Mratibu wa mradi kigamboni vs katibu mkuu ardhi (Patrick Rutabanzibwa) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mratibu wa mradi kigamboni vs katibu mkuu ardhi (Patrick Rutabanzibwa)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Elam, Mar 31, 2011.

 1. E

  Elam Member

  #1
  Mar 31, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  JAMANI LEO NIMEONA KITU CHAKUSHANGAZA SANA KTK MKUTANO WA WAZIRI WA ARDHI KUHAMASISHA UENDELEZAJI WA MJI MPYA KIGAMBONI.KUNA KIKUNDI KILICHOJUNDA NAKUJITAMBULISHA NI WAWAKILISHI WA WAKAZI WA KIGAMBONI,HAWA WATU WANAPATA SAPORT KUBWA KUTOKA KWA KM WA ARDHI Bw.RUTABANZIBWA,HUYU MTU NIKERO KUBWA SANA WIZARANI KWAKE KILA MFANYAKAZI ANALALAMIKA NA HATA WANANCHI,TOKA AMEAMIA PALE WIZARANI INASEMEKANA MIRADI YOTE YA MAENDELEO IMESIMAMA,KAMA MRADI WA PERI-URBAN DEVELOPMENT,20,000PLOT,NA SASA ANATAKA KUUA MRADI WA MJIMPYA KIGAMBONI..MH.RAIS ALIPOTEMBELEA WIZARA HIYO MAPEMA MWEZI HUU ALISIFIA SANA HATUA ILIO FIKIWA KTK KUENDESHA MRADI..JAMBO HILI LILIONEKANA KUMKERA SANA BW.RUTA,IKAFIKIA HATUA YA KUTAKA KUMHAMISHA MRATIBU WA MRADI HUO BW.MTUI NA KATIBU WAKE BI.MPETULA,MADIWANI WA KIGAMBONI WALIPINGA SANA HII ATUA..CHAKUSHANGAZA LEO KTK KIKAO KUNABAADHI YA WATU WALIBEBA MABANGO KUMPINGA BW.MTUI KWAMBA ANAUZA VIWANJA KIGAMBONI BILA USHAIDI WOWOTE,HII NI MBINU YA BW.RUTA KUHALALISHA NIA YAKE MBELE YA MADIWANI. KWA HALI HII KWELI TANZANIA ITAPIGA HATUA YA MAENDELEO KAMA KUNA WATENDAJI WAKUU WANARUDISHA MAENDELEO NYUMA KIASI IKI? WAKAZI WA KIGAMBONI WANASEMA HAWATAMBUI KUWEPO KWA KIKUNDI HICHO KAMA WAWAKILISHI WAO..TUSHAURIANE WADAU!
   
 2. Gamaha

  Gamaha JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2011
  Joined: Jul 17, 2008
  Messages: 2,694
  Likes Received: 752
  Trophy Points: 280
  Kwa ninavyomfaham Bwana Patric kama anapinga hiyo miradi amenusa harufu ya rushwa.
   
 3. K

  Kleptomaniacs Member

  #3
  Mar 31, 2011
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakazi gani wa Kigamboni wanasema hawaitambui Kamati ya ufuatiliaji wa Mradi wa Kigamboni City? na huyu Ruta anahusika vipi na kamati hii iliyoundwa na waathirika wa mradi huu ambao kwa sehemu kubwa wanachokidai ni kushirikishwa kama wadau?Kama wananchi wana sema jamaa anauza yaweza kuwa kweli wewe unataka ushahidi wa aina gani! kwanini usiwaulize hao wananchi waliokuwa wana mabango wakupe ushahidi, wewe una ushahidi kuthibitisha madai yako dhidi ya Bwn Ruta? let us be serious, JF is for great thinkers not stinkers!
   
 4. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #4
  Mar 31, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kigambu sio tena kwa bush, hebu tuelewesheni vizuri:tape:
   
 5. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #5
  Mar 31, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Hayo ndio matunda ya harakati za kuwatetea wananchi wanyonge wanaoishi maeno pembezoni mwa jiji la dar es salaam zilizoanzia luguruni kibamba katika mradi unaoitwa wa kuendeleza maeno yaliyoko pemebzoni mwa dar es salaam, ulianzia eneo la luguruni kama majaribio
   
 6. W

  Wanji Member

  #6
  Mar 31, 2011
  Joined: Jul 28, 2010
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kama umekurupuka vile. Halafu maandishi yanasumbua kusoma.


