Mradi wa songa - bora uvunjwe hauna maslahi na tanzania. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mradi wa songa - bora uvunjwe hauna maslahi na tanzania.

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Macos, Jul 21, 2011.

 1. Macos

  Macos JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2011
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 1,831
  Likes Received: 1,003
  Trophy Points: 280
  Mradi wa gesi ya songo songo unajulikana zaidi kama songas-ambao unamilikiwa na kuendeshwa na kampuni ijulikanayo kama Pan african ni wa kijinga na hauna maslhai yoyote kwa mtanzania.kwa nini mradi huu niwizi mtumpu?'
  • kwanza Tanzania haina mamlaka yoyote ya kibiashara katika mrado huo.
  • ati Pan African wao tu ndio watazalisha gesi hiyo kuisafirisha kutoka songo songo hadi Dar es salaam kwa ajili ya kuzalisha umeme katika mitambo ya gesi ya kampuni yao nyengineSANGAS (hapa ni ujanja ujanja tu ili ionekene wanao zalisha na kusafirisha na kuzalisha umeme ni kampuni tofauti)
  • songas wao 'wananunua' gesi kuzalisha umeme na kuiuzia Tanesco
  • Tanesco hawaruhisiwi kununua na kuendesha mitambo ya umeme na kutumia gesi hio ya songo songo.
  • songas wanapaswa kulipwa kitu kinaitwa capacity charges na Tanesco eti kama Songas hawazalishi umeme na hizi ni kwa mabilioni kila mwezi. na lini mkataba huo utaisha haijulikani.
  • kama tanesco wanalipa capacity charges......bili ya kutofanya kazi kwa songas shs 3,000,000,000/= kwa mwezi basi kwa miaka zaidi ya 8 waliyoanza Songas kama utachukua wastani wa miezi 30 tanesco hawakuhitaji umeme wa songas hawa jamaa wameshajichukulia zaidi ya 90 billions..!! na katika hio miezi mingine tanesco wananunua umeme kutoka kwa songas kwa bei kubwa
  • hawa songas walijenga pipeline ya kusafirisha gesi ndogo wakati wanajua wazi matumizi ya gesi yataongezeka ila walifanya makusudi ili wafanye tena mradi wa upanuzi hivyo wamepata kisingizio cha kukopa na deni watasema litachukua miaka 100 hii itaonndoa nafasi yoyote ya serikali kuingia hapo na kufanya uzalishaji .
  • lakini kwa nini tanzania ama serikali wakubali kupanua pipeline hii? kuna maslahi gani?
  • tunachohitaji kutoka na gesi ya songo songo ni kuzalisha umeme basi... hatutaki gesi hio kutumiwa kwa kitu chengine sasa ni wazo wazo la mwanzo la kuzalisha umeme huko huko songo songo ndio sahihi na lina maslahi.
  • wakati ule kuna watu walipiga kelele kwamba ni bora hayo majenereta yapelekwe songo songo na serikali igharamie kujenga nyaya hadi kwenye gridi ya taifa.
  • kama gesi ile ipo ya kutosha na serikali haijatapeliwa basi tatizo la umeme haliwezi kuendelea kwani kila mwaka tukiweka mkakati wa kupeleka generator moja huko songosongo basi hata mvua isiponyesha karne nzima umeme utapatikana.
  • kujenga na kuzalisha umeme kule songo songo ni rahisi zaidi na investment yake ni mara moja.....yaani kuunganishwa na gridi ya taifa.
  • lakini pipeline gharama yake ni kubwa ,, kusukuma gesi , maintanance yake ni gharama.na sasa kama tulivo ona pipe ni ndogo inabidi iongezewe
  • tunajua hawa wazungu waloshikilia mradi huu hawawezi kukubali kuitumia gesi yetu kujitosheleza na umeme lakini ni vyema ikataifishwa hawa jamaa wakalipwa fidia.tukazalisha hii gesi wenyewe kwa kuanzisha conmpany ya taifa ya gesi na wao watawauzia Tanesco kwa bei ya chini ya kibiashara.
  • lakini haya yanataka mwanaume wa kweli kama Ghadafi...
  • ni aibu kubwa kwamba nchi hii ina gesi lakini hatuwezi kuzalisha umeme na nchi ipo kwenye giza...aibu kubwa.
  • lakini cha kushangaza hakuna hata mbunge ambaye analaumu kwamba mradi wa songo tumehujumiwa...
  • watanzania tunaonekana wa ajabu kweli kwenda kuomba omba wakati tuna gesi kuzalisha umeme.
  • lets go to china , au malaysia au india kama ni technoligia inatushinda....
  • ukweli tunahitaji mapinduzi makubwa ya akili ili tufike....kwa kwa kweli hatuna sababu ya kuwa gizani..
  • wabunge taifisheni songo songo ni mradi unao filisi Tanesco.
   
 2. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2011
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,692
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  Tunahitaji mapinduzi ya serikali, kwa kura au kwa shari. Nitaambiwa mchochezi au muhaini. Liwalo na liwe.
   
Loading...