Mrejesho biashara ya madini 'third season'

Ipo haja ya kujua maeneo ya migodi kwenye mikoa tofauti, nna ambition ya kutembelea maeneo kabla sija settle sehemu, hii nimesha iwekea bajeti, nnajua na nimeshapitia baadhi katika mi,koa ya Tabora na Shinyanga, mwenye kuweza kuataja vitongoji vingine vya mikoa mingine, kama mbeya na mpanda nk, tafadhali.
 
Singida ,dodoma, kilindi kuna dhahabu pia..vika na huko.

#MaendeleoHayanaChama
 
Tatizo nnaloliona mimi kwa muwekezaji ni uchimbaji, ukiwa mchimbaji michirizi inasumbua sana mara ipo mara haipo, afu maponcha wenyewe hawapo sirias, time yoyote akijisikia kuhama ana hama, bora kua na vifaa nakuwafanyia kazi watu kufukuzia kifusi, ndio maana naona umuhimu wa kutembelea maeneo kuona wapi kuna shortage ya vifaa.
 
Njoo geita kuna sehemu moja mpya
 
Hongera, Una connection na watu wanaouza madawa ya kulipua?
Salam zangu na zisambae kwenu nyote. Matumaini yangu mu buheri wa afya tele, na hata walioteteleka mwenyezi Mungu awajaalie wepesi wa kupona haraka.

Ahadi ni deni. Nami tangu nimeanza mbio zangu za kibiashara kwenye madini ya Dhahabu nimekuwa na tendency ya kuripoti wapi nimefikia kila baada ya miezi sita. Niliwahi kuja na post ya mrejesho first season Mrejesho: Biashara ya madini aina ya dhahabu

baadae nikaleta second seoson Mrejesho biashara ya madini ya dhahabu second season

Na sasa naileta 'third season'. Labda nianze kwa kusema kuwa watu wengi wananifuata pm kutaka kuonana na Mimi. To be honest, siko tayari kuonana na mtu ila kama utahitaji msaada mwingine wa maelekezo nitakujibu. Nafanya hivi kwa sababu hatujuani, nami sitaki kumulikwa kihivyo.

Baada ya kununua Karasha mwezi may 2021, nikitumia takribani 11mil, nilibakiwa na mtaji wa kama 12 millions. Kwa ukanda wetu huku huwa tunasaga mawe bure, hivyo ni kuhudumia tu yaani unanunua diesel mwanzo mwisho hela ukitoa mfukoni.

Kazi ya kusaga mawe nilianza kwenye tar 10 may hivyo Sasa nimekamilisha miezi sita. Nilipata sehemu ya kuchimba mawe kwenye mgodi wa rafiki yangu. Huwa naajiri watu nawalipa kwa mwezi wanafanya kazi ya kutoa mawe baada ya kulipua. Mawe hayo huwa nagawana na mwenye mgodi yeye akichukua 40%, Mimi nachukua 60% ya mawe. Kisha huwa nayabeba na kwenda kuyasaga karashani kwangu.

Saivi rudio limekuwa kubwa nakadiria gari za tani kumi 20. Sampo nikipima maabara inasoma 8ppm na zaidi. Mpaka saivi natoa faida kwenye biashara ya Dhahabu nahudumia Karasha, na Sasa nataka mlima uendelee kukua hadi mwakani mwezi may.

Changamoto ni pesa ya mtaji imezidiwa na matumizi ya Karasha kwani inapungua siku hadi siku. Kwa hiyo nitapambana kwa namna yoyote ili hadi kufikia mwakani mwezi wa sita nichenjue mlima.... Na hapo nikipata angalau kilo mbili za Dhahabu, nitapambania lessen ya u dealer. Na hapo nitaianza rasmi safari ya kuusaka ubilionea.

Vijana wenzangu wakike na wakiume ni wakati sahihi sasa wa kuamua kuzifuata ndoto zako. Wengi tunashindwa kuingia kwenye fulsa za biashara kwa kuamini kuwa hatuna mitaji. Nikwambie tu mtaji ni kitu kidogo sana kwenye biashara. Unaweza uwe na mtaji na ushindwe kufanya biashara ikakua. Hivyo kitu kikubwa kwenye biashara lazima uwe na confidence na utashi wa kuifanya hiyo biashara.

Nitoe mfano wa binti mmoja nimemfahamu anaitwa Diana (jina la uongo). Alikuwa anafanya biashara ya kujumua pombe kali anapeleka migodini.

Alikuwa anafuata mpakani Tunduma anakuja kuuza Chunya. Alianza na mtaji wa laki na nusu tokea 2019. Diana alifanya biashara hiyo kwa miezi saba akawa na hela kama laki 9. Akaamua kuongeza vitenge kwenye kufunga mzigo. Bahati mbaya siku moja akiwa kwenye usafiri gari ilipata ajali akavunjika mguu. Alitumia pesa karibia yote aliyokusanya kujiuguza.

Mpaka anapona alikuwa amebakiwa na kama laki mbili tu. Mguu ulipona vizuri. Alichofanya Diana aliamua kubadilisha biashara, alikodi fremu akafungua genge la mbogamboga. Amefanya biashara hii kwa mwaka, ikamlipa maradufu.

February ya mwaka huu alifungua grocery karibu na pale anapouzia mbogamboga. Bia ambazo zinauzwa 2500 bar yeye anauza buku jero. Savi mwezi November ameongeza duka la mitumba hapohapo karibu.

Nimemtolea mfano Diana kuonyesha ni jinsi gani unaweza kuwa na ndoto kubwa ya kumiliki benki, ukaanza na sh elfu hamsini kuitekeleza ndoto yako.

Panapo majaaliwa tukutane tena June 2022 hapahapa kupeana update.
 
Ipo haja ya kujua maeneo ya migodi kwenye mikoa tofauti, nna ambition ya kutembelea maeneo kabla sija settle sehemu, hii nimesha iwekea bajeti, nnajua na nimeshapitia baadhi katika mi,koa ya Tabora na Shinyanga, mwenye kuweza kuataja vitongoji vingine vya mikoa mingine, kama mbeya na mpanda nk, tafadhali.
Mbeya Chunya yote wanachimba kuanzia mlima njiwa, sangawale, mapogoro, mbigwa, makatang'ombe, itumbi, matondo, makongolosi, matundas, mkwajuni mpaka saza karibu na ziwa Lukwa etc.
 
Back
Top Bottom