Mrejesho biashara ya madini 'third season'

mcrounmj

JF-Expert Member
Feb 26, 2016
380
885
Salam zangu na zisambae kwenu nyote. Matumaini yangu mu buheri wa afya tele, na hata walioteteleka mwenyezi Mungu awajaalie wepesi wa kupona haraka.

Ahadi ni deni. Nami tangu nimeanza mbio zangu za kibiashara kwenye madini ya Dhahabu nimekuwa na tendency ya kuripoti wapi nimefikia kila baada ya miezi sita. Niliwahi kuja na post ya mrejesho first season Mrejesho: Biashara ya madini aina ya dhahabu

baadae nikaleta second seoson Mrejesho biashara ya madini ya dhahabu second season

Na sasa naileta 'third season'. Labda nianze kwa kusema kuwa watu wengi wananifuata pm kutaka kuonana na Mimi. To be honest, siko tayari kuonana na mtu ila kama utahitaji msaada mwingine wa maelekezo nitakujibu. Nafanya hivi kwa sababu hatujuani, nami sitaki kumulikwa kihivyo.

Baada ya kununua Karasha mwezi may 2021, nikitumia takribani 11mil, nilibakiwa na mtaji wa kama 12 millions. Kwa ukanda wetu huku huwa tunasaga mawe bure, hivyo ni kuhudumia tu yaani unanunua diesel mwanzo mwisho hela ukitoa mfukoni.

Kazi ya kusaga mawe nilianza kwenye tar 10 may hivyo Sasa nimekamilisha miezi sita. Nilipata sehemu ya kuchimba mawe kwenye mgodi wa rafiki yangu. Huwa naajiri watu nawalipa kwa mwezi wanafanya kazi ya kutoa mawe baada ya kulipua. Mawe hayo huwa nagawana na mwenye mgodi yeye akichukua 40%, Mimi nachukua 60% ya mawe. Kisha huwa nayabeba na kwenda kuyasaga karashani kwangu.

Saivi rudio limekuwa kubwa nakadiria gari za tani kumi 20. Sampo nikipima maabara inasoma 8ppm na zaidi. Mpaka saivi natoa faida kwenye biashara ya Dhahabu nahudumia Karasha, na Sasa nataka mlima uendelee kukua hadi mwakani mwezi may.

Changamoto ni pesa ya mtaji imezidiwa na matumizi ya Karasha kwani inapungua siku hadi siku. Kwa hiyo nitapambana kwa namna yoyote ili hadi kufikia mwakani mwezi wa sita nichenjue mlima.... Na hapo nikipata angalau kilo mbili za Dhahabu, nitapambania lessen ya u dealer. Na hapo nitaianza rasmi safari ya kuusaka ubilionea.

Vijana wenzangu wakike na wakiume ni wakati sahihi sasa wa kuamua kuzifuata ndoto zako. Wengi tunashindwa kuingia kwenye fulsa za biashara kwa kuamini kuwa hatuna mitaji. Nikwambie tu mtaji ni kitu kidogo sana kwenye biashara. Unaweza uwe na mtaji na ushindwe kufanya biashara ikakua. Hivyo kitu kikubwa kwenye biashara lazima uwe na confidence na utashi wa kuifanya hiyo biashara.

Nitoe mfano wa binti mmoja nimemfahamu anaitwa Diana (jina la uongo). Alikuwa anafanya biashara ya kujumua pombe kali anapeleka migodini.

Alikuwa anafuata mpakani Tunduma anakuja kuuza Chunya. Alianza na mtaji wa laki na nusu tokea 2019. Diana alifanya biashara hiyo kwa miezi saba akawa na hela kama laki 9. Akaamua kuongeza vitenge kwenye kufunga mzigo. Bahati mbaya siku moja akiwa kwenye usafiri gari ilipata ajali akavunjika mguu. Alitumia pesa karibia yote aliyokusanya kujiuguza.

