Mramba na Kimaro wakimbilia kanisani

MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,975
Likes
5,347
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,975 5,347 280
headline_bullet.jpg
Wakutana na wachungaji 42 wa KKKT wala pamoja
headline_bullet.jpg
Waombwa wawapelekee salamu kwa waumini
headline_bullet.jpg
Mramba atamba ni mzoefu wa kesi, ubunge lazimaMramba%20B%281%29.jpg

Mbunge wa Rombo, Basil Mramba.

Kimaro.jpg

Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro

remove.jpg

box_on.jpg

box_off.jpg

add.jpg
Mbunge wa Rombo, Basil Mramba, ametumia fursa ya kuwahutubia wachungaji 42 wa Kanisa la Kiinjili la Kulutheri Tanzania (KKKT) kwa kujitakasa kwamba yu mtu safi na mchapa kazi na kwamba ataendelea kuwa mbunge wa jimbo hilo.
Sambamba na Mramba, pia Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro ambaye aliitisha mkutano wa wachungaji hao ulioanza saa 4:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni, aliwasilisha rasmi maombi ya kutaka wamsaidie kuwasilisha ujumbe kwa waumini wao kwamba anakusudia kuwania tena ubunge katika jimbo hilo.
Katika mkutano huo ambao ni nadra kutokea katika kipindi hiki cha kupanda kwa joto la uchaguzi, Mramba na Kimaro, walitumia jukwaa hilo kujisafishia njia ya kuwania ubunge huku Mramba akitamba hakuna wa kumzuia isipokuwa kama tu Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikimkataa.
Wachungaji hao wanatoka Jimbo la Kilimanjaro Mashariki la Dayosisi ya Kaskazini ya kanisa hilo linalojumisha sharika kutoka wilaya za Rombo na Moshi Vijijini.
Katika mkutano huo uliofanyika makao makuu ya jimbo hilo, Himo, Mramba ambaye aliwasili ukumbini saa 7:00 mchana na kulakiwa na Kimaro, alisema si kila mwanaume anayevaa suruali au mwanamke anayevaa sketi anastahili kuwa mbunge na kuwataka wananchi kuwa makini na watu wanaojipitisha pitisha katika majimbo yao.
Mramba alisema ingawa anakabiliwa na kesi mahakamani ambayo imempunguzia muda wa kuwahudumia wapigakura wake, bado anakubalika katika jimbo lake na hiyo inatokana na jitihada zake za kuwatumikia wananchi kwa moyo wake wote kuhakikisha wanajikwamua dhidi ya wimbi la umaskini.
“Siasa sio kamari, kuwa kiongozi ni lazima uwe na wito fulani ndani yako na vile vile siasa ni kazi mbaya,” alisema bila kufafanua.
Aidha, aliwaponda baadhi ya wabunge ambao kwa sasa wanahaha katika majimbo yao kwa kurudi kuwabembeleza wananchi dakika za mwisho ili hali muda wao wa miaka minne waliutumia kwa kukaa jijini Dar es Salaam na kuishi maisha ya starehe.
“Wabunge wengi hawaendi kwenye majimbo yao kwa ajili ya kufanya mikutano na kujua kero za wananchi, wametoa ahadi lukuki, lakini hakuna walizotekeleza na kwa sasa ndio wanahaha..haya ni mambo ya kutisha sana kwani ni wachache sana wanaopata ubunge na kutatua kero,” alisema.
Mramba alisema viongozi wanaandaliwa na hawaibuki tu kwa kuwa si kila mtu anaweza kuwa kiongozi na kama Mungu amepanga mtu awe kiongozi atakuwa tu hata wanadamu wakiweka vizuizi.
Alisema baadhi ya watu wanadhani kuwa mbunge ni mtu mwenye uwezo bila kujua kuwa mbunge ni yule ambaye ana nia ya dhati na uwezo katika kuwakwamua wananchi kwenye lindi la umaskini.
Alisema aliteuliwa na Mwalimu Julius Nyerere kama mbunge wa kuteuliwa miaka ya 80 ambapo alitumia miaka mitano kujifunza na baada ya hapo alikuwa mzoefu na kwamba kila mara anakumbuka kauli ya Mwalimu Nyerere iliyomwambia ‘mimi nastaafu ila wewe baki Rombo wasaidie wananchi wa Rombo’jambo ambalo amekuwa akilifanya hadi sasa.
Alisema kuwa yeye ni mzoefu katika utumishi wa umma na ubunge na amefanya kazi na marais wote wa awamu nne.
“Dunia ina watu wazuri na wabaya, tunaishi nao na tunafanya kazi nao, mimi ni mzoefu wa kushtakiwa na hilo halinikatishi tamaa ya kuwatumikia wananchi wangu ambao bado wana imani kubwa na mimi,” alisema Mramba.
