangu.
Huyu bwana anaishi kwenye hicho hicho chumba ninacholipia kodi hivyo wanambana mwanangu kwenye godoro langu nililonunua, hilo jitu linakula chakula kupitia hela zangu ninazotuma, zaidi ya yote halifanyi kazi yoyote linashinda nyumbani kutwa nzima kila siku, hata vibarua tu limeshindwa kwenda kufanya.
Baada ya kusitisha huduma mama mtoto aliniripoti dawati la jinsia na kuitwa ustawi wa jamii, ambapo hatukupata muafaka kwenye kikao cha kwanza ambacho nilikitolea taarifa hapa na kuchukua ushauri wenu kikamilifu, hivyo baada ya vikao mfululizo hapo Ustawi verdict imetolewa na nimeibuka mshindi kwa hoja zifuatazo;
Mashaidi wangu akiwemo mjumbe wa mtaa, mwenyekiti wa mtaa, baba mwenye nyumba na wapangaji wamethibitisha pasipo shaka kuwa mzazi mwenzangu na mpenzi wake hawana uwezo wa kuendesha maisha ya huyu mtoto kiuchumi na kimaadili, na kwa kuwa mtoto amefikisha miaka saba, ni bora akaishi pesa ziliko badala ya pesa hizo kumfuata yeye kila mara na hanufaiki nazo isipokua wale wapenzi wawili.
Ustawi wameridhika na maisha yangu kwamba naaminika, mke wangu ameshakoma kuzaa, tayari ana watoto wapo chuo, hivyo mtoto mdogo kwake ni baraka, atakua na chumba chake na sio ku share chumba na adults na kushuhudia tendo kila siku, under 3 of age anaweza asijue chochote lakini sio mtoto wa miaka saba tena darasa la pili.
Nimekwisha kupewa mtoto, Jana nimepewa ripoti za shule na barua ya head teacher ili aweze kupokelewa shule nyingine huko mwanza, bahati nzuri shule binafsi hazina usumbufu,mzazi mwenzangu alilia na kugala gala chini uamuzi huo ulipotolewa, Lakini akaambiwa aende mahakamani iwapo hakuridhika lakini wao wamezingatia hali halisi ilivyo.
Hata hivyo nimetoa offer kwake, kama kweli yupo serious kuishi na mwanae karibu aje na sisi Mwanza nitampangia mtaani chumba na sebule pengine na biashara ya kawaida aendelee na maisha yake na mtoto atakaa nae, maana tutakua mji mmoja nitaweza kujua wanaishije, hata akipata mpenzi sio shida ilimradi mtoto anaishi vizuri, tunaweza kuishi kwa ushirikiano.
Nasubiri majibu ya offer yangu.
Wadau nawashukuru