Mradi wa SGR umeendeshwa vibaya na utalitia Taifa hasara kizazi hadi kizazi

Nimewahi kuhoji zaidi ya mara moja humu jukwaani kwa washabiki wa hiyo reli ya SGR, je ni faida gani inapatikana kutoka kwenye reli ya kati na TAZARA, mpaka tuamini SGR itakuwa na ufanisi kuliko hizi zilizopo? Sioni majibu ya maana zaidi ya propaganda mfu. Nilisema iwapo watu wanaamini hiyo SGR itakuwa na ufanisi,ni kipi kinafanya huu mradi wa mwendo kasi uendeshwe kwa ufanisi duni, wakati abiria ni wa kumwaga?
Hivi changamoto ni mradi haufai au changamoto ni uendeshaji mbovu wa mradi?kwenye mwendokasi umesema vyema,abiria wapo wakutosha,Shida nini?nadhani itafutwe dawa ya usimamizi na uendeshaji mzuri wa hii miradi na sio kusema haifai kabisa
 
Ni mpaka tutakapobadili katiba na kuambiana ukweli kwamba ujamaa umeshindikana. Hizi biashara tuwape wazawa ambao wako serious serikali kusanya kodi na kulinda muslahi ya waajiriwa kama nchi za Magharibi. Vinginevyo hakuna jipya atakuja rais huyu "ubinafsishaji" akija mwingine "rudisha serikalini".Miaka inaenda😭
Unamaanisha hakuna nchi ambako serikali zimefanikiwa kuendesha miradi kama hii ya reli au ndege?hivi Fly Emirates ni Kampuni binafsi,au ya Serikali?Ethiopia Airline je?tutafute tiba ya kuhakikisha haya mashirika na hii miradi inaendeshwa kwa ufanisi na sio kulalamika tu
 
Mwaka 1970-1974 mchina alijenga reli ya Tazara ya kisasa kwa wakati huo na watanzania waliaminishwa makubwa Sana juu ya faida ya mradi husika. Miaka 25 tu baada ya mradi kukamilika reli ikachoka, ikakosa wateja, usimamizi mbovu. Zile hadithi na simulizi tamu za manufaa ya mradi huo walioaminishwa watanzania hakuna Tena na njia kuu ya uchukuzi Tanzania to Zambia kubaki NI barabara ya Rami.

Pia Serikali ililithi reli ya Kati kutoka kwa mkoloni. Na reli ilibaki njia kuu ya uchukuzi Hadi miaka ya 90s katikati. Lakini shirika liliendeshwa kihuni Sana. Shirika liliuza tiketi chache Sana. Zaidi ya 80% ya abilia walilipa Ela keshi zilizoishia mikononi mwa walinzi na wafanyakazi wa shirika lenyewe.

Mpaka leo reli haikujiendesha. Inakula Kodi zetu kila siku kukarabatiwa lkn maingizo hakuna NI hasara tu.
Nisiwachoshe kabisa. Sizungumzii kbs mradi wa Mabasi ya mwendokasi unavyoumiza taifa ikiwa NI chini ya miaka kumi tu uanshwe. Serikali inamwaga fedha kuuokoa Ila watachoka tu. Mabasi kibao yameharibika yakatelekezwa na kuoza.
Ndege zipo kwaajili ya kujisifu lkn hakuna faida ya . Kila mwaka Serikali inakula lose ya mabilioni

Ambao wanachukulia Mambo kirahisi hawataelewa. Wataamini propaganda na hadidhi za bulicheka na ndoto za abunuasi za kuvuka bahati kwa kugeuza meza na kupanda juu yake.

Ukweli NI kuwa mradi utakausha kau fedha mtaani, Utajiendesha kwa hasara, hautaleta faida.

Serikali ingejitoa kabisa kwenye ujenzi na uendeshaji ikakaa kusubili kodi.
Ila Kama Serikali itafanya biashara hii ni hatari kwake na Sekta binafsi za usafirishaji. Haina ubunifu. Wanachojua Serikali NI kuwafungia Sekta binafsi ili wao wauze. Kama ilivyofanya Air Tz dhidi ya fast jet. lkn Serikali haifaidiki chochote na abiria wanaumia.

Tunaitaji reli nzuri lkn bila hakukuwa na ulazma wa Serikali yenyewe kuhusika.


