Mradi wa umeme wa maporomoko ya Rusumo gharama kubwa mara 4 ya mradi wa umeme Stiegler’s Gorge pigo kwa walala hoi wa (Tanzania, Rwanda na Burundi)

MZK

JF-Expert Member
Sep 13, 2012
223
303
1574796604830.png





Mradi wa Umeme wa maporomoko ya Mto Rusumo uliopo mpakani wa Tanzania na Rwanda, unazishirikisha Nchi tatu za Tanzania, Rwanda na Burundi unaendeshwa kwa mkopo Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo Afrika kupitia taasisi au mtu kati anayeitwa NELSAP, mradi huu unatarajiwa utakapokamilika utazalisha umeme wa kiasi cha 80MW, ambazo zitagawanywa kwa Nchi tatu Mradi huu mpaka utakapokamilika unatarajiwa kutumia kiasi cha Zaidi dola za Kimarekani milloni 500, ambazo ni Zaidi ya trilioni moja ya Tanzania

Mradi huu ni mojawapo ya miradi ya gharama sana Duniani ,ni mara 4 hivi ya gharama za mradi wa Umeme wa Stieglers Gorge (mradi wa Rufiji Stieglers gorge ni kama 3.9trilioni lakini 2100MW, ) Gharama hizi za mradi wa wa Umeme wa Maporomoko ya Rusumo zilitakiwa zijenge miradi kama 4 mingine ya 80MW ukilinganisha na mradi wa Umeme wa Stieglers Gorge. Ugharama huu wa mradi wa Umeme wa Maporomoko ya Rusumo ni kutokana na muundo wa wa usimamizi wa mradi huu.

Mradi huu una wasimamizi takribani Wanne, World Bank, African Development Bank, Nelsap, Rusumo Power Company limited, na Mshauri Mwelekezi, wote hawa wanatafuna pesa itakayolipwa na mlala hoi kutoka Tanzania, Burundi na Rwanda. Pesa za mradi huu zimetafutwa na taasisi au mtu kati anayeitwa NELSAP, akakopa kwa niaba ya Serikali hizi tatu na kampuni tarajiwa itakayoendesha mradi huu(Rusumo Power Company Limited) ambayo ipo hewani hewani kama Nchi ya Kusadikika mpaka sasa hivi.

Wasimamizi hawa wa Mradi na waliokopa hizi pesa NELSAP wamejitengea takribani dola za Kimarekani miliono 37 sawa na takribani Zaidi ya Tsh bilioni 70. Wanaishi katika Mbingu ya Saba kwa kulipana mipesa minono kupitia semina, warsha, makongamano na tour mbali mbali yote haya yakifanyika Ughabuni ili mipesa ya mkopo itakayolipwa na walalahoi iendelee kuteketea kama Msitu wa AMAZON. Wananchi wanaoishi eneo la Mradi ( Kijiji cha Rusumo Tanzania na Rusumo Rwanda) wanaendelea kuishi katika maisha duni wakikosa hata huduma za msingi za Kiafya, maji, barabara n.k

Wakati mradi huu ukianza ulitengewa kiasi cha Zaidi ya dola za Kimarekani milioni (sawa takribani billioni 70 za Kitanzania) kwa ajiri shughuri za maendeleo ya Jamii kwa vijiji vinavyozunguka mradi huu (LOCAL DEVELOPMENT AND BENEFIT SHARING) Fungu hili lilikuwa hasa kwa ajiri ya kazi kuu mbili, Resetlement Action Plan (RAP) na Local Area Development Plan (LADP). Wasimamizi wa Mradi NELSAP waliahidi miradi kadhaa watakayoifanya kwa vijiji vilivyopo eneo la mradi kama, Ujenzi wa Shule, Kituo cha Afya, Kuleta Maji na Kusaidia Wananchi wa Chini kupitia miradi ya Ujasiramali. Hadi naandika Makala hii hizi pesa za mafungu hayo imebaki ni kitendawili huku kina mama na watoto wa eneo hili wakitaabika kwa huduma za maji na afya.Ziko wapi hizi bilioni 70?

Wananchi wa Eneo hili kabla ya kuanza mradi waliopo ndani ya eneo la mradi waliahidiwa watalipwa na kuhamishwa kwa nyumba zilizopo karibu na eneo laulipuaji wa miamba kupitia fungu la Resettlement Action Plan (RAP) na NELSAP ili kupisha ulipuaji wa miamba , tofauti yake walifanyiwa tathimini na wengine hawakulipwa pesa yoyote. Nyumba nyingi za wakazi maskini wa eneo hili hasa upande wa Tanzania zimepasuka na kuharibiwa vibaya na ulipuaji wa miamba hali inayotishia usalama wa wakazi wa hizi nyumba

Wasimamizi hawa wa mradi huu NELSAP wanasuasua hata kuhamia kwene nyumba za kisasa zilizopo eneo la mradi ili kuweza kufuatilia kwa Makini kinachoendelea katika mradi , nyumba nzuri wamejengewa ili waishi kupunguza gharama lakini wamezipuuzia na wameamua kuishi katika Mahoteli makubwa upande wa Rwanda, huku wakendesha magari ya kifali kila siku Zaidi ya Kilometer 60 kwa kila siku kuja eneo la mradi.