   
 7. K

  Kleptomaniacs Member

  #7
  Mar 31, 2011
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu Jatropha upo sahihi kabisa na hiyo attachment big up, hawa wengine hata undani wa miradi hii hawafahamu ama kama wanafahamu basi wana maslahi binafsi! Unaandaliwa mradi ambao matokeo yake ni upokaji wa ardhi na umasikini uliopindukia kwa ndugu zetu wakazi wa maeneo ya pembezoni wakisimama kuandamana na kupinga oh,ati wanatumiwa mbona tunawadharau wenzetu kiasi cha kufikiri hawayaoni yanayotokea?
   
 8. E

  Elam Member

  #8
  Mar 31, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  sijakurupuka..najaribu kukupa latest news,tega sikio kwenye vyombo vya habari leo jioni,au fwatilia kwa makini miradi ya ardhi ilivyo kufa,kama ule wa maji uliokufa akiwa km wizara ya maji..kama ni ndugu yako mwambie sasa wananchi hawata kaakimya..sisi wakazi wakigamboni hatutakaa kimya, tunajua tunachokitaka ktk mji wetu
   
 9. M

  Mkandara Verified User

  #9
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ni Patrick Rutabanzibwa aliyekataa mkataba wa IPTL na akapigwa vita sana hadi akahamishwa na madudu yaliyofuata tukaficha sura zetu..Leo tunalea donda ndugu kwa ubishi wetu..

  Sasa kama kisha unusha mradi wa Bush na ameupinga nadhani tuna muda wa kutosha kumuuliza kwa nini anapinga na kanusa ufisadi gani?
   
 10. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #10
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  kama kuna mtu ametembelea wizara ya ardhi akaona zile picha za mji mpya wa kigamboni atajua fika kuwa ule ni mchanga wa macho. serikali haina hela za kujenga eneo lote lile as shown on the picture, na kama haina uwezo na hawataki kutoa hizo picha basi huu ni udanganyifu kwa wananchi
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  Mar 31, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Ninamjua Patrick, mleta mada ameamua kumchafua

  LAzima nitarudi, mimi nimdau kwenye hili
   
 12. akajasembamba

  akajasembamba Senior Member

  #12
  Mar 31, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 161
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  KM WA ARDHI Bw.RUTABANZIBWA,HUYU MTU NIKERO KUBWA SANA WIZARANI KWAKE KILA MFANYAKAZI ANALALAMIKA NA HATA WANANCHI,TOKA AMEAMIA PALE WIZARANI INASEMEKANA MIRADI YOTE YA MAENDELEO IMESIMAMA,KAMA MRADI WA PERI-URBAN DEVELOPMENT,20,000PLOT,NA SASA ANATAKA KUUA MRADI WA MJIMPYA KIGAMBONI.

  Wafanyakazi wa Wizara ya Ardhi lazima walalamike mana wamezoea kuishi kwa RUSHWA NA UFISADI! Hakuna cha miradi ya maendeleo ni miradi ya kula rushwa tu,lazima wamchukie sijui kama kina Wizara iliyobingwa kwa rushwa kama wizara ya Ardhi, Double Allocation uuzaji wa open spaces wao uchakachuaji wa hati ni wao kila ufisadi wao tu!
   
 13. akajasembamba

  akajasembamba Senior Member

  #13
  Mar 31, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 161
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  KM WA ARDHI Bw.RUTABANZIBWA,HUYU MTU NIKERO KUBWA SANA WIZARANI KWAKE KILA MFANYAKAZI ANALALAMIKA NA HATA WANANCHI,TOKA AMEAMIA PALE WIZARANI INASEMEKANA MIRADI YOTE YA MAENDELEO IMESIMAMA,KAMA MRADI WA PERI-URBAN DEVELOPMENT,20,000PLOT,NA SASA ANATAKA KUUA MRADI WA MJIMPYA KIGAMBONI.

  Wafanyakazi wa Wizara ya Ardhi lazima walalamike mana wamezoea kuishi kwa RUSHWA NA UFISADI! Hakuna cha miradi ya maendeleo ni miradi ya kula rushwa na kuiba hela za nchi tu,lazima wamchukie sijui kama kina Wizara iliyobingwa kwa rushwa kama wizara ya Ardhi, Double Allocation uuzaji wa open spaces wao uchakachuaji wa hati ni wao kila ufisadi wao tu!
   
