Mramba azidi kumkaba koo Mkapa; Adai ndiye aliyetoa maagizo

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
ALHAMISI, NOVEMBA 29, 2012 05:06 NA KULWA MZEE, DAR ES SALAAM


*Adai ndiye aliyetoa maagizo
*Asema hakukurupuka kutoa mkataba

ALIYEKUWA Waziri wa Fedha, Basil Mramba ameiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mji Dar es Salaam, kuwa hakukurupuka kuipatia Kampuni ya Alex Stewart mkataba, bali ni uamuzi wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa.

Mramba alidai hayo jana alipokuwa akihojiwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Fredrick Manyanda kutokana na ushahidi wake aliotoa mahakamani kuhusu tuhuma za kutoa msamaha wa kodi kwa kampuni hiyo na kuisababishia Serikali hasara ya Sh bilioni 11.7.

"Zoezi la kumpata mkaguzi wa dhahabu, Alex Stewart halikuhitaji pupa wala kufanywa kwa pupa, Rais Mkapa aliagiza utekelezaji ufanyike haraka na kuzitaka Benki Kuu Tanzania (BoT) na Wizara ya Fedha zitafute njia za kupata fedha za kuilipa kampuni hiyo ili ianze kazi.

"Kuna mambo ya msingi tulikubaliana, miongoni mwa hayo ni umuhimu wa kukagua madini, BoT isimamie kupata mkaguzi anayefaa kwa utaratibu wa zabuni, gharama zilipwe na Serikali na si kampuni za madini kwa sababu tungetaka walipie, lazima tungebadili mikataba iliyokuwepo," alidai Mramba.

Alidai hawakufanya pupa, kwani aliweza kumshauri aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona kuangalia na nchi nyingine wanafanyaje na kumweleza kwamba, akikubaliana na ushauri huo waendelee.

"Sikumwagiza Yona, bali nilimshauri hakuna waziri mwenye kumwagiza waziri mwenzake, kwa sababu wote wana hadhi sawa," alidai Mramba na kumsisitizia Manyanda kuwa katika barua yake ya Aprili 28,2002 kaeleza zaidi ya mara mbili kwamba anamshauri.

Mramba, alikubaliana na wakili Manyanda kwamba waziri ndiye msimamizi wa sera katika wizara anayohusika nayo na kwamba, watendaji wanasimamiwa katika utekelezaji na katibu mkuu wa wizara.

Kesi hiyo, inasikilizwa na jopo la mahakimu, John Mtemwa, Saul Kinemela na Sam Rumanyika.

Mramba, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona na aliyekuwa Katibu Mkuu, Wizaya ya Fedha, Grey Mgonja wanadaiwa kutumia madaraka vibaya kwa kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya Alex Stewart, nakuisababishia Serikali hasara ya Sh bilioni 11.7.

 
Ni VIZURI SANA... Sasa MMOJA NDANI ya KUNDI la CULT YA MAFISADI anaanza kuongea; KWAHIYO HAPO NDIO SAHIHI UCHACHU unatoka... NA WEZI Tutawajua karibuni... CCM OHYEE!!!
 
Ni VIZURI SANA... Sasa MMOJA NDANI ya KUNDI la CULT YA MAFISADI anaanza kuongea; KWAHIYO HAPO NDIO SAHIHI UCHACHU unatoka... NA WEZI Tutawajua karibuni... CCM OHYEE!!!

Wewe uliyeko CCM ndio huwajui,sisi tunawajua.
 
naona wanatumia loop holes za katiba yetu kujinasua!
Sasa ni dhahiri kuwa ben ndiye fisadi kuu na yampasa kufikishwa mahakamani.
 
Huyu naye ataachiwa huru kama ilivyokuwa kesi ya Mahalu.
Mkuu huyu naona atagota tu.
Maana kama uamuzi wa Mkapa haukuwa sahihi yeye alifanya nini?
Mahakama haitafunwa goli lile lile na mtu yule yule kwa staili ile ile.
 
Mbona sisi tunawajua. Kumbe kuna watu hawawajui MAFISADI ni wakina nani?



Ni VIZURI SANA... Sasa MMOJA NDANI ya KUNDI la CULT YA MAFISADI anaanza kuongea; KWAHIYO HAPO NDIO SAHIHI UCHACHU unatoka... NA WEZI Tutawajua karibuni... CCM OHYEE!!!
 
Nijuavyo mimi Rais kwenye mambo yanayohusu fedha ndefu huusika sana ktk maamuzi,maana pamoja na majukum mengine tuliyompa kama serikali lakini masuala yanayohusu fedha ndiyo hasa.So matumizi ya mabilioni lazima mkuu wa nchi ahusike na hata mahakama inalijua hilo. Mkapa hawezi kulikwepa hilo labda nae amkwepe kwa kusema alishauriwa vibaya na mramba.Vinginevyo kesi hii inawahusu wote tangu mwanzo wala si mramba pekee yake!
 
mi naona waachiwe huru tu kwa sababu hawa walifuata maagizo...mbona lowasa hayuko mahakamani, mbona ngeleja na wenzake hawako mahakamani ambao wamekula hela zaidi ya kina yona? kama hamuwezi kuwashtaki wote basi waachiwe wote
 
Hivi mnaamini hiki kiinimacho? Eti Mramba amkaba koo Mkapa! Ha ha ha ha! Huu ni mpango mahsusi uliopangwa kwa kutumia udhaifu wa Katiba iliyopo. Mkapa anajua vizuri sana kinachoendelea, Mramba anajua sana kinachoendelea, na CCM wanajua vizuri mno mpango mzima.

Iko hivi: Kwa kuwa CCM wanahusika na madudu yote haya na kwa kuwa wamemwekea "kinga ya kutoshtakiwa" mmoja wao (kwa sababu maalum kujinasua na ufisadi) na kwa kuwa wote ni wale wale, then peleka tuhuma zote kwa mwenye kinga na issue nzima itakuwa imekwisha. KINGA YA KUTOSHTAKIWA ni upuuzi zaidi ya upuuzi.
 
Mbona sisi tunawajua. Kumbe kuna watu hawawajui MAFISADI ni wakina nani?

Yaani Unaijua LIST ya WALIOFICHA PESA USWIS? Sabau kunahitajika SABABU za kuweza kuelewa ni KIASI gani na JINA LAKE... Sio habari za MITAANI...

Kama hivyo then TUELEZE sisi WENGINE hatujui...
 
Mungu ni mwema

atawaweka hai hao wahujum uchumi had 2015 kisha tutawahukumu kwa sheria za nchi hii mmoja baada ya mwingne

hata wakimbilie uhamishoni,,tutawakamata tuh
 
Kwenye hizi kesi Mkapa anatakiwa aunganishwe kama mshitakiwa si kutoa ushahidi wa kuwaokoa wezi wenzake kama alivyofanya kwa Mahalu.
 
Back
Top Bottom