Mratibu wa Kanda ya Pwani wa CHADEMA( TUGARA NI JANGA) (Simung'unyi)

May 5, 2014
92
0
Mimi kama mwanachama wa Kawaida na mkereketwa wa Chadema Mkoa wa Temeke nimefadhaishwa sana na Huyu Mtaribu wa Kanda ya pwani namna anavyoendesha chama na sijui pia waliomteua walitumia vingezo gani mbona ni tofauti na waratibu wengine. Nimekuwa pia nikisikia kutoka kwa wanachama na hasa Viongozi wengi wa Mkoa wa Dar wakimlalamikia kuwa anaua chama na walio mteua wanamuangalia tu.
1. Amekuwa anaficha kadi za Chama na viongozi wa chadema ni msingi wakienda kumomba kadi hatoi ila anagawa katika jimbo analotaka kugombea yeye huko Ukonga.
2. Ofisi ya Kanda ipo Kibaha ila yeye anashinda Makao Makuu wakati Chama kinatakiwa kijengwe maeneo ya pembezoni wa kanda hii hata vikao amekuwa akiitisha Makao Makuu na mara nyingi sisi wanachama na viongozi wa majimbo tumekuwa tukimpnga lakini bila mafanikio pamoja naa yeye kuwa na kiburi kupita kiasi.
3. Amekuwa na Arrogance za ajabu sana kiasi kwamba mpaka viongozi wa majimbo wamekuwa wakihoji je anatoa wapi hicho kiburi maana hafanyi kazi za Chama zaidi ya kujiita Wakili kumbe siyo wakili na habari hizi zimepatikana hivi punde kutoka kwa rafiki jamaa zake wa Karibu na amakuwa akiwadaanganya hata viongozi wake kuwa yeye ni wakili kumbe siyo na kasoma pale Open.( Ingawa uwakili wake hauna uhusiano na ujenzi wa Chama)
4. Kwa kiasi kikubwa tusipo kuwa makini kwa Mkoa wa Dar Chadema tunadidimiza Chama maana mratibu huyu ni tofauti na Waratibu wengine huko Mikioani wamekeuwa wakifanya kazi kubwa sana.
5. Ni rai yangu kuwa tumekuwa tukilalalamika kupitia vikao halali vya chama lakini hakuna chochote kinacho fanyika na Chama tunakipenda labda kupitia majukwaa kama haya viongozi watatuelewa maana mwisho wa siku sisi Canachama tutakata tamaa japo tunakipenda chama.
6.Viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam akina Kileo hakuna hatua walizochukua kabisa juu ya swala hili wakati Chama kinaendela kufa na ningependa viongozi wa juu walichukulie swala hili serious na si vinginevyo kwani karibu viongozi wa majimbo wote hawamtaki sasa je anafanya kazi na nani?.
 
Mikael P Aweda

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
2,933
0
Lord ashburton,
Inawezekana kuna jambo amekukera huyo mratibu lakini mimi nadhani kama wewe ni mwanachama na unataka chama kikue unafahamu utaratibu wa kupeleka malalamiko ili tatizo lako lishughulikiwe kwa mujibu wa katiba, kanuni na miongozo ya chama chetu. Ukiweka hapa JF, jambo rasmi la kichama sana sana unaongeza tatizo kwa washindani wetu wa kisiasa. Nakushauri andika barua ya malalamiko kwa mamlaka husika. Huku JF tupambane na ccm na siyo sisi kwa sisi. Simtetei Tugara kwa kuwa sijui lalamiko lako ila naelezea taratibu, kanuni na jinsi katiba inavyotutaka tufanye.
Hongera kwa kufanya kazi za chama kwa bidii kama maelezo yako yanavyojieleza.
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
20,342
2,000
umeshapeleka malalamiko yako kwenye vikao husika!! au JF ndiyo kikao chenyewe!!
 
MUSSA ALLAN

JF-Expert Member
Oct 13, 2013
18,938
2,000
Lord ashburton,
Inawezekana kuna jambo amekukera huyo mratibu lakini mimi nadhani kama wewe ni mwanachama na unataka chama kikue unafahamu utaratibu wa kupeleka malalamiko ili tatizo lako lishughulikiwe kwa mujibu wa katiba, kanuni na miongozo ya chama chetu. Ukiweka hapa JF, jambo rasmi la kichama sana sana unaongeza tatizo kwa washindani wetu wa kisiasa. Nakushauri andika barua ya malalamiko kwa mamlaka husika. Huku JF tupambane na ccm na siyo sisi kwa sisi. Simtetei Tugara kwa kuwa sijui lalamiko lako ila naelezea taratibu, kanuni na jinsi katiba inavyotutaka tufanye.
Hongera kwa kufanya kazi za chama kwa bidii kama maelezo yako yanavyojieleza.

Mkuu Mikael P Aweda:
Wewe ni mnafiki sana, mara ngapi viongozi wa CHADEMA tena wabunge wanakuja kukashifiana hapa jamvini na hauwashauri hivi? Acha kuwa biased mkuu.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ki-wa-zitto-kabwe-na-suala-la-posho-lema.html
 
Mandla Jr.

