Mrejesho baada ya kuagiza Gari toka Japan

Walikujaza upepo ty ili uendelee kuw mteja wao... Kiufupi autocom hiyo dsicount ndio wanayotoaga, maana ukiji register tu wanakuoa discount ya dola 100, na baada ya hapo kuna discount ya dola 300 hiyo ni uhakika ndio inakuja hiyo 400! Baada ya hapo utaendelea kula disc za dola 300! Jamaa wapo vizuri gari zao nzuri na bei ni cheap sana! Mm ninayotumia pia nilichukua kwao! Kuagiza ni uoga tu wa watu.. Hongera sana mkuu

 
Mimi Nimetembelea web yao jana nikaona bei yao iko juu kidogo. Magari mengine hawaandiki bei mpaka uulize. Mbaya zaidi wana magari machache sana. Ila magari yao mengi yako kwenye hali nzuri.

Wana gari chache kweli
 
Wakuu salama?

Kwanza kabisa niwashukuru wanajukwaa hili kwa ushirikiano mzuri mlionipa kabla sijaagiza chombo.

Nilikua sina uzoefu wa kuagiza hivyo ilikua mara yangu ya kwanza lakini nilifanikiwa na chuma ilifika imenyooka sana.

Nilitembelea kampuni Nyingi sana za japan kama Beforward, sbt, enhance, trust, autocom na real motors.

Nilitumia kama week mbili kutafuta gari lengo ilikua kwaajili ya wife hivo alikua anataka pearl white. Beforward niliona gari za kawaida na kama ukipata imenyooka bhs na bei imenyooka pia, SBT gari zao ni za kawaida sana na nyingi zmeenda mileage.

Nikatembelea trust na enhance kiukwel hawa wanagari kali sana hata bei zao zmenyooka pia. Mwisho wa siku nikatembelea AUTOCOM JAPAN hawa watu wana gari kali sana afu bei poa.

Baada yakupata gari tunayotaka nika regsta mjapan akanichek whatsapp akajitambulisha japo sikumzingatia nikamtumia ist tuliyoipenda ilikua $2620 C&F tukabargain mpaka $ 2220 so alinipa discount ya $400. Gari ilikua Auction Grade 4

Asbh akanichek anitengenezee invoice nikakubali niliwaza nikiikosa ndo bhs gari nzuri macho huwa mengi. Akanitumia kwa whatsapp japo nilikua simwamini kabisa nikampiga piga maswali nikawashirikisha watu nikaenda mpaka ofisi zao posta pale wakasema iko sawa nilipie tu na mjapan wanamjua ndo sales officer mkuu na walishangaa discount kanipa kubwa sana hata wao huwa hawapewi so ilikua baht tu.

Utaratibu wa kulipia autocom ni unafanya international transfer (TT) yani unaweka cash kwenye A/c yako then wanatransfer kwenye account yao japan ili kuepusha third parties hawataki pesa ishikwe mkononi.

Nililipia 06/04 nakumbuka kesho yake akanichek akasema muamala ameuona so anaanza na inspection na kutafuta space kwenue shipping lines.

Nilisubir kama siku 50 mpaka naipata gari bandarini. Nikipiga hesabu gharama ya gari, kodi na clearing nmetumia kama 12.5 million

Gari kwa kweli nilivyoiona kwa macho laivu ni kali tofauti na inavokua mtandaoni gari imenyooka battery iko safi, engine fresh, imekuja na fog, spare tyre nilichobadilisha ni oil na filter na airfilter bhs. Gari ni inachanganya fasta haili mafuta iko gud sana. Gari imefika ina 66,000 mileage.

View attachment 1861492


Siendi tena yard/ showroom gari naagza japan, shida uwe mvumilivu bhs kama unaharaka nenda showroom.

View attachment 1861493
Autocom Japan
Mbona kama wana uhaba sana? Nikimaanisha wana gari chache sana?
Nimesearch Toyota Rav 4, min year 2008, max year 2015.. Hakuna gari hata moja!!
Au nimekosea kusearch?
 
Yan mi ya kwangu mkuu ni kwamba ya TRA kwa mwezi huu imepungua kuliko ilivokua mwanzo sasa basi uyu wakala wangu badala ya kusema wameshusha yeye ananambia wamepandisha.

Wewe apo ata sasa ivi ingia TRA calculator ist ya 2006 ni sh ngapi ? Itakupa ni 6.1m wakati mwanzo ilikua 6.6m sijui inanielewa?...

Kwa kifupi jamaa kaingia cha kike kwangu kmmk
Mkuu , pamoja na ushuru kushuka ila Tra wanaangalia na invoice utakayopeleka, kama agent alijichanganya akapeleka invoice ambayo ipo juu ya base price kwenye calculator , Tra watatu mia invoice yako kukupatia kodi yako. Na hii ndo sababau ya kodi ku overshoot .
 
Kaka asubuhi hii..
Nimemkuta mshikaji na nafikiri alivoniona tu akajua sikuja vema ivo alikua mpole sana..

mosi.. alisema ushuru umepanda ni uongo akasema walikosea TRA kumwambia
Pili sasa akaanza sound pale port clearance imepanda...
TBS imepanda..
-usajir wa kupata no umepanda
-Yan ivo vikorombezo vyote vya kwenye profoma invoice vimepata ikabidi nitoe kwanza embassy cigarette nivute...nipomaliza nikamwambia bro unajua mpk nanunua hii gar nimedunduliza toka miaka mitano nyuma nipo chuo so nakupa pesa tuliongea awali na ninakata ya ushuru iliyopungua TRA nikamuhesabia hapo hapo nikampa mpunga nikamuuliza saa ngapi niijie gar akasema jion ntakupigia.. Nikasepa ntareta jion mresho na ndinga
😅😅
Baba ulirudi jioni?
 
Mkuu , pamoja na ushuru kushuka ila Tra wanaangalia na invoice utakayopeleka, kama agent alijichanganya akapeleka invoice ambayo ipo juu ya base price kwenye calculator , Tra watatu mia invoice yako kukupatia kodi yako. Na hii ndo sababau ya kodi ku overshoot .

Ok nashukuru kwa maelezo lkn mbona wametumia ya mwezi huu iliyoshuka ma agent uwa wanawapiga tu... wala invoice haipelekwi Uko TRA....
 
Sure, nenda yard afu leta mrejesho kaka

Achana na yard ujanja ni kuagiza gar ya mwaka 2002 tofaut na 2004.... 2005 tofaut na 2006 kuanzia bei mpk ushuru mkuu we umeagiza af hujui hizi mambo ama wewe ulipick tu moja iyo iyo.....izo rim ni size ngap nikitaka gar iwe jujuu kidogo tyre size ngapi.?
 
Back
Top Bottom