Mratibu wa mradi kigamboni vs katibu mkuu ardhi (Patrick Rutabanzibwa)

Hivi Magufuli alivyotua pale Ardhi wafanyakazi walimfurahia au La?

Ukipata jibu basi linganisha!
 
Kumbukumbu zangu zataka kurudi kwenye National ID Hivi ali handle vipi? Huyu bwana R'Banzibwa
 
km wa ardhi bw.rutabanzibwa,huyu mtu nikero kubwa sana wizarani kwake kila mfanyakazi analalamika na hata wananchi,toka ameamia pale wizarani inasemekana miradi yote ya maendeleo imesimama,kama mradi wa peri-urban development,20,000plot,na sasa anataka kuua mradi wa mjimpya kigamboni.

wafanyakazi wa wizara ya ardhi lazima walalamike mana wamezoea kuishi kwa rushwa na ufisadi! Hakuna cha miradi ya maendeleo ni miradi ya kula rushwa tu,lazima wamchukie sijui kama kina wizara iliyobingwa kwa rushwa kama wizara ya ardhi, double allocation uuzaji wa open spaces wao uchakachuaji wa hati ni wao kila ufisadi wao tu!

ni lazima hii miradi bomu isimame, kwa kuwa ilikuwa ni wizi mtupu. Kama vile luguruni watu wanatoka wizarani kwena hapo luguruni kibamba wanalipana posho za safari wakati luguruni kibamba ni willaya ya kinondoni. Mradi wa luguruni ulitumia bilioni tatu kwa ajili ya fidia wakati wananchi walilipwa si zaidi ya milioni 700, zingine zilikwnda wapi. Patrick rutabanzinbwa amesimamisha miradi hiyo hadi waote waliohusika na wizi wajulikane.
 
umakini wa namna gani ?kutia taifa hasara..!mradi wa 20,000plot uligarimu serikali mabilion ya fedha kabla haujakamilika nakurudisha garama na faida jamaa ameusimamisha,peri-urban hivyo hivyo fedha zimetolewa na worldbank na serikali lkn hakuna matunda!kwanin asiwafichue hao mafisadi kusimamisha miradi ndio kutimiza lengo la maendeleo?naomba tulifikirie hili swala kwa mapana zaidi sio kuangalia ufisadi tuu ..je amesaidia vp kufikiwa kwa malengo ya mradi?

MRADI WA VIWANJa 20000, ULIANZISHWA NA KATIBU MKUU ALIYEPITA SLAOME SIJAONA, ALIMDANAGANYA RAIS MKAPA KWA KUWA SEIKALI HAINA FEDHA ZA KUPIMA VIWANJA AKUBALI KUIRUHUSU WIZARA YA ARDHI KUWATOZA WANANCHI FEDHA KIDOGO KUFIDIA GHARAMA ZA UPIMAJI ILI VIWANJA ZAIDI VIPIMWE. KUTOKANA NA UFISADI MKUBWA ULIOJITOKEZA MIONGONI MWA WATUMISHI WA WIZARA MRADI HUO UKAGUEUKA KUWA CONDUIT YA KUWATENGENEZEA UMASIKINI WANANCHI WA MASKINI WALIONYANGANYWA ARDHI ZAO KWA FIDIA KIDUCHU. WATUMISHI WA WIZARA YA ARDHI WAKAJILIMBIKIZIA IDADI KUBWA YA VIWANJA VILIVYOPIMWA NA HUVIUZA KWA BEI YA JUU SANA. WANANCHI WALIOKUWA WAKIMILIKI ARDHI NA KUITUNZA KWA MIAKA YOTE WAMEBAKI MASKINI WA KUTUPA HADI LEO HII HUKU WATUMISHI HAO WAKICHUMA MABILIONI YA SHILINGI KW AKUTUMIA ARDHI WALIOWANYANG'ANYA WANANCHI KWA KUTUMIA MGONGO WA SERIKALI WAKIDAI NI KWA MASLAHI YA UMMA. ILITAKIWA WIZARA IPIME VIWANJA NA KUWAACHAIA VIWANJA HIVYO WANANCHI WALIOKUWA NA ARDHI HIYO WAUZE WENYEWE VIWANJA HIVYO.