JF-Expert Member
Dec 15, 2013
3,101
1,195
Viongozi wengi wa chadema ni majanga, usimuonee yeye tu. Slaa mbona anatumia hela za chama hovyo sana na mmekaa kimya tu. Kwa ujumla cdm ni janga tz.
 
T2015CCM

JF-Expert Member
Sep 13, 2012
7,931

MKUKI kwa nguruwe...mangapi chadema mmeyasemea hapa hapa kwa wale mnaowaona nguruwe, ila nyie wenye thamani sana, binadam ambao hamjazaliwa na mwanamke ndio yenu yakasemwe kwenye vikao??? tumia kichwa kufikiri wewe
 
Tetty

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
26,386
2,000
Mimi kama mwanachama wa Kawaida na mkereketwa wa Chadema Mkoa wa Temeke nimefadhaishwa sana na Huyu Mtaribu wa Kanda ya pwani namna anavyoendesha chama na sijui pia waliomteua walitumia vingezo gani mbona ni tofauti na waratibu wengine. Nimekuwa pia nikisikia kutoka kwa wanachama na hasa Viongozi wengi wa Mkoa wa Dar wakimlalamikia kuwa anaua chama na walio mteua wanamuangalia tu.

Ulitakiwa kumtafuta kiongozi mwingine muhusika na hilo ukamweleze.Hapa wala hautapata suluhisho sana umekiweka CHAMA rehani.Kufanya kosa si kosa kosa ni kurudia kosa.
 
nkongu ndasu

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
22,524
2,000
Tatizo la chadema ni kutoweka system ambayo itasaidia kukieneza chama vizuri, kila kiongozi anaenda kivyake! Mfano operesheni zao nyingi hufanyika mijini badala ya vijijini! Hilo limekuwa ni donda ndugu kwa chama!
 
Highlander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
3,094
1,195
Mkuu Mikael P Aweda:
Wewe ni mnafiki sana, mara ngapi viongozi wa CHADEMA tena wabunge wanakuja kukashifiana hapa jamvini na hauwashauri hivi? Acha kuwa biased mkuu.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ki-wa-zitto-kabwe-na-suala-la-posho-lema.html

Na kama kasome kosa la nyuma anafanya masahihisho kwa kuanza na huyu? Hivi kosa la zamani linahalalisha kosa jipya? lakini jengine ni hili: hapa wanachama wawili wanajadiliana jambo ambali halikuhusu. Pilipili kala Mshamu, wewe Rama zinakuwaje?
 
Mtamile

JF-Expert Member
Aug 2, 2011
2,829
1,750
Ulitakiwa kumtafuta kiongozi mwingine muhusika na hilo ukamweleze.Hapa wala hautapata suluhisho sana umekiweka CHAMA rehani.Kufanya kosa si kosa kosa ni kurudia kosa.

Mkuu Kufanya kosa ni Kosa na Kurudia Kosa ni kuimarisha Kosa
 
bujash

JF-Expert Member
Aug 9, 2013
3,468
0
Viongozi wengi wa chadema ni majanga, usimuonee yeye tu. Slaa mbona anatumia hela za chama hovyo sana na mmekaa kimya tu. Kwa ujumla cdm ni janga tz.

peleka porojo zako lumumba,hapa tunaongelea taratibu na kanuni za chama zinamtaka mwanachama mwenye malalamiko afanye nini? Kama wewe ni mwanachama basi peleka nawewe malalamiko yako panapostahili kwa mujibu wa taratibu na miongozo ya CDM.
 
May 5, 2014
92
0
Lord ashburton,
Inawezekana kuna jambo amekukera huyo mratibu lakini mimi nadhani kama wewe ni mwanachama na unataka chama kikue unafahamu utaratibu wa kupeleka malalamiko ili tatizo lako lishughulikiwe kwa mujibu wa katiba, kanuni na miongozo ya chama chetu. Ukiweka hapa JF, jambo rasmi la kichama sana sana unaongeza tatizo kwa washindani wetu wa kisiasa. Nakushauri andika barua ya malalamiko kwa mamlaka husika. Huku JF tupambane na ccm na siyo sisi kwa sisi. Simtetei Tugara kwa kuwa sijui lalamiko lako ila naelezea taratibu, kanuni na jinsi katiba inavyotutaka tufanye.
Hongera kwa kufanya kazi za chama kwa bidii kama maelezo yako yanavyojieleza.
Ukiona watu tunaweka kwenye mitandao ujue Chama chetu hakina mfumo mzuri wa kutatua matatizo na malalamiko yetu katika mfumo halali mara nyingi tumelalamika tunawachama wengi lakini hakuna kadi amekalia Mratibu hakuna chochote kinachofanyika nadhani kupitia humu jamvim labda watatuelewa. Pia sisi tuilopo chini huku ndiyo tunajua uchungu wa kujendga Chama Kamanda. Ujue pia Viongozi karibu wote wa Majimbo hawamtaki karibu mwaka sasa hakuna kinacho fanyika.Inauma sana
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom