Mradi wa Stieglers: Mwarabu anaharibu mradi hana utaalam wala ujuzi wa kujenga bwawa, italeta hasara kubwa kwa taifa na ubora hafifu

dosama

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
912
957
Naongea kama mwananchi na kushauri kuwa kumwendekeza huyu mwarabu wa Egypt's ni hasara kwa taifa na uharibifu wa mradi na uasili wake wa stiegler's gorge unapotea kwa sababu zifuatazo.

1. Hawa waarabu wa Misri kutoka Elsewedy electric na Arab contractors kutoka Misri hawana utaalamu wowote wa ujenzi wa bwawa kubwa kama la mwalimu nyerere wanatembelea nyota ya mchina waliyempa almost 90% ya mradi. Huyu mwarabu hata idea ya mining kwa manpower aliyokuja nao ni zero kabisa. Wazawa ndio wanaowafundisha kazi hawa wanaojiita maengener toka misri.

Ulipuaji wa miamba inafanyika kama vile hakuna site plani ya kujua kazi inatokea hapa inaenda kule wao kila siku wanakuja na plan mpya yaani haijulikani kesho itafanyika kazi gani.

2. Walio wengi wanahusika security kuhakikisha nani kaingia site, katoka na nini na kuandaa vibali pia administration na accomodation ambapo nadhani hii kazi wazawa kupitia suma jkt wanaweza kuifanya.

3. Wafanyakazi wengi wazawa mikataba yao na maslai yao sio mazuri na mahusioano kati ya mwarabu na mtanzania yako kibaguzi utadhani enzi za utumwa, wana mentality za kitumwa sana na kutomjali mwafrika.

4. Kazi inayoonekana inafanyika anafanya mchina toka kampuni ya Sinohydro akiwa na kampuni zake kama CBRC ndio wanafanya kazi na unaona kazi ya mchina inatoka hapa kwenda kule na sio mwarabu ambaye kama kama dalali.

5. Uongozi wa tanesco kama mwenye mradi pamoja na teku inaonekana hakuna umakini na ufatiliaji either wanajua na wasafikisha ila hakuna maamuzi au kuna kuwindana na uwoga kutoka juu.

Ushauri wangu

1. Kama hakuto athiri napendekeza huu mradi angepewa mchina utaisha kwa wakati ila huyu mwarabu hasara iliyo mbele ni kubwa sana katika pesa na wakati.
 
Usimlaumu mwarabu, huyo alijaribu bahati yake kwenye tender ilivyotangazwa akashinda, mlaumu aliempa kazi mwarabu, huyo ndie tatizo haswa, huwezi jua huyo mwarabu alitoa nini mpaka akapewa hiyo kazi.
 
Swali kwako, wewe fani yako ni ipi labda, hadi uweze kuona kwamba hawajui kazi? Kumbuka Mwendokasi wakati inajengwa mlisema hivyo hivyo leo hii ni success story, watu wanatoka ng'ambo kuja kujifunza kuhusu mwendo kasi yetu, hivyo wewe una utaalamu gani uliosomea usije kuwa unataka kuleta ubishani wa Simba vs Yanga, Diamond vs Kiba, wakati hakuna kitu unajua kuhusu Dam construction, ...
 
Kama ndivyo basi tujiulize Mhandisi mshauri yule mbongo ambaye anauzoefu china na italia hadi japan anaweza kazi aliyopewa?
Waziri mkuu na maofisa wengine waandamizi wa serikali hawakuliona hilo kabla na baada ya ziara yao?

Au mafao ndiyo kikwazo kwako
 
Swali kwako, wewe fani yako ni ipi labda, hadi uweze kuona kwamba hawajui kazi? Kumbuka Mwendokasi wakati inajengwa mlisema hivyo hivyo leo hii ni success story, watu wanatoka ng'ambo kuja kujifunza kuhusu mwendo kasi yetu, hivyo wewe una utaalamu gani uliosomea usije kuwa unataka kuleta ubishani wa Simba vs Yanga, Diamond vs Kiba, wakati hakuna kitu unajua kuhusu Dam construction, ...
Ni kweli kabisa. Mradi ulijengwa kwa utaalam wa hali ya juu na mifumo ya kisasa. Hasa katika kituo cha jangwani ambacho kina mifumo ya kitaalam ya kudhibiti maji muda wa mvua. Pia mfumo wa kisasa wa kadi za kukatisha tiketi uliowekwa ni wa utaalam wa hali ya juu. Pamoja na mbinu za kisasa za kisasa za kubanana kwenye gari. Kwa kweli ni utaalam wa hali ya juu. Inawezekana anabisha kwa kuwa hana utaalam wowote.
 