Hayo matilioni yatapotea. Tulikuwa tunapiga hatua Ila Sasa tunatumia ma tilion kuliundia taifa zigo la kuhudumiwa na matilioni kila mwaka.
Kaka hoja yako Inawelekeo chanya Sana ila umeiwasilisha kinadharia Sana, no data, no cross reference! Kwa hiyo inabakia kuelea kama fiction!
 
Duniani kote ni nadra sana kupata serikali inayoweza kufanya biashara yoyote kwa faida. Biashara ni uwanja wa sekta binafsi, serikali iache kufanya biashara badala yake itengeneze mazingira mazuri ya biashara kufanyika na yenyewe ikusanye kodi.

Serikali ya Marekani hadi sekta nyeti kama ya Ulinzi imetoa fursa kubwa ya sekta binafsi kufanya kazi. Sekta binafsi inatengeneza silaha zote zinazotumika na jeshi la Marekani, zinazouzwa na kutolewa misaada nje ya nchi. Karibia vinu vyote vya nyuklia Marekani vinamilikiwa na makampuni binafsi, sisi bado tumebaki na mawazo ya kijima ya karne za giza ya serikali kumilik hadi ng'ombe kwenye ranchi!
Ni kweli serikali haiwezi kufanya biashara, lakini biashara zote kubwa zilianza kidogokidogo, makampuni mengine yalianza karne ya 18. Yakaendelea kukua kwa kufuatia uendelevu wa teknologia. Kwa sasa ni nani angeweza kujenga reli ya mwendo kasi au bwawa la Nyerere au miradi mikubwa inayofanyika sasa? Hao wawekezaji walikuwa hawaoni fursa hizo? Hiyo miradi kwa gahrama zake hakuna budi serikali ifanye. Inafanya hivi kwa kodi zetu kwa kutuhudumia sisi wenyewe. Faida ipo ila ni Indirect, na kama walivyosema wengine hizo ni huduma kwa wananchi. Hebu nenda vijijini uone wananchi wanavyofaidika na huduma za umeme. Isingewezekana umeme kutoka Njombe, Songea mpaka Mtwara ujengwe kwa kutegemea faida, hicho kitu hakingewezekana milele, Mtanzania gani angeweza kulipia? Tuliona huko nyuma gharama halisi ya kuingiza umeme nyumbani ilikuwa ni zaidi ya laki sita, huko vijijini wangeweza? Tunachotakiwa kufanya ni kuhakikisha miradi hii baada ya kukamilika ijiendeshe yenyewe. Tuendelee kulipa kodi ili Watanzania wenzetu wafaidike, sisi tunaoongea sana tuko mijini hatujui maisha ya tabu wanayoyapata wenzetu vijijini.
 
Anaongea jambo la muhimu serikali sio wabunifu na hawawez competition si umeona kwenye airtavel wameua baadhi ya Makampuni yenye nguvu kama fastjet
Complain ya jamaa ina msingi isijekuwa wakalazimisha mizigo kupita kwenye reli na kuua biashara ya malori wakati watu wame invest billion of dollars
Biashara ya malori itakuwepo tu kwani wenye bidhaa wataangalia na gharama nyingine za usafirishaji. Reli haifiki kila eneo lakini malori yanafikisha mzigo mpaka mlangoni. Hata abiria vile vile. Kama unakwenda Chalinze kutoka Morogoro, utapanda treni ya mwendo kasi au utapanda basi? Sasa hivi mabasi mengi hayachukui abiria wanaoshukia njiani vinginevyo ulipe nauli ya mpaka mwisho wa safari, ikiwepo reli ya mwendo kasi hii kero itaondoka tu.
 
Bado sijapata jibu hivi ni kwa nini SGR isingeanzia Pugu...kulikuwa na haja gani kujenga daraja la juu namna hii kwanza kuokoa gharama pia nafasi (msomgamano) katikati ya jiji.
 
Watakuja kukuelewa tu
Nimewahi kuhoji zaidi ya mara moja humu jukwaani kwa washabiki wa hiyo reli ya SGR, je ni faida gani inapatikana kutoka kwenye reli ya kati na TAZARA, mpaka tuamini SGR itakuwa na ufanisi kuliko hizi zilizopo? Sioni majibu ya maana zaidi ya propaganda mfu. Nilisema iwapo watu wanaamini hiyo SGR itakuwa na ufanisi,ni kipi kinafanya huu mradi wa mwendo kasi uendeshwe kwa ufanisi duni, wakati abiria ni wa kumwaga?
 
Back
Top Bottom