Kwa ushauri wangu hawa wasimamizi World Bank, African Bank na NELSAP ambao maamuzi yao yamekuwa ni ya kuchelewesha mradi huu usiishe kwa wakati maana mpaka hivi sasa hata nusu ya uj(mradi ulitegemewa kukamilika mwaka 2019) ili pesa za mradi huu ziendelee kuteketea kupitia semina, warsha, makongamano na tour mbali mbali wajiondoe kwenye usimamizi wa mradi huu wamwachie TANESCO wa mradi huu kutoka Nchi Tatu za Tanzania, Burundi na Rwanda (RUSUMO POWER COMPANY LIMITED) ili asimamie usimamizi kwa kushirikiana na Mshauri mwelekezi ambao wanatosha kabisa. Muda wote toka mradi huu umeanza 2016 mpaka leo pesa tuliyopoteza walala hoi wa hizi Nchi Tatu imetosha kwa kuhudumia hawa watu wa kati wa mradi huu. Kinachofanyika kwa hawa ni kuona huu mradi ni wa Nchi Tatu hivyo hakuna atakayekuwa anafuatilia na mwenye uchungu nao

Mawaziri wa husika wa hizi Nchi Tatu za Tanzania, Burundi na Rwanda wafanye mchakato haraka wa kuipa meno kampuni ya Kizalendo ya Rusumo Power Company Limited ili iwe na maamuzi ya mradi huu hawa NELSAP , World Bank na African Development Bank wasubiri ripoti ya utekelezaji tu, maana huu mkopo hawatatusaidia kulipa bali tutalipa sisi Walalahoi wa Tanzania, Rwanda na Burundi.

Hongera ziende kwa Rais wa Awamu ya Tano wa Tanzania Dk JOHN POMBE MAGUFULI(PhD) kwa kuamua kujenga miradi mikubwa kwa kutumia Pesa zetu za ndani na kukataa mikopo ya hawa Wafadhili wenye masharti magumu yanayoongeza Gharama mara dufu ya miradi kama huu wa Umeme Maporomoko ya Rusumo.
 
Bila shaka kuna ufisadi 1.2 trion investment kuzalisha 80MW? are we serious au ni utoto umeme hautoshi hata kulisha dar pekee.
 
Hongera ziende kwa Rais wa Awamu ya Tano wa Tanzania Dk JOHN POMBE MAGUFULI(PhD) kwa kuamua kujenga miradi mikubwa kwa kutumia Pesa zetu za ndani na kukataa mikopo ya hawa Wafadhili wenye masharti magumu yanayoongeza Gharama mara dufu ya miradi kama huu wa Umeme Maporomoko ya Rusumo...

Pesa za ndani
 
What is renewable energy?
Ni lini Tanzania tutafaidika na jua na upepo tulivyopewa bure na mwenyezi MUNGU
 
What is renewable energy?
Ni lini Tanzania tutafaidika na jua na upepo tulivyopewa bure na mwenyezi MUNGU
Achana na hizo porojo za renewable energy, dunia ya kwanza wenyewe wanazalisha sehemu kubwa ya umeme wao kwa makaa ya mawe na gesi alfu wanakuja kuwakongopea nyie huko juu ya upepo na upuuzi mwingine.
 
serikali ya Rais Magufuli imefunikwa na wingu zito za afisadi wa kimyakimya!
 
What is renewable energy?
Ni lini Tanzania tutafaidika na jua na upepo tulivyopewa bure na mwenyezi MUNGU

This is also one of renewable energy sources. It's cheap and environmentally friendly energy source.
Ni moja wapo ya nishati jadidifu.
 
Rusumo Fall Hydroelectric Project will produce 80 MW and cost is 340 MUSD (construction) + 121 MUSD (Power lines). Building time: March. 2017 - Feb 2020.
In July 2019 the project was reported to be delayed because money was lacking to buy necessary additional explosives. Governments refused funding and insisted the contractor stick to time schedule. .

Stiegler's Gorge will produce maximum 2100MW, cost 3,600 MUSD and be completed by June 14, 2022.

Anyone who has looked at comparable projects knows that nothing close to that cost and time frame has been achieved. And definitively not in Africa.. My prediction is that Tanzania will need extensive external funding to commission the dam for production within 6-10 years.

At a constructor site I read the dam is estimated to produce 5,920,000 MWh per year.
Which breaks down to 5,920,000 / (365x24) = 676MW per hour. 2100MW is max capacity.
 
Bila shaka kuna ufisadi 1.2 trion investment kuzalisha 80MW? are we serious au ni utoto umeme hautoshi hata kulisha dar pekee.

Haiingii akilini kutumia 1.2T kuzalisha 80MW ni bora tungewapa tenda wale jamaa waliopewa milioni 10 na magufuli kwa kuzalisha umeme kwao huko vijijini ndio wazalishe hizo MW 80 na wangechukua fedha ndogo tu.
 
Back
Top Bottom