BIG UP PATRICK SIMAMISHA KILA AINA YA UFISADI HAPO WIZARANI!!!!!!!!!!!!
 
sisi wakazi wa kigamboni infact hatuna shida ya mradi huu. Mradi huu hautuhusu kwa vile tunachokiona ni hata kile kidogo tunachomiliki kinaweza kudhulumiwa.
 
JAMANI LEO NIMEONA KITU CHAKUSHANGAZA SANA KTK MKUTANO WA WAZIRI WA ARDHI KUHAMASISHA UENDELEZAJI WA MJI MPYA KIGAMBONI.KUNA KIKUNDI KILICHOJUNDA NAKUJITAMBULISHA NI WAWAKILISHI WA WAKAZI WA KIGAMBONI,HAWA WATU WANAPATA SAPORT KUBWA KUTOKA KWA KM WA ARDHI Bw.RUTABANZIBWA,HUYU MTU NIKERO KUBWA SANA WIZARANI KWAKE KILA MFANYAKAZI ANALALAMIKA NA HATA WANANCHI,TOKA AMEAMIA PALE WIZARANI INASEMEKANA MIRADI YOTE YA MAENDELEO IMESIMAMA,KAMA MRADI WA PERI-URBAN DEVELOPMENT,20,000PLOT,NA SASA ANATAKA KUUA MRADI WA MJIMPYA KIGAMBONI..MH.RAIS ALIPOTEMBELEA WIZARA HIYO MAPEMA MWEZI HUU ALISIFIA SANA HATUA ILIO FIKIWA KTK KUENDESHA MRADI..JAMBO HILI LILIONEKANA KUMKERA SANA BW.RUTA,IKAFIKIA HATUA YA KUTAKA KUMHAMISHA MRATIBU WA MRADI HUO BW.MTUI NA KATIBU WAKE BI.MPETULA,MADIWANI WA KIGAMBONI WALIPINGA SANA HII ATUA..CHAKUSHANGAZA LEO KTK KIKAO KUNABAADHI YA WATU WALIBEBA MABANGO KUMPINGA BW.MTUI KWAMBA ANAUZA VIWANJA KIGAMBONI BILA USHAIDI WOWOTE,HII NI MBINU YA BW.RUTA KUHALALISHA NIA YAKE MBELE YA MADIWANI. KWA HALI HII KWELI TANZANIA ITAPIGA HATUA YA MAENDELEO KAMA KUNA WATENDAJI WAKUU WANARUDISHA MAENDELEO NYUMA KIASI IKI? WAKAZI WA KIGAMBONI WANASEMA HAWATAMBUI KUWEPO KWA KIKUNDI HICHO KAMA WAWAKILISHI WAO..TUSHAURIANE WADAU!

Mtoa mada... Pole sana kwa kuwa frustrated na Bwana Rutabanzibwa, ukiwa kama mmoja wa wengi wanaopenda vitu vya mkato na mambo ya valuvalu lazima ikuume

Wizara ya ardhi ilikua inanuka rushwa na bado inanuka rushwa, katibu mkuu kaja kaanza kwanyima ulaji na inawauma

  • tuanze mradi wa kibamba... kiko wapi? waliobomoa makazi ya watu, wakalipana kinyemela sasa hivi ni mwendo wa kesi tu, you know why? corruption
  • Viwanja vilipimwa mwongozo (kigamboni) miaka zaidi ya minne... hadi leo wanauza kinyemela kwani wanaficha vouchers (mnauza 8-15M kiwanja chenye vocha ya sh. 2.3M) na hilo amegundua sasa mnauza kwa shida - reason corruption!!
  • Miradi ya viwanja 20,000 hamjiulizi kwanini hakuna ujenzi active?? ni wkasbabau watu walijilimbikizia viwanja, endapo vingeenda kwa wanaohitaji kweli basi tungeona ujenzi... HUU NI UHUJUMU UCHUMI

Ningekua JK... ningempa rutabanzibwa sapoti zaidi
 
Hivi huu mradi upo kweli au changa la macho? hadi hivi leo watu wanajenga majumba kwa kasi ya ajabu, by the time mradi huu unaanza sijui watabomoa majumba yote hayo?