Mpaka anapona alikuwa amebakiwa na kama laki mbili tu. Mguu ulipona vizuri. Alichofanya Diana aliamua kubadilisha biashara, alikodi fremu akafungua genge la mbogamboga. Amefanya biashara hii kwa mwaka, ikamlipa maradufu.

February ya mwaka huu alifungua grocery karibu na pale anapouzia mbogamboga. Bia ambazo zinauzwa 2500 bar yeye anauza buku jero. Savi mwezi November ameongeza duka la mitumba hapohapo karibu.

Nimemtolea mfano Diana kuonyesha ni jinsi gani unaweza kuwa na ndoto kubwa ya kumiliki benki, ukaanza na sh elfu hamsini kuitekeleza ndoto yako.

Panapo majaaliwa tukutane tena June 2022 hapahapa kupeana update.
 
Changamoto ya makarasha ni kupata sehemu nzuri yenye mwamba mzuri wenye uhakika wa kupata mawe mengi

Unaweza ukapata ka long base ukafaidika siku mbili ya tatu mchirizi ukakata.

Ni biashara yenye pesa nyingi endapo uta point sehemu yenye mawe yenye dhahabu na sio unakusanya dumu saba unapata point mbili
 
Changamoto ya makarasha ni kupata sehemu nzuri yenye mwamba mzuri wenye uhakika wa kupata mawe mengi

Unaweza ukapata ka long base ukafaidika siku mbili ya tatu mcjirizi ukakata.

Ni biashara yenye pesa nyingi endapo uta point sehemu yenye mawe yenye dhahabu na sio unakusanya dumu saba unapata point mbili
Hapo kweli mkuu. Yaani ukiwa unasaga mwamba angalau dumu litoe point moja kwenye rudio lazima lisome kuanzia 4ppm. Na kikubwa ukiwa unakuza mlima angalau uanzie kusoma 2.5ppm na siyo chini ya hapo
 
Unajua hii biashara ilianza kimazabe sana, awali watu walikua wanafunga makarasha kwa ajili ya kupata wateja wanaosaga mawe, yani mmiliki wa karasha faida yake ilikuwa ni ile 5,000 anayolipwa na mteja anayeleta mawe yake

Kipindi hicho bado hawajasanuka kua sainet ni bonge la mchongo maana kipindi hicho hata jiwe lilikuwa lina dhahabu sana tofauti na saizi yalivyokua adimu
 
KARASHA ni lile mashini la kusaga mawe yaani CRUSHER! Au siyo kama nimekosea nisahihisheni! KARASHA ni nickname ya CRUSHER huko migodini!

Haya kazi yake ni kusaga mawe "yenye dhahabu". Kwa nini ni ghali sana huko Chunya, nadhani Kahama na hata Geita yanatengenezwa kwa kati 5 na 8mi!? Halafu, kwa hili, nisameheni sana, sijui kama hicho kipimo cha ppm, uliwahi kukitaja kwenye 1st au 2nd sessions!? Hicho "ppm" ni kipimo cha nini - ni cha wingi wa dhahabu kwa kiroba au nini? Saidia Msomi wangu.
 
Salam zangu na zisambae kwenu nyote. Matumaini yangu mu buheri wa afya tele, na hata walioteteleka mwenyezi Mungu awajaalie wepesi wa kupona haraka.

Ahadi ni deni... Nami tangu nimeanza mbio zangu za kibiashara kwenye madini ya Dhahabu nimekuwa na tendency ya kuripoti wapi nimefikia kila baada ya miezi sita. Niliwahi kuja na post ya mrejesho first season Mrejesho: Biashara ya madini aina ya dhahabu

baadae nikaleta second seoson Mrejesho biashara ya madini ya dhahabu second season

Na sasa naileta 'third season'.... Labda nianze kwa kusema kuwa watu wengi wananifuata pm kutaka kuonana na Mimi. To be honest, siko tayari kuonana na mtu ila kama utahitaji msaada mwingine wa maelekezo nitakujibu. Nafanya hivi kwa sababu hatujuani, nami sitaki kumulikwa kihivyo.