Ni kweli kabisa. Mradi ulijengwa kwa utaalam wa hali ya juu na mifumo ya kisasa. Hasa katika kituo cha jangwani ambacho kina mifumo ya kitaalam ya kudhibiti maji muda wa mvua. Pia mfumo wa kisasa wa kadi za kukatisha tiketi uliowekwa ni wa utaalam wa hali ya juu. Pamoja na mbinu za kisasa za kisasa za kubanana kwenye gari. Kwa kweli ni utaalam wa hali ya juu. Inawezekana anabisha kwa kuwa hana utaalam wowote.


Tangia lini maji yakadhibitiwa?
 
Kwa upande wa serikali yetu kuna mwangalizi wa kuhakikisha vigezo, taratibu,usalama vinazingatiwa .Kwa hiyo amekaa kama boya?

kwa unafki grade one kama huu kuna kaukweli flani unakaongea na huyo mkandarasi kweli ni feki na hafai kwa ushahidi wa kumpa kazi Mchina nae kutupiga percent ya malipo ya udalali bila jasho na pia yaonesha mwangalizi mkuu wa hapo yaani Waziri wa Nishati ni feki kama ilivyokuwa enzi za Mwalimu alihangaika mpaka akakonda kila mradi kama hakuna upigaji basi hakuna usimamizi!!Nyerere alitamani kuwa waziri wa kila kitu alipoona kachoka kuzuia maji kwa mikono nchi nzima imejaa majizi akabwaga manyanga akapiga ukunga akasema yuwiiiii wabongo siwawezi ni majizi kuanzia babu anarithisha wizi mpaka mjukuu Nyerere akamtupia kijiti Mzee Ruksa na kukimbilia zake Butiama kutuliza kichwa chake!! Mkulu akiunda tume kuchunguza zoezi zima la hiyo tenda lazima atapata wa kuwatumbua sababu katika maombi yao waarabu walipaswa kusema si wao watakaochimba bwawa kama hawakusema hiyo yatosha kuwafukuzilia mbali na kubaki na hao wachina Mkulu amewashindwa?

Mradi huu ni mkubwa wenye maslahi makubwa kwa raia wote yafaa kuvunja mkataba na Watu wa Egypt na kuwapa mkataba hao wachina wanaojenga ili tupunguze costs na bureaucracy na kumuondoa mtu wa kati ili mradi uishe kwa wakati, yafaa Mkulu apewe activity plan yote ikiwa na dates za kila stage of implementation na awe kila three months anaenda mwenyewe kukagua kama reality ina reflect what is on the paper!! akikuta karatasi na reality ni tofauti hiyo ni kigezo cha kuvunja mkataba, heri nusu shari kuliko shari kamili!! huu ni mradi mkubwa wa kimkakati uliomshinda Nyerere na wengine waliomfuatia , ni mradi utakaoacha alama ya Mkulu na Chato kwa karne nyingi! Mkulu asione aibu kuwaita mawaziri na kuwakaripia na kubadilisha wasimamizi wa mradi , Nyerere aliwachekea kina Kambona akavuna mabua!!

Wakati huu mawaziri wake Mkulu wote wamepagawa na majimbo yao wanahangaika kuhonga huko vijijini warudi bungeni ni muda miradi yote itavurugika na kukosa usimamizi Mkulu awe makini!! ni ngumu Mkulu kushtuka kuwa serikali iko likizo kwa mawaziri wake kuhangaikia urais na ubunge sababu yeye Mkulu sote tunajua hana upinzani kwenye kiti chake kupitia kazi bora aliyowafanyia watanzania na systemic threat kwa kila mwana CCM anaetaka kupimana nae ubavu , vitisho vilivyopo ni grade one wanafki wote wa sisiem wanaotaka kugombea urais bara wamekunja mikia, wengine wametupiliwa mbali kina Maembe!! Mkulu for five months from now needs to create a small taskforce kuangalia miradi mikubwa kwakuwa mawaziri wake hawamsikilizi na hawatulii now wanasaka kura!!na kama wachumia tumbo wengine nchi hii ni haki yao kuhangaika majimboni kusaka ugali wa familia zao!! Mkulu needs to be waziri wa kila kitu temporarily!!
 
Kwa hilo la waraarabu kukuchukulia kama mtumwa naweza kulielewa maana ni kawaida ya watu wa jamii karibu dhidi ya mtu mweusi, wanatubagua na wengi hawatupendi. Ila kwa suala la kwamba sio wajuzi, hawana uwezo na kwamba wanauharibu mradi hapo nadhani ni zile stori za ma engineer mwitu na stori zao za vijiweni za kujua kila kitu
 
We una utaalamu kiasi gani au ndio utaalam kwenye mambo ya majungu na fitna za kiafrika?

Najua unatamani mradi ufeli ili upate cha kuongea, kwa uwezo wa Mungu mradi utaisha na nchi itanufaika sana
kama angependa mradi ufeli basi asinge shauri mradi kupewa mchina ili ukamilike kwa wakati na usahihi.

ume comment kihisia na chuki
 
Back
Top Bottom