Hii nchi mipango mingi utekelezaji sifuri, mimi nina heka zangu tatu pale kibada nimeanza kujenga ghorofa waje walibomoe, nilishajichokea na mipango ya nchi hii.
 
KM WA ARDHI Bw.RUTABANZIBWA,HUYU MTU NIKERO KUBWA SANA WIZARANI KWAKE KILA MFANYAKAZI ANALALAMIKA NA HATA WANANCHI,TOKA AMEAMIA PALE WIZARANI INASEMEKANA MIRADI YOTE YA MAENDELEO IMESIMAMA,KAMA MRADI WA PERI-URBAN DEVELOPMENT,20,000PLOT,NA SASA ANATAKA KUUA MRADI WA MJIMPYA KIGAMBONI.

Wafanyakazi wa Wizara ya Ardhi lazima walalamike mana wamezoea kuishi kwa RUSHWA NA UFISADI! Hakuna cha miradi ya maendeleo ni miradi ya kula rushwa tu,lazima wamchukie sijui kama kina Wizara iliyobingwa kwa rushwa kama wizara ya Ardhi, Double Allocation uuzaji wa open spaces wao uchakachuaji wa hati ni wao kila ufisadi wao tu!

Hao wanomchukia Ruta hapo wizarani,watueleze vyema anawanyima nini?
pia hiyo miradi like 20,000plots mimi ni muathirika nayo kwani toka vipimwe na kuwekwa michoro ya barabara mpaka leo hakuna ukarabati,maji,umeme nk kama walivyotueleza wakati wa kununua kwamba kila kitu kitakuwepo.

sasa huyu Ruta anahusikaje kwalo?
 
Hao wanomchukia Ruta hapo wizarani,watueleze vyema anawanyima nini?
pia hiyo miradi like 20,000plots mimi ni muathirika nayo kwani toka vipimwe na kuwekwa michoro ya barabara mpaka leo hakuna ukarabati,maji,umeme nk kama walivyotueleza wakati wa kununua kwamba kila kitu kitakuwepo.

sasa huyu Ruta anahusikaje kwalo?

Patrick Rutabanzibwa kwa wanaomjua ni Kiongozi Makini. Tunaloshuhudia hapa ni kutapatapa kwa genge la mafisadi na makuadi wao wa Ardhi ambao amewakalia vibaya kooni. KM Patrick anasimamia haki na aendelee hivyo. Bahati ana Waziri makini hivyo mafisadi wa ardhi ni bora muachie ngazi mapema badala ya kuhamishia mapigano JF. Tuwakatae kwa nguvu zote.
 
pale tunapo jaribu kuzuia ruswa na kujikuta tunazuia maendeleo ndio hatua inapofika nchi inakuwa na sera nzuri sheria kali na kila mwananchi ni mwadilifu lakini hakuna maendeleo,jana nilipenda sana kuuzuria kile kiako cha wizara na sisi wakazi wa kigamboni..chaajabu na ambiwa na jirani zangu walio uzuria Bw.Rutabanzibwa hakufika,pia mh.waziri wa ardhi bi.tibaijuka alionekana kuhafiki kuitambua kamati isio rasmi inayo jiita wawakilishi wa kigamboni(sisi wananchi hatuwatambui kwakuwa hatukuwachagua)ungozi tunaotambua ni madiwani na serikali za mitaa kama wawakilishiwetu.Hii inaonyesha jinsi gani awa WAHAYAA wananvyo taka kdhorotesha maendeleo ktk mjiwetu.
 
Wewe umetumwa na mafisadi na unaonekana humjui Ruta ni mzalendo wa kweli kati ya viongozi wachache tulionao hivi sasa, rejea sakata la vitambulisho vya taifa alipoweza kupambana na aliyekuwa boss wake Waziri wa mambo ya ndani Laurence masha hadi Masha akasalimu wakati huo Ruta alikuwa katibu mkuu wa wizara hiyo. Ruta ni mwadilifu kama amestukia jambo katika mradi wa kigamboni mimi nina imani naye naomba sote tufuatilie lakini nilichotaka kukujulisha tu kwamba Ruta ni mpambanaji kama kutakuwa na uozo kauona katika mradi huo.