Baada ya kununua Karasha mwezi may 2021, nikitumia takribani 11mil, nilibakiwa na mtaji wa kama 12 millions. Kwa ukanda wetu huku huwa tunasaga mawe bure, hivyo ni kuhudumia tu yaani unanunua diesel mwanzo mwisho hela ukitoa mfukoni.

Kazi ya kusaga mawe nilianza kwenye tar 10 may hivyo Sasa nimekamilisha miezi sita. Nilipata sehemu ya kuchimba mawe kwenye mgodi wa rafiki yangu. Huwa naajiri watu nawalipa kwa mwezi wanafanya kazi ya kutoa mawe baada ya kulipua. Mawe hayo huwa nagawana na mwenye mgodi yeye akichukua 40%, Mimi nachukua 60% ya mawe. Kisha huwa nayabeba na kwenda kuyasaga karashani kwangu.

Saivi rudio limekuwa kubwa nakadiria gari za tani kumi 20. Sampo nikipima maabara inasoma 8ppm na zaidi. Mpaka saivi natoa faida kwenye biashara ya Dhahabu nahudumia Karasha, na Sasa nataka mlima uendelee kukua hadi mwakani mwezi may.

Changamoto ni pesa ya mtaji imezidiwa na matumizi ya Karasha kwani inapungua siku hadi siku. Kwa hiyo nitapambana kwa namna yoyote ili hadi kufikia mwakani mwezi wa sita nichenjue mlima.... Na hapo nikipata angalau kilo mbili za Dhahabu, nitapambania lessen ya u dealer. Na hapo nitaianza rasmi safari ya kuusaka ubilionea.

Vijana wenzangu wakike na wakiume ni wakati sahihi sasa wa kuamua kuzifuata ndoto zako. Wengi tunashindwa kuingia kwenye fulsa za biashara kwa kuamini kuwa hatuna mitaji. Nikwambie tu mtaji ni kitu kidogo sana kwenye biashara. Unaweza uwe na mtaji na ushindwe kufanya biashara ikakua. Hivyo kitu kikubwa kwenye biashara lazima uwe na confidence na utashi wa kuifanya hiyo biashara..... Nitoe mfano wa binti mmoja nimemfahamu anaitwa Diana (jina la uongo). Alikuwa anafanya biashara ya kujumua pombe kali anapeleka migodini.

Alikuwa anafuata mpakani Tunduma anakuja kuuza Chunya. Alianza na mtaji wa laki na nusu tokea 2019. Diana alifanya biashara hiyo kwa miezi saba akawa na hela kama laki 9. Akaamua kuongeza vitenge kwenye kufunga mzigo. Bahati mbaya siku moja akiwa kwenye usafiri gari ilipata ajali akavunjika mguu. Alitumia pesa karibia yote aliyokusanya kujiuguza. Mpaka anapona alikuwa amebakiwa na kama laki mbili tu. Mguu ulipona vizuri. Alichofanya Diana aliamua kubadilisha biashara, alikodi fremu akafungua genge la mbogamboga. Amefanya biashara hii kwa mwaka, ikamlipa maradufu. February ya mwaka huu alifungua grocery karibu na pale anapouzia mbogamboga. Bia ambazo zinauzwa 2500 bar yeye anauza buku jero. Savi mwezi November ameongeza duka la mitumba hapohapo karibu.

Nimemtolea mfano Diana kuonyesha ni jinsi gani unaweza kuwa na ndoto kubwa ya kumiliki benki, ukaanza na sh elfu hamsini kuitekeleza ndoto yako.

Panapo majaaliwa tukutane tena June 2022 hapahapa kupeana update.
Nafasi ya WAZEE iko wapi kwenye biashara hii ya dhahabu!? Nashangaa na ninauliza hivyo kwani mnazungumzia vijana, vijana tu kwenye hii biashara! Nauliza hivyo kwa sababu mimi ni MZEE MTAFUTAJI!
 
Kitu pekee nashauri vijana kutokana na thread ya jamaa ana motivate kutokukata tamaa stick on what you do… hasara zipo faida zipo.. else where anakosea kukisia kwamba ataweza tu.. yaani stry yake kama imeshawahi tokea yeye anahadithia..
Tupambane ndugu zangu.
Huyu jamaa tumuache kwenye dhahabu. Ukihitaji zaidi fanya research.
 
Salam zangu na zisambae kwenu nyote. Matumaini yangu mu buheri wa afya tele, na hata walioteteleka mwenyezi Mungu awajaalie wepesi wa kupona haraka.

Ahadi ni deni... Nami tangu nimeanza mbio zangu za kibiashara kwenye madini ya Dhahabu nimekuwa na tendency ya kuripoti wapi nimefikia kila baada ya miezi sita. Niliwahi kuja na post ya mrejesho first season Mrejesho: Biashara ya madini aina ya dhahabu

baadae nikaleta second seoson Mrejesho biashara ya madini ya dhahabu second season

Na sasa naileta 'third season'.... Labda nianze kwa kusema kuwa watu wengi wananifuata pm kutaka kuonana na Mimi. To be honest, siko tayari kuonana na mtu ila kama utahitaji msaada mwingine wa maelekezo nitakujibu. Nafanya hivi kwa sababu hatujuani, nami sitaki kumulikwa kihivyo.

Baada ya kununua Karasha mwezi may 2021, nikitumia takribani 11mil, nilibakiwa na mtaji wa kama 12 millions. Kwa ukanda wetu huku huwa tunasaga mawe bure, hivyo ni kuhudumia tu yaani unanunua diesel mwanzo mwisho hela ukitoa mfukoni.

Kazi ya kusaga mawe nilianza kwenye tar 10 may hivyo Sasa nimekamilisha miezi sita. Nilipata sehemu ya kuchimba mawe kwenye mgodi wa rafiki yangu. Huwa naajiri watu nawalipa kwa mwezi wanafanya kazi ya kutoa mawe baada ya kulipua. Mawe hayo huwa nagawana na mwenye mgodi yeye akichukua 40%, Mimi nachukua 60% ya mawe. Kisha huwa nayabeba na kwenda kuyasaga karashani kwangu.

Saivi rudio limekuwa kubwa nakadiria gari za tani kumi 20. Sampo nikipima maabara inasoma 8ppm na zaidi. Mpaka saivi natoa faida kwenye biashara ya Dhahabu nahudumia Karasha, na Sasa nataka mlima uendelee kukua hadi mwakani mwezi may.

Changamoto ni pesa ya mtaji imezidiwa na matumizi ya Karasha kwani inapungua siku hadi siku. Kwa hiyo nitapambana kwa namna yoyote ili hadi kufikia mwakani mwezi wa sita nichenjue mlima.... Na hapo nikipata angalau kilo mbili za Dhahabu, nitapambania lessen ya u dealer. Na hapo nitaianza rasmi safari ya kuusaka ubilionea.

Vijana wenzangu wakike na wakiume ni wakati sahihi sasa wa kuamua kuzifuata ndoto zako. Wengi tunashindwa kuingia kwenye fulsa za biashara kwa kuamini kuwa hatuna mitaji. Nikwambie tu mtaji ni kitu kidogo sana kwenye biashara. Unaweza uwe na mtaji na ushindwe kufanya biashara ikakua. Hivyo kitu kikubwa kwenye biashara lazima uwe na confidence na utashi wa kuifanya hiyo biashara..... Nitoe mfano wa binti mmoja nimemfahamu anaitwa Diana (jina la uongo). Alikuwa anafanya biashara ya kujumua pombe kali anapeleka migodini.

