Mradi wa Ujenzi wa Mji wa Kigamboni ulioanzishwa na NSSF (Dege Eco Village) unapigwa mnada

Mradi ni tsh billion 78 zilizo fisadiwa billion 179! Inawezekanaja mradi uwe na thamani ndogo kuliko pesa iliyopotea?

Sent using Jamii Forums mobile app
na kesi kama hizi,mahakamani haiwezekani kushinda,
no wonder kesi haziishi,maana mahakimu wanashindwa watahukumu vipi kwa ushahidi wa kimajungu.

Jaji mkuu anataka kesi ziishe haraka lakini kesi hazihukumiki,mwisho wa siku DPP anaondoa mashitaka
 
Huyo Mama wa Yono wa pili kama akili zake sio nzuri kidogo anataka diaspora wa Kitanzania wanunue Nyumba ni kama mtu asiyesikiliza habari za nchi hii... Akamuulize kwanza Lukuvi alisema nini kuhusu hao Diaspora... Walivyokuwa navyo mwanzo wamenyang'anywa sasa anawaambia wanunue ili wanyang'anywe tena? ni uchizi kabisa huu...
 
Tanzania tushaambiwa sio sehemu salama kiuwekezaji... Yono wajiuzie tu wenyewe... tukijitokeza tutaambiwa Pesa tumezipata wapi na tutaambiwa ni wapiga Deal...

Wamuuzie Dau am sure atapata wawekezaji... Dr. Dau ni mtu wa Maendeleo... na Sio Mshamba wala Limbukeni...
 
nssf ma director ni matajiri wa kutupa.. wamepiga sana hela kwenye hii miradi...

hapo bei waliyonunua kiwanja ukiambiwa utalia... msumari kilo moja tu unakuta wamenunua laki 1....

hapo wame inflate bei za vifaa si mchezooo
Hekari moja iliuzwa milioni 800 aibu
 
Mradi una thamani ya bil 78 ilavufisadi bil 179! Kazi ipo.
Mradi umeshadoda huu, mtahangaika nao kuuza na pesa meshazitia chooni. Tz uwekezaji ni maigizo tu.
 
Hiloo ndoo tatizo kubwa la kuwa na akili ndogo kutaka kutawala akili kubwa haiwezekan hata Kidogo!
 
Hatukuwahi kusikia NSSF inayumba au kujiendesha kihasara awamu ya nne. Sasa hivi kila kitu kitavurugika kisingizio kikiwa ufisadi na upigaji dili.

Hao waliowekwa ni wabovu hawajui walifanyalo. Nina uhakika wangekuwepo waliouanzisha huo mradi ungekamilika na ungekuwa na projected returns/profit licha ya changamoto.
 
mi nachoshwa na lugha za kibiashara Tanzania ! Hivi Yono mnajua kuwa nafasi ya huyo mama inatakiwa mtu smart akiongea unatamani arudie na armudie hivi hata kwa wakenya hatuoni? Same as ATCL jamani nchi ya viwanda wekezeni kwenye customer service kwa kweli ni Janga mmama anaongea Kama Yuko na kikao cha ukoo biashara Tanzania kazi tunayo . Pili kaongeeni na Lukuvi ndo mrudi kujipendekeza kwa diaspora . Serikali yenye chuki na wananchi wake wa nje ni Maajabu
 
Mradi mkubwa wa ujenzi wa mji mpya wa Kigamboni jijini Dar es Salaam uitwao Dege Eco Village, ulioanzishwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya jamii 'NSSF' ulisimama mwaka 2016 huku ikiripotiwa kuwapo kwa ufisadi wa zaidi ya TSH bilioni 179 katika mradi huo.
Cha kufahamu ni kwamba sasa anatafutwa muwekezaji kwenye mradi huo na kazi hiyo wamepewa kampuni ya udalali ya Yono

Mradi huo unaelezwa kuwa na thamani ya dola za Kimarekani milioni 350 sawa na shilingi bilioni 78 za Tanzania



Chanzo: Millard Ayo

Huu mradi ili uwe na tija kwa taifa badae nadhani serikali ingefanya utaratibu wa kuhamisha umiliki kutoka NSSF kwenda NHC.

Wangeangalia stahiki za NSSF na kuwalipa kabla ya kukabidhiwa NHC kuliko huu udalali unaotaka kufanyika chini ya usimamizi wa kampuni ya udalali YONO.

Nina imani sana na utendaji wa ndugu Nehemiah Mchechu ambaye ni mkurugenzi mkuu wa NHC.

NHC wanauzoefu wa miradi mikubwa kama hii kwa hiyo chini ya ndugu Nehemiah Mchechu sina shaka mpango wa ule mji wa kisasa ECCO DEGE VILLAGE mambo yatakaa sawa
 
Mambo yote mazuri yaliyoanzishwa na tawala zilizopita yanaharibiwa

Serikali iliyopita haikuanzisha chochote. Rais alikuwa hana time, ni ilikuwa ni kuponda mali na kusafiri tu. Ilikuwa ni serikali ya kihuni na wizi mutupu kila kona. Chini ya Kikwete watu walikuwa wakiitafuna Tanzania utafifikiri nchi ilikuwa haina kiongozi. Kusema miladi ilianzishwa na uongozi uliopita inakuumbuwa hujui jawabu la moja kujumulisha moja, serikali zilizopita zimewaangusha Watanzania kwa wizi wa kimachomacho. Imewasaidia kwa Kuwa wengi wetu hatuna elimu bora ya kujuwa tumeibiwa tunashangilia uongozi uliopita. Ni AIBU kwa taifa. Kenya wanaiba lakini hawaibi kijinga kama viongozi wetu, wanapewa kitu kidogo, wageni wanabeba kila kitu. Wizi wa Tanzania ni wakijinga.
 
Back
Top Bottom