Lakini pia Ruta sio mwenye kauli ya mwisho kwenye mradi huo kwani kuna waziri wake mama Tibaijuka naamini hataonewa mtu lakini kwa mama huyu chonde chonde wale wote wanaotaka kujinufaisha kupitia mradi huu badala ya wananchi wa kigamboni na taifa kwa ujumla wamekutana na visiki safari hii. Mradi huu ni wa wananchi sio wa Mtui wala Ruta tunachotaka ni manufaa kwa taifa letu.
 
Wewe umetumwa na mafisadi na unaonekana humjui Ruta ni mzalendo wa kweli kati ya viongozi wachache tulionao hivi sasa, rejea sakata la vitambulisho vya taifa alipoweza kupambana na aliyekuwa boss wake Waziri wa mambo ya ndani Laurence masha hadi Masha akasalimu wakati huo Ruta alikuwa katibu mkuu wa wizara hiyo. Ruta ni mwadilifu kama amestukia jambo katika mradi wa kigamboni mimi nina imani naye naomba sote tufuatilie lakini nilichotaka kukujulisha tu kwamba Ruta ni mpambanaji kama kutakuwa na uozo kauona katika mradi huo.

Lakini pia Ruta sio mwenye kauli ya mwisho kwenye mradi huo kwani kuna waziri wake mama Tibaijuka naamini hataonewa mtu lakini kwa mama huyu chonde chonde wale wote wanaotaka kujinufaisha kupitia mradi huu badala ya wananchi wa kigamboni na taifa kwa ujumla wamekutana na visiki safari hii. Mradi huu ni wa wananchi sio wa Mtui wala Ruta tunachotaka ni manufaa kwa taifa letu.
Mradi sio wa MTUI au RUTA,ila kama watendaji wakianza kutofautiana inakuwaje sisi wananchi tusipatwe na wasiwasi na wale wanaosema huu mradi hauna manufaa kwa kigamboni wamechelewa sana,nawashauri watembele wiazara ya ardhi nakujua umuhimu wa mradi kwa taifa na wakazi wakigamboni..rais alisifia sanaa juhudi zilizofikiwa,Ruta hakufurahishwa na kitendo icho hali inayopelekea kudhorotesha utendaja,kama yeye ni mtendaji kweli alipaswa awashuulikie hao mafisadi na kuakikisha malengo ya miradi yanafikiwa..sio kuiua miradi na kuamisha watumishi..mm nadhani huyu bwana sio mpenda maendeleo ila ni mzuia maendeleo na yoyote anaye mtetea basi ana maslai kwake, katika orodha ya mafisadi wa CHADEMA ameshika nafasi ya saba.
 
Elam,

ama wanayoandika wenzio (pamoja na attachement ya Jatropha) huyasomi au huna upeo wa kuyaelewa. Ni dhahiri lakini kwamba wewe ni fisadi uliyeathirika kutokana na utendaji wa Ruta.
 
Ndugu Rutabanzibwa anafanya kazi nzuri pale Ardhi na amewatimua au kuwahamisha maafisa ardhi wengi ambao ni mafisadi. Ni mtu makini sana na hapendwi na mafisadi kwani huzuia ulaji wao.

Rugemeleza
Hata mimi naweza kukuunga mkono kuwa huyu jamaa Rutabanzibwa ni mtendaji mzuri, Kwa mtu yeyote hebu nenda pale ardhi utaona mabadiliko makubwa sana ya kiutendaji kwani kila kitu ni mtandao hakuna eti mafaili kama zamani.

Mwaka jana mwezi wa 10 nilifatilia hati yangu ya kiwanja hakika ilinichukua wiki tatu 3 tu bila hata rushwa, hauwezi kuamini hata kidogo. Mtu unaweza kujiuliza ule ukilitimba wa miaka ya nyuma umeenda wapi? Hkuna rushwa wala mizengwe, pale dirishani kuna watu kama akina Fred hakika ni wachapa kazi.

Nadhani bwana Rutabanzibwa kuhusu huu mradi kuna kitu kagundua na wala si bule

Tujipe muda kuna mengi yatagundulika.
 
Back
Top Bottom