Mramba na Yona, Wakabidhiwa vifaa vya usafi Hospitali ya Palestina

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
Mawaziri wa zamani Basil Mramba na Daniel Yona wameripoti katika hospitali ya Sinza Palestina na kukabiziwa vifaa kwa ajili ya kufanya usafi.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliridhia waliokuwa Mawaziri wastaafu Basil Mramba na Daniel Yona kutumikia adhabu ya kifungo cha nje kwa kufanya usafi katika maeneo ya kijamii ikiwemo Hospitali ya Sinza Palestina.

Hatua hiyo inatokana na Mramba ambaye alikuwa Waziri wa Fedha na Yona aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, kupitia Mawakili wao kuwasilisha barua mahakamani hapo kutoka Magereza kuhusu kutumikia kifungo cha nje.

Mawaziri hao, Jul 6, 2015, walihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela na kulipa faini ya Sh milioni tano, baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 11.7.

Kwa mara ya kwanza washtakiwa hao walifikishwa mahakamani mwaka 2008, wakikabiliwa na mashtaka ya kuisababishia serikali hasara ya kiasi hicho cha fedha kutokana na kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya kukagua madini ya dhahabu ya M/S Alex Stewart ya Uingereza.


IMG-20160208-WA0013.jpg


yona.png
 
Daaah! Natamani niwaone wakiinama na kudeki, hivi hawaruhusiwi kuajiri watu wa kuwasaidia kufanya usafi?
 
Kwa hiyo wamepata nafasi nzuri ya kutumia walicho tuibia.Kweli mahakama ya mafisadi itawafunga kweli hawa jamaa?
 
wale vibaka walioiba kuku na bata ndo wangepewa adhabu km hizi...... hawa majambazi sugu wanatakiwa wapate adhabu pa,oja na kuporwa mali za watanzania
 
Acha ifikie hapo, pamoja na makosa yao yapo pia waliyoyafanya mazuri enzi zao.

Tukitaka tuelewe zaidi tujiulize je kama wafanyakazi hatujawahi kufanya errors katika kutoa maamuzi yetu?!?!?
 
  • Thanks
Reactions: ram
Daaah! Natamani niwaone wakiinama na kudeki, ...
Hata wao wanatamani kudeki kuliko kukaa gerezani, kwa hiyo wewe utakuwa unatamani kitu ambacho mwenzako amekichagua
Mwisho wa siku kila upande utafaidika na kitendo cha wao kupiga deki, wewe utafaidi kuona na wao watafaidi kuwa nje ya jengo la gereza. Wao wana chenji ya yale mahela ila wewe huna, lakini walau unafaidi kuwaona wakipiga deki. Jioni kila mtu anarudi kwao, mmoja ana hela za kufaidi na familia yake na mwingine ana simulizi za kufaidi na familia yake
 
Uisababishie serikali hasara ya bilioni upewe adhabu ya kufagia, uibe kuku ili ana wewe uonje ladha yake kwa kuwa ni maskini umeshindwa kununua hiyo kuku, unafungwa mika mingi halafu jaji anaongeza adhabu kwa kusema na kazi ngumu kipindi akitumikia adhabu, aisee kweli acheni watu wakimbizane kwenye siasa kuna faida nyingi huko.
 
Kwa hiyo taifa hili limepata hasara kwa akili ya hawa watu wawili tu
 
Back
Top Bottom