Mrejesho: Chikira Mtabari natoa mrejesho wa nilipokuwa

NAKWEDE

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
27,966
35,152
Nawasalimu wote humu JF kwa kuzingatia utukufu wa aliyejuu.

Ninayo furaha kuwajulisha kuwa nimetoka vijijini nilipokuwa na sasa niko hapa Mwanza town.

Katika safari yangu huko vijijini niliona, kusikia na kushiriki mambo mengi,lakini kuna hili ambalo ninaomba niwashirikishe.

Issue yenyewe ni kwamba nilikuta mtoto wa kiume yuko darasa la nne anaitwa jina ambalo kusema kweli halina "ladha" kulitamka mdomoni. Baada ya kusikia jina hilo ilibidi nimuulize mama wa mtoto huyo ilikuwaje hadi kumuita mwanae jina ambalo halinogi?

Ni kwamba, mtoto huyo anaitwa NYEGE, historia ya kupewa jina hilo kwa maelezo ya mama yake ni kwamba mtoto NYEGE alipozaliwa alipewa jina lingine lakini akawa analia sana usiku na mchana hapo ndipo ilibidi wazazi wake waende kwa "WATAALAMU" na huko iligundulika kuwa mtoto huyo analilia jina la mzee ambaye ni marehemu katika ukoo huo alikuwa anaitwa NYEGE na kwamba kama wanataka kunusuru maisha ya mtoto huyo basi waache kumuita lile jina la awali walilokuwa wamempa na rasmi mtoto huyo aitwe jina na babu yake marehemu mzee NYEGE. Mama alizidi kunieleza kuwa baada kuzingatia ushauri wa MTAALAMU wa kumpa mtoto jina la NYEGE basi mtoto siku hiyo hiyo aliacha kulia, akawa buheri wa afya hadi mie nilivyomuona yuko darasa la nne, na kwamba shuleni imebidi aandikwe jina hilo hilo.

mmmmmh! mambo ya mila hayo! sikujua kama mtoto anaweza kulilia jina la marehemu mababu na mababu.

Mshana jr, unasemaje kwenye hili na wataalamu wengine wa masuala ya kijamii naombeni uzoefu wenu.
 
Mh hizi mila nazo, mi nilikutana na mtoto anaitwa kifuu ila sikujua asili yake
 
Wala halina shida kabisa...bonge la jina!

Shida ni pale ambapo rafiki yake atakapochelewa kurudi nyumbani kisha aulizwe na wazazi wake alikokuwa.

Jane: "Nilikuwa na Nyege"
Kuna mama yeye aliambia kuwa yani mimi huwa huyu mtoto akija kucheza nyumbani kwangu na wanangu namwambia haraka sana NYEGE rudi kwenu maana naona aibu pale wanangu wakianza, weee NYEGE nipe mpira wangu, au mama NYEGE ni mchokozi"
 
Back
Top Bottom