Mramba anakabiliwa na kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya matumizi mabaya ya madaraka wakati akiwa Waziri wa Fedha kwa kutoa msamaha wa kodi kwa kampuni tanzu ya Alex Stewart (ASSAYERS) na kuisababishia serikali hasara ya Sh. bilioni 11.7.
Akimzunguzia mbunge huyo, Mchungaji Elias Sillayo, alisema alimfahamu miaka ya 80 akiwa usharika wa Mengwe na kwamba wananchi bado wanamuhitaji na wanaomba kesi yake imalizike haraka ili aendelee kuwatumikia.
Naye Kimaro akizungumza na wachungaji hao alisema utumishi wa umma si fursa ya kunufaisha mtu binafsi, rafiki, wapambe na si fursa ya kutukuza itikadi za kisiasa.
Alisema utumishi wa umma ni dhamana na fursa adimu kwa ajili ya kulinda na kutetea maslahi ya wananchi wote.
Kimaro alisema daima ataendelea kuwa mkweli kwani mtu anapokosea asipoambiwa kuwa amekosea ni kutenda dhambi na anapoona maovu na kutokusema ni kumkosea Mungu na ndio maana amekuwa akisimama kidete bungeni na kuwaeleza.
Wachungaji hao kwa kauli moja waliunga mkono kazi zilizofanywa na Kimaro na kuahidi kuhakikisha anarudi tena jimboni kwa kusoma maazimio yao.
Akisoma azimio la wachungaji hao kutoka katika sharika za jimbo hilo, Mchungaji wa Usharika wa Karimeni Mwika, Elias Sillayo, alisema kwa kauli moja wachungaji hao wataenda kuwaeleza waumini wao kuwa mapungufu yaliyopo yanarekebishwa hivyo ni vyema wakampa nafasi nyingine ya uongozi.
Alisema kipindi cha miaka mitano amejitahidi kufanya mambo mengi na alitumia muda huo kujifunza hivyo ni vyema wakampa nafasi ya kumaliza aliyoyaanza.
Mchungaji Sillayo aliongeza kuwa jimbo hilo linahitaji viongozi bora na si bora viongozi na kuhoji kama wanaweza kuchagua viongozi wazuri wa kanisa ni kwanini washindwe kuchagua viongozi wazuri wa jamii.
“Mbunge wetu huyu tumpe nafasi nyingine ya kutuwakilisha bungeni,” alisema.
Aidha, wachungaji hao walimtaka mbunge huyo iwapo atapata ridhaa ya wananchi katika kipindi kingine atekeleze ahadi zote alizoahidi.
Alisema wachungaji hao wanafanya ibada maalum kwa ajili ya kuombea uchaguzi mkuu wa Oktoba ili uwe wa amani na utulivu ikiwa ni pamoja na wananchi kufunuliwa katika kuchagua kiongozi mwenye nia ya kuwaletea maendeleo na si kujinufaisha binafsi.
Mkutano huo ulifanyika chini ya uenyekiti wa Mkuu wa jimbo hilo, Mchungaji Luca Kessy.
Akiwakaribisha wachungaji hao, Mchungaji John Mlay alisema kila serikali ni lazima imkubali Mungu kwani hakuna serikali inayoweza kufanikiwa bila kumtambua Mungu kwani pasipo yeye hakuna serikali inayoweza kusimama.
“Tambueni kuwa mnaongoza kwa niaba ya Mungu, pasipo Mungu hatuwezi lolote na ni vyema tukawa macho uchaguzi usitufikishe katika machafuko ya kupoteza lulu ya amani na utulivu iliyopo kwa sasa,” alisema.
Mbali na wachungaji na wabunge hao, pia mkutano huo ulihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Musa Samizi, ambaye aliwataka viongozi wa dini waombee amani wakati nchi inapoelekea kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu.
Alisema Serikali inatambua mchango wa makanisa katika elimu, afya, maji kwani yamekuwa yakitoa huduma bora ndiyo maana shule zake ni bora katika kufaulisha.
Alimsifu Kimaro kwa kusema Vunjo wana bahati ya kuwa na mbunge muwazi kwani kama mtu ni mlarushwa anampa wazi kuwa ni mlarushwa; ni jasir.
Pia alikuwapo Katibu wa CCM Mkoa Kilimanjaro, Stephen Kazidi, ambaye aliwataka viongozi wa dini kutokukubali makanisa kutumika kama majukwaa ya kisiasa; wasaidie kuhubiri amani; waonye wanaoleta chokochoko; wasikubali nchi kuingia katika machafuko kama majirani zetu. Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Katibu CCM Wilaya ya Moshi, Kingazi, ambaye hakusema kitu. Mkutano huo ulifungwa saa 12 jioni.CHANZO: NIPASHE
 