 14. E

  Elam Member

  #14
  Mar 31, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kama nikweli huyu bwana ni mtendaji..yaliyo jifisha yatajifunua tuu,lakini nadhani ni wakati wa sisi watanzania kuchukua jukumu la kufwatilia maendeleo yetu na sio kuachia viongozi walaji wachache nakuwa na nidhamu ya woga,mradi unawezekana kabisa na utashirikisha wa wekezaji na wananchi sio fedha za serikali tuu...pia watu wengi wana mtazamo hasi juu ya secta ya ardhi na watumishi wake..kwa hilo naomba kila mmoja awasilishe malalamiko yake pale anapoona hakuna haki.
   
 15. kintu

  kintu JF-Expert Member

  #15
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 508
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35

  Ulitegemea wamfurahie wakati ufisadi wanao fanya umethibitiwa....!
   
 16. R

  Rugemeleza Verified User

  #16
  Mar 31, 2011
  Joined: Oct 26, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ndugu Rutabanzibwa anafanya kazi nzuri pale Ardhi na amewatimua au kuwahamisha maafisa ardhi wengi ambao ni mafisadi. Ni mtu makini sana na hapendwi na mafisadi kwani huzuia ulaji wao.
   
 17. U

  Ugweno Member

  #17
  Mar 31, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wabongo hebu tuwe serious kwenye mambo ya msingi sio kuchafua watendaji wazuri kwa maslahi binafsi!hv kwa akili ya kawaida kabisa unategemea watumishi wa Ardhi wanaonuka rushwa watamfurahia Ruta?wewe kama mkazi wa kigamboni kwanini husimuulize Ruta alipokuja kwenye kikao?acheni unafiki waTZ badala ya kupiga kazi ndio maana tunaonekana kuongoza kwa kuamini ushirikina!BIG UP RUTA,WW NI MIONGONI MWA KM TUNAOWAHESHIMU SANA
   
 18. E

  Elam Member

  #18
  Mar 31, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  umakini wa namna gani ?kutia taifa hasara..!mradi wa 20,000plot uligarimu serikali mabilion ya fedha kabla haujakamilika nakurudisha garama na faida jamaa ameusimamisha,peri-urban hivyo hivyo fedha zimetolewa na worldbank na serikali lkn hakuna matunda!kwanin asiwafichue hao mafisadi kusimamisha miradi ndio kutimiza lengo la maendeleo?naomba tulifikirie hili swala kwa mapana zaidi sio kuangalia ufisadi tuu ..je amesaidia vp kufikiwa kwa malengo ya mradi?
   
 19. anti-fisadi

  anti-fisadi JF-Expert Member

  #19
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hivi kweli kuzuia ufisadi ni pamoja na kuzuia miradi endelevu ya serikali? Kwanini huyu Ruta ameshindwa kuweka mipango mbadala ya kuhakiki fedha za miradi amebaki kuzuia utekelezaji wake?? Wewe unaemtetea nawe unajiita thinker??

  Basi mtetee na pinda aliyekataa vx V8 wakati mawaziri wake wanatanua nayo? Huu ndio utendaji wa kibongo sio? Unafki unafki tu..

  Hii nchi haiwezi kuendelea kwa kuwa na viongozi waoga na wavivu wa kufanya kazi zao. Kazi za ardhi ni za field zaidi,ukichelewesha leo umechelewesha masaa ya kutosha ya kazi husika. Serikali haijaajiri watu pale ili wapige desk wakae tu ofisini,hii ni hasara; kwani masaa wanayopoteza yana-cost implication zake baadae.

  Lingekuwa ni shirika binafsi lingekuwa linaelekea kufa,ila kwakuwa wanalipwa kwa hela ya sisi walipa kodi basi wanajibwetesha tu. Ningesema wapumbavu,ila tuache tu
   
 20. k

  kayumba JF-Expert Member

  #20
  Mar 31, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mmmmmh!

  Mdau hivi KM anaweza kufikia hatua ya kupanga watu waandamane (kama madai yao si kweli basi tutasema amewapa pesa) ili tu apate sababu ya kumwamisha MTUI??????????? FIKIRIA TENA!

  Au mdau unajua sababu halisi ni nini na hutaki kutwambia. Kweli sababu ni RUTA kutaka kukwamisha mradi kama alivyozoea? Najiuliza anakwamisha ili iweje? Nimejiuliza swali hili, hivi utendaji wa KM unapimwa kwa mafanikio au kwa mapungufu? kama ni mafanikio sioni sababu ya KM kuamua kukwamisha miradi wakati ni wajibu wake kuhakikisha hiyo miradi inafanikiwa.

  Ningeomba wadau wengine watujuze zaidi juu ya sintofahamu katika mradi wa Kigamboni

   
Loading...