Mrejesho: Anatumia bracelet aliyopewa na mama yake aliyekufa asipate mimba, kapata mimba nifanyaje?

Karimu123

JF-Expert Member
Aug 3, 2015
244
114
Wakuu Habari zenu Natumain Mko Njema kabisa Nimerudi tena Wadau Ikiwa ni Kama Mwezi Umepita Baada ya Kuleta Tatizo langu la Anatumia bracelet aliyopewa na mama yake aliyekufa asipate mimba, kapata mimba nifanyaje?

Baada ya Kumchunguza sana huyu binti Aligoma kabisa Kufunguka zaidi sasa Leo Amenipa Msg Ambayo Imenifanya nianze kuamin maneno ya Mkuu sonnita nakukuu Msg zake nitatumia Jina sio Halisi

''Najisikia Naumwa Sana na Tumbo nataka kwenda Hospital kucheki inawezekana Mtoto kafia Tumboni''

Nilimjibu sawa utanijulisha basi majibu yatakavyo kuwa baada ya mda kama lisaa hivi aanisms akanimbia

''Hawana Jipya Hawa wanasema ni kawaida tumbo kuuma kipindi cha mwanzo mtoto yuko vizuri sana na ana miez miwili wiki moja na siku tano''

Nizungumze Ukwel nilikutana kimwili na huyu bint tareh 25 mwezi wa saba tarehe moja aliniambia ana ujazito wangu wa siku 11 sasa leo ndo nimeanza kumtilia mashaka kabisa ananibambikizia ujazito ukupiga mahesabu ya haraka haraka ni siku 44 sawa na mwezi na week 2 sasa wakuu nimerudi tena je nimwache nimwambie ukweli kuwa hiyo mimba sio yangu au nikaushe niendelee kumfariji hadi mtoto azaliwe niangalie mahesabu siku

CC sonnita nakushukuu sana mkuu mungu akujalie mume mema unaakili kama redio ya mkoloni I owe you Alot Dear...
 
Last edited by a moderator:
kama ulipiga dry sioni sababu ya kukataa mimba at this stage... subiri ajifungue ukapime dna kama unawasiwasi!!!
matumizi ya condom ni mazuri kwa maendeleo yako... hasa kama unatabia ya kukataa mimba
 
Pole sana!!ila fanya kumfariji mpaka ajifungue den ukishapma DNA kila kitu kitakuw wazi na ndo utaamua nn ufanye
 
Dogo bora ungepelekwa jeshini tuuu kuliko kubaki mtaaani....

Huo Ujinga Ndo sifanyi Kabisa Heri Nimebaki nina Million tatu sasa kwa miezi hii mitatu nilikaa nyumbani mfano ningeende ningezinyea wap hizi hela...japo kuna mabalaa kama hili limenitokea namshukuru mungu atanisaidia niliepuke
 
Pole sana!!ila fanya kumfariji mpaka ajifungue den ukishapma DNA kila kitu kitakuw wazi na ndo utaamua nn ufanye

Mkuu swala la DNA nasikia ni mambo ya Kuputia kwa Mkemia mkuu wa Serikali alafu kuwe na mambo ya Mahakani tena sasa napiga hesabu za haraka haraka sio chini ya Laki Tano hapo
 
mahesabu unajua,ila kondomu ndo huvai

Binti Mwenywew alikataa alisema mafuta ya Kondom yanamumiza alikuwa patashika nguo kuchanika jaribu kucheki uzi wa nyuma nimweka link hapo juu utajua kisa chote huu ni muendelezo tu mkuu
 
kama ulipiga dry sioni sababu ya kukataa mimba at this stage... subiri ajifungue ukapime dna kama unawasiwasi!!!
matumizi ya condom ni mazuri kwa maendeleo yako... hasa kama unatabia ya kukataa mimba

Thank You Boss ttz la kutotumia kinga siku hiyo alilama sana kuwa mafuta ya kondom yana muumiza sana ndo maana nikaacha ila nikuwa nimebeba zangu kila kitu ilikuwa patashika nguo kuchanika nikasema isiwe kesi nkachapa
 
Amka ulitegewa mimba, mchane live kabla haijakuwa ili mjue la kufanya badala ya kukaa kimya halafu uje umkatae baadae.
 
Wewe hujui kuwa kitanda hakizai haramu? Huyo ni mwanao bwana, unless mlizini sakafuni ama kwenye gari.
 
Huo Ujinga Ndo sifanyi Kabisa Heri Nimebaki nina Million tatu sasa kwa miezi hii mitatu nilikaa nyumbani mfano ningeende ningezinyea wap hizi hela...japo kuna mabalaa kama hili limenitokea namshukuru mungu atanisaidia niliepuke

Sasa kumbe unapesa alafu unalia lia kama mtoto...we wakiume subir mtoto azaliwe alafu ukapime...
 
Sasa kumbe unapesa alafu unalia lia kama mtoto...we wakiume subir mtoto azaliwe alafu ukapime...

Mkuu tuzungumze tu ukweli wew uko tayari kuona unapoteza pesa inapotea kwa kitu ambacho huna uhusika nacho?isitoshe mkuu swala la DNA lina process elfu sita sijui mkemia mkuu sijui mwanasheria huko kote tunazungumzia kunyoosha mkono aisee hata kama
 
Back
Top Bottom