Geza Ulole

Geza Ulole

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2009
Messages
16,590
Likes
8,888
Points
280
Geza Ulole

Geza Ulole

JF-Expert Member
Joined Oct 31, 2009
16,590 8,888 280
4th March 2010
Na Salome Kitomary

Mbunge wa Rombo, Basil Mramba, ametumia fursa ya kuwahutubia wachungaji 42 wa Kanisa la Kiinjili la Kulutheri Tanzania (KKKT) kwa kujitakasa kwamba yu mtu safi na mchapa kazi na kwamba ataendelea kuwa mbunge wa jimbo hilo.

Sambamba na Mramba, pia Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro ambaye aliitisha mkutano wa wachungaji hao ulioanza saa 4:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni, aliwasilisha rasmi maombi ya kutaka wamsaidie kuwasilisha ujumbe kwa waumini wao kwamba anakusudia kuwania tena ubunge katika jimbo hilo.

Katika mkutano huo ambao ni nadra kutokea katika kipindi hiki cha kupanda kwa joto la uchaguzi, Mramba na Kimaro, walitumia jukwaa hilo kujisafishia njia ya kuwania ubunge huku Mramba akitamba hakuna wa kumzuia isipokuwa kama tu Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikimkataa.

Wachungaji hao wanatoka Jimbo la Kilimanjaro Mashariki la Dayosisi ya Kaskazini ya kanisa hilo linalojumisha sharika kutoka wilaya za Rombo na Moshi Vijijini.

Katika mkutano huo uliofanyika makao makuu ya jimbo hilo, Himo, Mramba ambaye aliwasili ukumbini saa 7:00 mchana na kulakiwa na Kimaro, alisema si kila mwanaume anayevaa suruali au mwanamke anayevaa sketi anastahili kuwa mbunge na kuwataka wananchi kuwa makini na watu wanaojipitisha pitisha katika majimbo yao.

Mramba alisema ingawa anakabiliwa na kesi mahakamani ambayo imempunguzia muda wa kuwahudumia wapigakura wake, bado anakubalika katika jimbo lake na hiyo inatokana na jitihada zake za kuwatumikia wananchi kwa moyo wake wote kuhakikisha wanajikwamua dhidi ya wimbi la umaskini.

"Siasa sio kamari, kuwa kiongozi ni lazima uwe na wito fulani ndani yako na vile vile siasa ni kazi mbaya," alisema bila kufafanua.

Aidha, aliwaponda baadhi ya wabunge ambao kwa sasa wanahaha katika majimbo yao kwa kurudi kuwabembeleza wananchi dakika za mwisho ili hali muda wao wa miaka minne waliutumia kwa kukaa jijini Dar es Salaam na kuishi maisha ya starehe.

"Wabunge wengi hawaendi kwenye majimbo yao kwa ajili ya kufanya mikutano na kujua kero za wananchi, wametoa ahadi lukuki, lakini hakuna walizotekeleza na kwa sasa ndio wanahaha..haya ni mambo ya kutisha sana kwani ni wachache sana wanaopata ubunge na kutatua kero," alisema.

Mramba alisema viongozi wanaandaliwa na hawaibuki tu kwa kuwa si kila mtu anaweza kuwa kiongozi na kama Mungu amepanga mtu awe kiongozi atakuwa tu hata wanadamu wakiweka vizuizi.

Alisema baadhi ya watu wanadhani kuwa mbunge ni mtu mwenye uwezo bila kujua kuwa mbunge ni yule ambaye ana nia ya dhati na uwezo katika kuwakwamua wananchi kwenye lindi la umaskini.

Alisema aliteuliwa na Mwalimu Julius Nyerere kama mbunge wa kuteuliwa miaka ya 80 ambapo alitumia miaka mitano kujifunza na baada ya hapo alikuwa mzoefu na kwamba kila mara anakumbuka kauli ya Mwalimu Nyerere iliyomwambia 'mimi nastaafu ila wewe baki Rombo wasaidie wananchi wa Rombo'jambo ambalo amekuwa akilifanya hadi sasa.

Alisema kuwa yeye ni mzoefu katika utumishi wa umma na ubunge na amefanya kazi na marais wote wa awamu nne.

"Dunia ina watu wazuri na wabaya, tunaishi nao na tunafanya kazi nao, mimi ni mzoefu wa kushtakiwa na hilo halinikatishi tamaa ya kuwatumikia wananchi wangu ambao bado wana imani kubwa na mimi," alisema Mramba.

Mramba anakabiliwa na kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya matumizi mabaya ya madaraka wakati akiwa Waziri wa Fedha kwa kutoa msamaha wa kodi kwa kampuni tanzu ya Alex Stewart (ASSAYERS) na kuisababishia serikali hasara ya Sh. bilioni 11.7.

Akimzunguzia mbunge huyo, Mchungaji Elias Sillayo, alisema alimfahamu miaka ya 80 akiwa usharika wa Mengwe na kwamba wananchi bado wanamuhitaji na wanaomba kesi yake imalizike haraka ili aendelee kuwatumikia.

Naye Kimaro akizungumza na wachungaji hao alisema utumishi wa umma si fursa ya kunufaisha mtu binafsi, rafiki, wapambe na si fursa ya kutukuza itikadi za kisiasa.

Alisema utumishi wa umma ni dhamana na fursa adimu kwa ajili ya kulinda na kutetea maslahi ya wananchi wote.

Kimaro alisema daima ataendelea kuwa mkweli kwani mtu anapokosea asipoambiwa kuwa amekosea ni kutenda dhambi na anapoona maovu na kutokusema ni kumkosea Mungu na ndio maana amekuwa akisimama kidete bungeni na kuwaeleza.

Wachungaji hao kwa kauli moja waliunga mkono kazi zilizofanywa na Kimaro na kuahidi kuhakikisha anarudi tena jimboni kwa kusoma maazimio yao.

Akisoma azimio la wachungaji hao kutoka katika sharika za jimbo hilo, Mchungaji wa Usharika wa Karimeni Mwika, Elias Sillayo, alisema kwa kauli moja wachungaji hao wataenda kuwaeleza waumini wao kuwa mapungufu yaliyopo yanarekebishwa hivyo ni vyema wakampa nafasi nyingine ya uongozi.

Alisema kipindi cha miaka mitano amejitahidi kufanya mambo mengi na alitumia muda huo kujifunza hivyo ni vyema wakampa nafasi ya kumaliza aliyoyaanza.

Mchungaji Sillayo aliongeza kuwa jimbo hilo linahitaji viongozi bora na si bora viongozi na kuhoji kama wanaweza kuchagua viongozi wazuri wa kanisa ni kwanini washindwe kuchagua viongozi wazuri wa jamii.

"Mbunge wetu huyu tumpe nafasi nyingine ya kutuwakilisha bungeni," alisema.
Aidha, wachungaji hao walimtaka mbunge huyo iwapo atapata ridhaa ya wananchi katika kipindi kingine atekeleze ahadi zote alizoahidi.

Alisema wachungaji hao wanafanya ibada maalum kwa ajili ya kuombea uchaguzi mkuu wa Oktoba ili uwe wa amani na utulivu ikiwa ni pamoja na wananchi kufunuliwa katika kuchagua kiongozi mwenye nia ya kuwaletea maendeleo na si kujinufaisha binafsi.

Mkutano huo ulifanyika chini ya uenyekiti wa Mkuu wa jimbo hilo, Mchungaji Luca Kessy.

Akiwakaribisha wachungaji hao, Mchungaji John Mlay alisema kila serikali ni lazima imkubali Mungu kwani hakuna serikali inayoweza kufanikiwa bila kumtambua Mungu kwani pasipo yeye hakuna serikali inayoweza kusimama.

"Tambueni kuwa mnaongoza kwa niaba ya Mungu, pasipo Mungu hatuwezi lolote na ni vyema tukawa macho uchaguzi usitufikishe katika machafuko ya kupoteza lulu ya amani na utulivu iliyopo kwa sasa," alisema.

Mbali na wachungaji na wabunge hao, pia mkutano huo ulihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Musa Samizi, ambaye aliwataka viongozi wa dini waombee amani wakati nchi inapoelekea kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu.

Alisema Serikali inatambua mchango wa makanisa katika elimu, afya, maji kwani yamekuwa yakitoa huduma bora ndiyo maana shule zake ni bora katika kufaulisha.

Alimsifu Kimaro kwa kusema Vunjo wana bahati ya kuwa na mbunge muwazi kwani kama mtu ni mlarushwa anampa wazi kuwa ni mlarushwa; ni jasir.

Pia alikuwapo Katibu wa CCM Mkoa Kilimanjaro, Stephen Kazidi, ambaye aliwataka viongozi wa dini kutokukubali makanisa kutumika kama majukwaa ya kisiasa; wasaidie kuhubiri amani; waonye wanaoleta chokochoko; wasikubali nchi kuingia katika machafuko kama majirani zetu. Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Katibu CCM Wilaya ya Moshi, Kingazi, ambaye hakusema kitu. Mkutano huo ulifungwa saa 12 jioni.

Source: NIPASHE

10th March 10
Mramba aibuka kwa mapadri, masheikh

Salome Kitomary

[FONT=ArialMT, sans-serif]Mbunge wa Rombo, Basil Mramba (CCM), amekutana na viongozi wa dini za Kikristo na Kiislamu pamoja na wa serikali kuzungumzia maendeleo ya wilaya na kutumia fursa hiyo kuwaomba viongozi hao wamuunge mkono nia yake ya kutetea kiti cha jimboni hilo, katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, mwaka huu.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Katika mkutano huo uliofanyika Machi 2, mwaka huu katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Peter Toima, na kuhudhuriwa na mapadri wa Kanisa Katoliki na masheikh wa wilaya hiyo, Mramba aliwaeleza kuwa ana nia ya kuwania ubunge katika jimbo hilo mwaka huu.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Taarifa kutoka katika mkutano huo, uliochukua zaidi ya saa tano, zinadai kuwa Mramba alichelewa kufika na kukuta mkutano ukiendelea na katika mazungumzo yake, aliwaomba viongozi hao kufikisha salamu kwa waumini wao na kuhakikisha wanamuunga mkono ili aweze kufanikiwa.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Aidha, aliwaomba viongozi hao kumsaidia ili aweze kurejea tena katika nafasi hiyo na kuwaeleza wazi kuwa bado ana nia ya kuwania ubunge katika jimbo hilo na kwamba nia yake itakwama tu kama Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakitampa ridhaa.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Wakizungumzia ombi hilo, ambalo ni nadra sana kutokea, hasa katika kipindi hiki, ambacho joto la uchaguzi limepanda katika maeneo mbalimbali nchini, baadhi ya viongozi walidai wana taratibu zao za kufanya kazi na hawawezi kuburuzwa na wanasiasa.[/FONT]
"[FONT=ArialMT, sans-serif]Sisi kama viongozi wa dini tuna taratibu zetu za kufanya kazi, kama mtu ametuita na ameonyesha nia ya kuwania ubunge," alisema kiongozi mmoja wa dini na kuongeza: "Sisi tunamsikiliza na kuwaachia maamuzi wapigakura, ambao ni wananchi kwani hatuwezi kuwaambia wamchague nani na kumuacha nani."[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema kwa sasa nchi ikiwa inaelekea katika uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu, wanajitokeza watu wengi na kuongea nao, lakini wao wanawasikiliza wananchi pekee ndiyo wenye maamuzi.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Akizungumzia mkutano huo ambao ulihudhuriwa pia na Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo na viongozi wengine wa serikali, Mkuu wa wilaya hiyo alisema mkutano huo aliuitisha yeye kwa lengo la kukutana na viongozi hao wa dini kujadilia masuala ya maendeleo ya wilaya hiyo.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema kuwa hakujua Mramba alitokea wapi na kuhudhuria mkutano huo na kwamba hakumwalika, lakini kwa kuwa alifika alipewa nafasi ya kuzungumza na viongozi hao kama mbunge wao.[/FONT]
"[FONT=ArialMT, sans-serif]Sikumuita Mbunge (Mramba), yeye alihudhuria kama mtu mwingine ambaye angeruhusiwa kuhudhuria, kama ungekuwa mkutano wa viongozi wa siasa lazima ningemuita Mwenyekiti wa CCM mkoa na Katibu," alisema DC Toima na kuongeza: "Mkutano wangu ulikuwa wa kawaida na si wa kisiasa."[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Toima alisema mkutano huo ulijadili ushirikishwaji wa viongozi wa dini katika masuala ya maendeleo ya afya, maji, miundombinu na masuala mengine ya maendeleo ya wilaya hiyo.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alipohojiwa juu ya hatua ya kuitisha mkutano huo wakati kukiwa na joto la uchaguzi, alisema yeye si kiongozi wa siasa bali ni mtumishi wa serikali na kwamba hachanganyi siasa na dini na endapo kiongozi mwingine wa siasa angefika katika mkutano huo angeruhusiwa kuhudhuria.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Siku hiyo hiyo, majira ya saa 7 mchana, Mramba alizungumza na wachungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini katika mkutano ulioitishwa na Mbunge wa Jimbo la Vunjo, Aloyce Kimaro (CCM).[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mkutano huo ulifanyika makao makuu ya jimbo la Kilimanjaro Mashariki, katika mji mdogo wa Himo chini ya uenyekiti wa Mkuu wa Jimbo hilo, Luca Kessy.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Katika mkutano huo, Mramba alisema licha ya kukabiliwa na kesi mahakamani, bado ataendelea kuwa mbunge wa jimbo hilo kwani wananchi wake bado wanampenda na watampa nafasi tena ya kuwawakilisha bungeni.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema ni mzoefu wa kesi na kwamba ana uzoefu katika utendaji kazi serikalini na ubunge kwani amekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa vipindi vitatu tofauti.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Aligusia kesi ya jinai inayomkabili mahakamani kuwa inamnyima nafasi ya kuwahudumia vyema wananchi wake.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mramba alisema si kila mwanaume anayevaa suruali au mwanamke anayevaa sketi anastahili kuwa mbunge, hivyo ni vyema wananchi wakawa makini sana na watu wanaojipitisha pitisha katika majimbo yao.[/FONT]
"[FONT=ArialMT, sans-serif]Siasa siyo kamari, kuwa kiongozi ni lazima uwe na wito fulani ndani yako na vile vile siasa ni kazi mbaya," alisema bila kufafanua.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Aidha, aliwabeza baadhi ya wabunge, ambao kwa sasa wanahaha katika majimbo yao kwa kurudi kuwabembeleza wananchi dakika za mwisho ilhali muda wao wa miaka minne waliutumia kwa kukaa jijini Dar es Salaam na kuishi maisha ya starehe.[/FONT]
"[FONT=ArialMT, sans-serif]Dunia ina watu wazuri na wabaya, tunaishi nao na tunafanyakazi nao, mimi ni mzoefu wa kushtakiwa na hilo halinikatishi tamaa ya kuwatumikia wananchi wangu ambao bado wana imani kubwa na mimi," alisema.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Hivi karibuni, Katibu wa CCM mkoani hapa, Steven Kazidi, alikaririwa akiwataka viongozi wa dini kutokubali makanisa kutumika kama majukwaa ya kisiasa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi huo.[/FONT]

NIPASHE
http://www.ippmedia.com/frontend/functions/print_article.php?l=14308
 
Geza Ulole

Geza Ulole

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2009
Messages
16,590
Likes
8,888
Points
280
Geza Ulole

Geza Ulole

JF-Expert Member
Joined Oct 31, 2009
16,590 8,888 280
Mimi chichemi nikiongea humu ndani kuna Warombo watanishambulia nina chuki! lakini kwa upeo wangu mdogo Mungu alionijalia that was a church used and a KKT church in Northern diocese! God have mercy on us! and second Nyerere legacy misused! though he might be attesting what Nyerere told him, his acts didn't honour the legacy of Nyerere after his death! "His time to eat arrived after his teacher was gone"! sasa sijui kuna lipi la ziada hapa naanza kusema character na personality ya mhusika inaongea vyoote! sihitaji kusema chochote!
 
N-handsome

N-handsome

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2008
Messages
2,337
Likes
141
Points
160
N-handsome

N-handsome

JF-Expert Member
Joined Jan 23, 2008
2,337 141 160
Watubu tu, Mungu
 
Regia Mtema

Regia Mtema

R I P
Joined
Nov 21, 2009
Messages
2,974
Likes
31
Points
0
Regia Mtema

Regia Mtema

R I P
Joined Nov 21, 2009
2,974 31 0
Viongozi wa dini nao nowdays,mmh..Wanahubiri wasiyoyaishi.
 
Ben Saanane

Ben Saanane

Verified Member
Joined
Jan 18, 2007
Messages
14,602
Likes
3,893
Points
280
Ben Saanane

Ben Saanane

Verified Member
Joined Jan 18, 2007
14,602 3,893 280
-Kwa kweli itafika siku hapa Tanzania watu wataacha kuabudu makanisani

-Sikubaliani na maneno ya Mramba kutumia vibaya jina la mwalimu Nyerere.Haya ni matusi mazito.Nyerere alijenga usawa,sasa mramba ndugu yangu,aliambiwa awasaidie wananchi wa Rombo kwa njia aliyotumia?

Hwa wachungaji nao,mhh! nimekumbuka maandiko ya biblia kuhusu manabii wa uongo walivyoawaangusha wafalme!
 
Geza Ulole

Geza Ulole

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2009
Messages
16,590
Likes
8,888
Points
280
Geza Ulole

Geza Ulole

JF-Expert Member
Joined Oct 31, 2009
16,590 8,888 280
-Kwa kweli itafika siku hapa Tanzania watu wataacha kuabudu makanisani

-Sikubaliani na maneno ya Mramba kutumia vibaya jina la mwalimu Nyerere.Haya ni matusi mazito.Nyerere alijenga usawa,sasa mramba ndugu yangu,aliambiwa awasaidie wananchi wa Rombo kwa njia aliyotumia?

Hwa wachungaji nao,mhh! nimekumbuka maandiko ya biblia kuhusu manabii wa uongo walivyoawaangusha wafalme!
halafu hajaeleza kama Nyerere alisema atawale Rombo milelea au la! aibe wizara ya fedha au la? hapa huyu mtu anatumia jina la Nyerere kwa manufaa binafsi to gain popularity! sasa sijui watu wa Mwl Nyerere foundation wako wapi? Butiku yuko wapi?
 
K

Kilembwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2009
Messages
1,135
Likes
53
Points
145
K

Kilembwe

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2009
1,135 53 145
Eeeh! Mola tuepushe na hawa wanasiasa walionza kufilisika, yaani sasa wameishiwa na kuanza kukimbilia kwenye nyumba za ibada, nanyi wachungaji hebu muogopeni muumba wenu, kumbukeni mafundisho ya bwana yesu alipojaribiwa na shetani baada ya funga yake ya siku 40"... shetani akamuambia yesu, nisujudu nami nitakupa kipande cha mkate, yesu akamuambia imeandika mwanadamu hataishi kwa kipande cha mkate, bali kwa kla neno litokalo mbinguni, shetani akampandisha hata juu ya kilele cha mlima na kumwambia tazama nchi yote hii, ukinisujudia nitakupa uitawale, yesu akamwambia Kwenda zako shetani mkubwa we, maana imeandika usimsujudie mwingine ila mimi muumba wako.." Enyi wachungaji mbona mnashawishika kwa kipande cha mkate na mnatamni kutawala na shetani? wafukuzeni Mramba na Kimaro waambieni " imeandika kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe!
 
Mshiiri

Mshiiri

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2008
Messages
1,900
Likes
83
Points
145
Mshiiri

Mshiiri

JF-Expert Member
Joined Jun 16, 2008
1,900 83 145
Rombo ni yetu si ya Mramba na hatumtaki akale majani
 
Ben Saanane

Ben Saanane

Verified Member
Joined
Jan 18, 2007
Messages
14,602
Likes
3,893
Points
280
Ben Saanane

Ben Saanane

Verified Member
Joined Jan 18, 2007
14,602 3,893 280
halafu hajaeleza kama Nyerere alisema atawale Rombo milelea au la! aibe wizara ya fedha au la? hapa huyu mtu anatumia jina la Nyerere kwa manufaa binafsi to gain popularity! sasa sijui watu wa Mwl Nyerere foundation wako wapi? Butiku yuko wapi?

Only in tanzania,mtu anatuhumiwa kuiba mabilioni ya fedha halafu anaenda kutoa matamko makanisani.

Kwanza alikua mtetezi mkubwa wa ununuzi wa ndege na Radar ya wizi,kiongozi wa aina hii anathubutu vipi ku-associate his political legacy with JK nyerere's?

Watu wa mwalimu nyerere foundation wafikie mahala watoe tamko au kuchukua hatua pale ambapo watu wanalikashfu jina la Mwalimu
 
vivian

vivian

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2009
Messages
1,730
Likes
52
Points
145
vivian

vivian

JF-Expert Member
Joined Nov 2, 2009
1,730 52 145
Rombo ni yetu si ya Mramba na hatumtaki akale majani
Utapiga kura? kama ni ndio, Je utakua wapi kipindi cha uchaguzi? Rombo au...
our Ignorance will leave Mramba as our MP for the next 5yrs. believe you me. Mramba atakua tena mbunge wa Rombo.
 
bona

bona

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2009
Messages
3,794
Likes
180
Points
160
bona

bona

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2009
3,794 180 160
hili kanisa linatumiwa vibaya sana, mtanzania ambaye si mchaga kua m kkt ni kama unajipendekeza, ilo ni kanisa la ma mangi na pesa ndio mungu wao, viongozi wengi wa kanisa ili wanatukuza sana ela pasipo kujali uadilifu, nasikia mengi pale st alban ana kiti chake, muumini mwingine hawezi kaa, tujiulize mengi ni nani zaidi ya kua tu mfanyabiashara, angekua rais tungekubali labda sababu za kiusalama!
 
Ben Saanane

Ben Saanane

Verified Member
Joined
Jan 18, 2007
Messages
14,602
Likes
3,893
Points
280
Ben Saanane

Ben Saanane

Verified Member
Joined Jan 18, 2007
14,602 3,893 280
Utapiga kura? kama ni ndio, Je utakua wapi kipindi cha uchaguzi? Rombo au...
our Ignorance will leave Mramba as our MP for the next 5yrs. believe you me. Mramba atakua tena mbunge wa Rombo.

Yeah,its true.The guy is taking advantage of ignorance ya wale walioko kule.it's a pity kuwa most people especially youth hawana utamaduni wa kupiga kura.Hao ndio wanaomu-endorse Mramba.

But the time has come,he should face a serious challenge within the party to start with.
 
Ben Saanane

Ben Saanane

Verified Member
Joined
Jan 18, 2007
Messages
14,602
Likes
3,893
Points
280
Ben Saanane

Ben Saanane

Verified Member
Joined Jan 18, 2007
14,602 3,893 280
Nadhani hii habari ipo
 
Ben Saanane

Ben Saanane

Verified Member
Joined
Jan 18, 2007
Messages
14,602
Likes
3,893
Points
280
Ben Saanane

Ben Saanane

Verified Member
Joined Jan 18, 2007
14,602 3,893 280
Mramba%20B%281%29.jpg

Mh.Basil Pesambili mramba,Mp Rombo constituency
 
PJ

PJ

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2007
Messages
297
Likes
2
Points
35
PJ

PJ

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2007
297 2 35
Kila jambo lina wakati wake. NaMramba alikuwa na wakati wake ambao sasa umeisha na tunamwomba kwa ustaarabu asijaribu kujiabisha. Alinde heshima yake aondoke kwa amani. Alizokusanya zinamtosha na tuna watu wengi wengi wenye uweza na uelewa na sympathy na wananchi wa Rombo.

Tumamtakia maisha mema baada ya kustaafu
 
babu M

babu M

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2010
Messages
4,140
Likes
1,145
Points
280
babu M

babu M

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2010
4,140 1,145 280
-kwa kweli itafika siku hapa tanzania watu wataacha kuabudu makanisani

-sikubaliani na maneno ya mramba kutumia vibaya jina la mwalimu nyerere.haya ni matusi mazito.nyerere alijenga usawa,sasa mramba ndugu yangu,aliambiwa awasaidie wananchi wa rombo kwa njia aliyotumia?

hwa wachungaji nao,mhh! Nimekumbuka maandiko ya biblia kuhusu manabii wa uongo walivyoawaangusha wafalme!
mkuu ben, naomba unifafanulie hapo kwenye red...njia gani hiyo aliyotumia kuwasaidia warombo?
 
Kiby

Kiby

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2009
Messages
5,556
Likes
1,353
Points
280
Kiby

Kiby

JF-Expert Member
Joined Nov 16, 2009
5,556 1,353 280
Kimaro anaweweseka kwa kivuli cha Lyatonga hata kuamua kutumia mimbara za makanisa kwa propaganda za kisiasa. Binafsi mimi naamini damokrasia ya atakaeletwa na wengi na kuiheshimu tofauti na hawa wachungaji ambao washamweka mtu wao mfukoni tayari halafu wanawaasa waumini wamwombe Mungu awafunulie kiongozi ni yupi. Haka ni kamchezo ka kum-remote Mungu kinataka kuchezwa hapa. Kwa upande wa mramba wachungaji wanapaswa wajionee aibu wenyewe juu ya nyuso zao. Maana hata wao wanastaafu kazi ya utumishi wa Mungu sembuse huyu Mwanasisa anaetaka kudumisha utawala wa kifalme katika jimbo. Anataka afe akiwa madarakani kama Mugabe?. Hivi anaamini nini kama sii kwamba sekondari zote na vyuo hazijawahi kutoa mwenye akili ila yeye? Ndio maana kwenye mkutano mmoja wa kampeni jimboni aliwahi kuwatukana warombo kwamba hakuna mama anaeweza kuzaa waziri. Maana yake ni nini ila kwamba Rombo yote mama yake ndie pekee aliyepewa uwezo wa kuzaa waziri. Yuu angali akidumu katika fikara zake. Kkkt kaskazini nawashauri mbadilishe jina ili liendane na itikadi yenu ya kisiasa, badala yake muitwe ΚKKTccm kaskazini.
 
J

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Messages
14,355
Likes
8,711
Points
280
J

JokaKuu

Platinum Member
Joined Jul 31, 2006
14,355 8,711 280
..huyu Kimaro si alikuwa kwenye kundi la "wapiganaji"? halafu leo yuko pamoja na Basil Pesambili Mramba? CCM kweli ni wasanii.
 
Augustine Moshi

Augustine Moshi

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2006
Messages
2,281
Likes
367
Points
180
Augustine Moshi

Augustine Moshi

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2006
2,281 367 180
This is much ado about nothing. If Mramba wanted to use Churches to campaign, he wouldn’t have used the KKT. It has zero influence in Rombo. There are simply no Lutherans there.

The people of Rombo care passionately about one thing, and only about one thing, and that is their road. Mramba knows that very well. He has fought hard and long to have that road tarmacked.

A couple of years back, Mramba asked the people of Rombo to start “practising on how to cross a tarmac road". They have dutifully done that, but I was there this last Christmas and all I saw was mud. I hadn’t practised crossing that, so I got stuck in it.

Mramba will win re-election if and only if there is tarmac on the Rombo Road by election time. It won’t depend on court cases in Dar.
 
Forum statistics

Threads 1,236,244
Members 475,030
Posts 29,251,507