Nilichojifunza kutokana na maandamano ya vijana wa ccm kwenye ubalozi wa Sauz ni
1. Mradi wa "Ndege za Magufuli" ndio kielelezo nambari moja kinachotumiwa na wana ccm na serikali ya awamu ya tano katika kuonesha mafanikio ya uthubutu na uchapaji kazi wa Jiwe (hapa kazi tu).
2. Ndege hizi ndio "jeuri" ya Jiwe dhidi ya watangulizi wake na hutumika "kuwachambia" wakosoaji kwa kuwaonesha kuwa "nchi hii ni tajiri" na tuna uwezo wa kununua "equipment" hizi kwa fedha taslim.
3. Mradi huu umegeuka kama mpira katika mchezo wa kabumbu unaogombewa na timu mbili pinzani kwa maana ya serikali/ccm dhidi ya wakosoaji na kila upande unataka kuibuka mshindi.
4. Hivyo basi, serikali ya Jiwe iko tayari kutumia gharama yoyote kuhakikisha mradi huu unasonga mbele hata husipoleta faida ili tu kuthibitisha kwamba wanaokosoa mradi huu hawako sawa sawa.
5. Sasa basi, zinapotokea changamoto katika mradi huu kama vile kuharibika kwa ndege, kushindwa kuruka masafa ya kimataifa, uchache wa abiria au kushikiliwa na wadeni wetu kama ilivyotokea kule Canada na hii ya Sauz, inachukuliwa kama ni kufeli kwa serikali ya Jiwe na ushindi kwa wakosoaji.
6. Kwa kuwa mradi huu ni "critical move" kwa serikali ya awamu ya tano, changamoto zinapotokea serikali huwa "inapata tabu sana" dhidi ya wakosoaji, bali hutafutwa "mchawi" kuwa ndiye anayekwamisha. Kule Canada Tundu Lisu ndiye aliyechochea kukamatwa kwa ndege na hii ya Sauz tunaambiwa Mtanzania aliyefukuzwa kazi UD ndiye aliyeongoza jopo la mawakili wa ukoo wa Steyn katika madai yao dhidi ya serikali.
7. Kinyume chake, mafanikio yoyote yanayopatikana katika mradi huu yanakuwa ni ya Jiwe na huwa "highly promoted" dhidi ya wakosoaji.
Binafsi natambua mtazamo wa Rais Magufuli na nia njema aliyonayo juu ya kuifanya Tanzania yetu "Great Nation".
Rais Magufuli anaumia sana kuona nchi yetu pamoja na utajiri tulionao bado tunapitwa na nchi duni kama Ruanda, Ethiopia na Kenya ambazo zina mashirika makubwa ya ndege na hupeperusha bendera zake (ndege) kimataifa. Kwanini isiwe na Tanzania nayo? Ukweli ni kwamba sisi watanzania tulikuwa tukikosoa serikali zilizopita kuwa zilikosa maarifa ya kulinyanyua shirika letu la ndege. Tulikuwa tunasema tunashirika la ndege lisilo na ndege bali ni wafanyakazi tu. Swali la msingi hapa ni je Magufuli kama Rais wa awamu ya Sasa, hakupaswa kufanya chochote katika kuliendeleza shirika letu? Je, Kwanini kuna watu wanakosoa mradi wa ATCL? Je, wazalendo ni wale wanaosapoti au wanaokosoa? Je, kuna haja au tuachane na mradi huu?
Katika kujibu maswali haya napenda kuishauri serikali ya awamu ya tano kuwa kuna sehemu inakosea katika kutekeleza miradi ya maendeleo. Kwanza kabisa ieleweke hakuna Rais aliyeongoza nchi hii ambaye si mzalendo. Hakuna Rais ambaye hakuwa na nia njema au alipenda kuona ATCL inakufa. Wote walijitahidi kuiruzuku ATCL lakini changamoto za ATCL ni kubwa mno kiasi kwamba inatakiwa tuchague kuendeleza shirika au tupate hasara. Rais Kikwete alikuwa anasikitika sana kuhusu mwenendo wa shirika hili kuipa hasara serikali kwa kushindwa kujiendeleza licha ya jitihada za serikali kulisaidia shirika.
Ninaposema kuna sehemu sarikali ya awamu hii inakosea licha ya nia njema iliyonayo maana yangu ni moja tu, serikali hii inapenda sifa. Hulka ya sifa hupelekea serikali kushindwa kuona na kupima ugumu wa kutatua changamoto za kuiendeleza ATCL kwa maana ya madeni.
Gharama ya kuwa na ATCL ya "kimataifa" ni kubwa kuliko faida yake kiuchumi. Labda ndioma hesabu zake zinahifadhiwa ikulu na hazikaguliwi na CAG. Bali ni kujenga sifa tu kwamba Tanzania tuna shirika la ndege kama nchi zingine za jirani.
Lakini tunapoamua kutumia fedha taslim nyingi kununua midege hii wakati serikali na shirika lenyewe lina madeni na vikwazo kibao katika anga za kimataifa sijui tuite nini hii?
Kwa kumalizia, changamoto hizi za ndege za ATCL ni matokeo ya kukurupuka kuliendeleza shirika bila kutathmini changamoto zake ambazo viongozi wa awamu za nyuma waliziona. Lakini makada wa CCM wanapoandamana kwenye ubalozi wa Sauz kwa kisingizio cha kuonesha uzalendo kwa mali za nchi ni upuuzi. Wala wasijaribu kutuonesha kuwa Srikali ya Afrika Kusini ndiyo walioishikilia ndege. Na ikiwa serikali ya Sauz imeshindwa kumsaidia Jiwe kwa kuingilia maamuzi ya mahakama ya nchi hiyo, vijana wa ccm watambue kuwa mfumo wetu wa kiutawala na mambo ya sheria hauko sawa na ule wa Sauz. Serikali haipaswi kuingilia maamuzi ya mahakama kama ilivyo hapa Tanzania. Kenya walisaidia kurudisha dhahabu iliyoibiwa Tanzania. Je, wanataka kutuambia akina Steyn wapeiba ndege yetu serikali ya Sauz ifanye kama ile ya kenya kuturudishia ndege?