Alikuwa anafuata mpakani Tunduma anakuja kuuza Chunya. Alianza na mtaji wa laki na nusu tokea 2019. Diana alifanya biashara hiyo kwa miezi saba akawa na hela kama laki 9. Akaamua kuongeza vitenge kwenye kufunga mzigo. Bahati mbaya siku moja akiwa kwenye usafiri gari ilipata ajali akavunjika mguu. Alitumia pesa karibia yote aliyokusanya kujiuguza. Mpaka anapona alikuwa amebakiwa na kama laki mbili tu. Mguu ulipona vizuri. Alichofanya Diana aliamua kubadilisha biashara, alikodi fremu akafungua genge la mbogamboga. Amefanya biashara hii kwa mwaka, ikamlipa maradufu. February ya mwaka huu alifungua grocery karibu na pale anapouzia mbogamboga. Bia ambazo zinauzwa 2500 bar yeye anauza buku jero. Savi mwezi November ameongeza duka la mitumba hapohapo karibu.

Nimemtolea mfano Diana kuonyesha ni jinsi gani unaweza kuwa na ndoto kubwa ya kumiliki benki, ukaanza na sh elfu hamsini kuitekeleza ndoto yako.

Panapo majaaliwa tukutane tena June 2022 hapahapa kupeana update.
Nakushauri ufanye kununua na kuuza huku ukiendelea nakuchimba. Utafilisika ukiendelea kuchimba na kuchenjua,i have been doing that for time now.don't start like that,it needs more capital and u may not get the required amount za kufidia gharama za uzalishaji.

Kama huna trader nicheki ntakuelekeza trader uwe unanunua kwa wachimbaji wengine nakuuza kwa trader uku unaendelea nakuchimba. Mimi nilikuwa na mtaji wa laki 5 sasaivi nina mil.9 baada yakuanguka mara kadhaa kujifunza adi nlipokaa sawa.nimefilisika mara nyingi.

Ninavokuambia apa nina hecta 200 mkoa wa ruvuma pekee nilichukua leseni lakini ninazochimba ni kama hecta 2 tu.ninanunua na kuuza zaidi.ninafanya gold na germstones za aina nyingi kama ruby,alexandrite,saphire,tomarin. Shida ya uko uliko ni dhahabu tu germstones ni chache sana. Uku navuna vyote.
 
Basi na wewe tuelezee habari za GEMSTONES tupate elimu kama wafanyavyo wengine. Tueleze kuhusu ununuzi na uchimbaji wa gemstones na masoko yake humu nchini na nje ya nchi. Tunasubiri KKEngineer!
 
Hahaha nimecheka kishenzi, hizo ndio lugha zetu huko kwenye migodi

excavator kule tunaita skaveta

jaw crusher tunaita jograsha
Dah first time nafika kanda ya ziwa nilikuwa nashangaa hawa watu wanaongelea nini. Imebidi nizowee tu maana unaweza kuambiwa wekamo ukabaki huelewi.
 
Mimi nilipoenda machimboni nilijifunza kua kule wanaishi ulimwengu tofauti na huu ambao mimi na wewe tumeuzoea

Kule long base wanaita longobesi
 
Nakushauri ufanye kununua na kuuza huku ukiendelea nakuchimba. Utafilisika ukiendelea kuchimba na kuchenjua,i have been doing that for time now.don't start like that,it needs more capital and u may not get the required amount za kufidia gharama za uzalishaji.

Kama huna trader nicheki ntakuelekeza trader uwe unanunua kwa wachimbaji wengine nakuuza kwa trader uku unaendelea nakuchimba. Mimi nilikuwa na mtaji wa laki 5 sasaivi nina mil.9 baada yakuanguka mara kadhaa kujifunza adi nlipokaa sawa.nimefilisika mara nyingi.

Ninavokuambia apa nina hecta 200 mkoa wa ruvuma pekee nilichukua leseni lakini ninazochimba ni kama hecta 2 tu.ninanunua na kuuza zaidi.ninafanya gold na germstones za aina nyingi kama ruby,alexandrite,saphire,tomarin. Shida ya uko uliko ni dhahabu tu germstones ni chache sana. Uku navuna vyote.
Gemstones ni biashara ya kubahatisha mauzo yake..sio kama dhahabu..

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom