Mradi wa SGR umeendeshwa vibaya na utalitia Taifa hasara kizazi hadi kizazi

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
1,657
2,252
Mwaka 1970-1974 mchina alijenga reli ya Tazara ya kisasa kwa wakati huo na watanzania waliaminishwa makubwa Sana juu ya faida ya mradi husika. Miaka 25 tu baada ya mradi kukamilika reli ikachoka, ikakosa wateja, usimamizi mbovu. Zile hadithi na simulizi tamu za manufaa ya mradi huo walioaminishwa watanzania hakuna Tena na njia kuu ya uchukuzi Tanzania to Zambia kubaki NI barabara ya Rami.

Pia Serikali ililithi reli ya Kati kutoka kwa mkoloni. Na reli ilibaki njia kuu ya uchukuzi Hadi miaka ya 90s katikati. Lakini shirika liliendeshwa kihuni Sana. Shirika liliuza tiketi chache Sana. Zaidi ya 80% ya abilia walilipa Ela keshi zilizoishia mikononi mwa walinzi na wafanyakazi wa shirika lenyewe.

Mpaka leo reli haikujiendesha. Inakula Kodi zetu kila siku kukarabatiwa lkn maingizo hakuna NI hasara tu.
Nisiwachoshe kabisa. Sizungumzii kbs mradi wa Mabasi ya mwendokasi unavyoumiza taifa ikiwa NI chini ya miaka kumi tu uanshwe. Serikali inamwaga fedha kuuokoa Ila watachoka tu. Mabasi kibao yameharibika yakatelekezwa na kuoza.
Ndege zipo kwaajili ya kujisifu lkn hakuna faida ya . Kila mwaka Serikali inakula lose ya mabilioni

Ambao wanachukulia Mambo kirahisi hawataelewa. Wataamini propaganda na hadidhi za bulicheka na ndoto za abunuasi za kuvuka bahati kwa kugeuza meza na kupanda juu yake.

Ukweli NI kuwa mradi utakausha kau fedha mtaani, Utajiendesha kwa hasara, hautaleta faida.

Serikali ingejitoa kabisa kwenye ujenzi na uendeshaji ikakaa kusubili kodi.
Ila Kama Serikali itafanya biashara hii ni hatari kwake na Sekta binafsi za usafirishaji. Haina ubunifu. Wanachojua Serikali NI kuwafungia Sekta binafsi ili wao wauze. Kama ilivyofanya Air Tz dhidi ya fast jet. lkn Serikali haifaidiki chochote na abiria wanaumia.

Tunaitaji reli nzuri lkn bila hakukuwa na ulazma wa Serikali yenyewe kuhusika.

Hayo matilioni yatapotea. Tulikuwa tunapiga hatua Ila Sasa tunatumia ma tilion kuliundia taifa zigo la kuhudumiwa na matilioni kila mwaka.
 
Umeandika jambo kubwa lakini bila vielelezo na uthibitisho mfano umeandika serikali inatoa fedha kwenye mradi wa mwendokasi ilitakiwa useme inatoa kiasi gani na mradi unapata hasara kiasi gani na kwanini unashindwa kujiendesha.Umeandika kuhusu SGR lakini sijaona facts kuthibitisha mradi utashindwa.
 
LOooh, mkuu 'William Mshumbusi', umeweka bonge la mada hapa, lakini najua, kama kawaida yetu siku hizi hapa JF, tutaigusagusa tu na kwenda zetu kwenye utani wetu wa CCM na CHADEMA!

Umeanza na mfano mzuri sana wa TAZARA, jinsi reli ile ilivyojengwa haraka na kwa ufanisi na wachina. Madhumuni wa ujenzi wa reli ile ulijulikana bayana, kuondokana na utegemezi wa nchi za mstari wa mbele katika ukombozi kuwategemea makaburu katika maswala yao ya uchukuzi na usafirishaji wa mizigo yao.

Kabla ya mchina kujenga ile reli, wafadhiri wa nchi za Magharibi waliombwa kusaidia kuijenga, wakang'aka, huku wakisema reli eneo hilo haina faida. Hao hao, walipoona mchina anaijenga reli, haraka wakawa mbioni kwenye ujenzi wa barabara. Unaweza kutafsiri mwenyewe maana ya hayo yote.

Reli, kama ulivyoeleza ilifanya kazi vizuri mwanzoni mwa utumikaji wake, na umeeleza kwa nini kadri miaka ilivyoendelea, ndio ufanisi wake ulivyozidi kufifia hadi sasa.

Binafsi ningependa sana ukazie hapa, penye udhoofu wa ufanisi. Ueleze sababu hasa ni zipi, pamoja na kwamba umegusia kama kawaida yetu sote siku hizi, lawama za kwamba serikali haiwezi kufanya biashara. Mimi sikubaliani na jibu hilo jepesijepesi hivyo. Serikali inaweza sana kufanya mambo yake kwa ufanisi iktaka kufanya hivyo. Nyakati hizi haifanyi hivyo kwa sababu mbalimbali, ikiwemo hiyo ya sekta binafsi unayoipigia chapuo hapa, ikiwa ndio kikwazo kikubwa sana katika kudhoofisha shughuli za serikali.

Wenye malori bila shaka hawawezi kulaza damu wakiona shughuli za reli zinafana huku zikiwapunguzia wao wanachokitafuta. Tunaweza sana kulijadili hili, hata kama hatuwezi kukubaliana.

Matatizo yanayojitokeza ndani ya mashirika ya umma, yanaanzia huko huko kwenye sekta binafsi, na ukosefu wa usimamizi bora ndani ya mashirika yenyewe. Hii haimaanishi kwamba udhaifu huo hauwezi kudhibitiwa kama serikali ikiamua na kuwa na nia ya kufanikisha shughuli zake. Kusema serikali haiwezi kufanya biashara, ni sawa pia na kusema serikali haiwezi kufanya shughuli yoyote kwa ufanisi. Kwa hiyo tuondoe serikali tubinafsishe shughuli zote zinazofanywa na serikali?

Tusifanye uwekezaji ndio uwe muarobaini wa matatizo yetu, kila mara tunaposhindwa kwa uzembe tu, eti tukimbilie kwenye uwekezaji.
 
Nimewahi kuhoji zaidi ya mara moja humu jukwaani kwa washabiki wa hiyo reli ya SGR, je ni faida gani inapatikana kutoka kwenye reli ya kati na TAZARA, mpaka tuamini SGR itakuwa na ufanisi kuliko hizi zilizopo?

Sioni majibu ya maana zaidi ya propaganda mfu. Nilisema iwapo watu wanaamini hiyo SGR itakuwa na ufanisi,ni kipi kinafanya huu mradi wa mwendo kasi uendeshwe kwa ufanisi duni, wakati abiria ni wa kumwaga?
 
Pili si kila mradi wa serikali upo pale kuleta faida, mingine inakuwa ni vichocheo vya uchumi

Kwani wewe ukiona serikali inajenga barabara za lami kwa mabilioni ya shillingi unategemea serikali ipate faida ya moja kwa moja?
 
Nimewahi kuhoji zaidi ya mara moja humu jukwaani kwa washabiki wa hiyo reli ya SGR, je ni faida gani inapatikana kutoka kwenye reli ya kati na TAZARA, mpaka tuamini SGR itakuwa na ufanisi kuliko hizi zilizopo? Sioni majibu ya maana zaidi ya propaganda mfu. Nilisema iwapo watu wanaamini hiyo SGR itakuwa na ufanisi,ni kipi kinafanya huu mradi wa mwendo kasi uendeshwe kwa ufanisi duni, wakati abiria ni wa kumwaga?

Ni jambo Jema sana Mradi kujiendesha,
Lakini Muhimu zaidi na lengo namba moja la serikali inatakiwa iwe ni kutoa huduma kwa wananchi, profit iwe ni lengo la pili,
Ziko nchi kama China hawa madereva Wa madaladala wanalipwa kama wafanyakazi Wa umma. They know this.
 
Kwa hiyo mwendo kasi ni huduma au biashara? Ukiniambia shule za msingi ni huduma nitakuelewa, sio hayo mabasi yanayojaza abiria wanaolipa nauli mpaka mlango inakuwa shida kuufunga.
 
Umeandika jambo kubwa lakini bila vielelezo na uthibitisho mfano umeandika serikali inatoa fedha kwenye mradi wa mwendokasi ilitakiwa useme inatoa kiasi gani na mradi unapata hasara kiasi gani na kwanini unashindwa kujiendesha.Umeandika kuhusu SGR lakini sijaona facts kuthibitisha mradi utashindwa.
Kwa hiyo kilichoandikwa ni uongo?
 
Ni jambo Jema sana Mradi kujiendesha,
Lakini Muhimu zaidi na lengo namba moja la serikali inatakiwa iwe ni kutoa huduma kwa wananchi, profit iwe ni lengo la pili,
Ziko nchi kama China hawa madereva Wa madaladala wanalipwa kama wafanyakazi Wa umma. They know this.
Nafikiri kwa uwekezaji, unaofanywa kwenye Reli,ni lazima lengo.liwe n biashara.
Nina mashaka makubwa na hii miradi ya Mwendazake!
Kuna kila dalili tutakujakulia huko mbeleni.
Nafikiri kinachoendelea Kenya kwenye SGR ya Nairobi Mombasa ni mfano.mzuri ,sana!
Haiwezekani nchi ikajiingiza kwenye miradi mikubwa hivi ,bika mjadala wa kutosha!
 
Nimewahi kuhoji zaidi ya mara moja humu jukwaani kwa washabiki wa hiyo reli ya SGR, je ni faida gani inapatikana kutoka kwenye reli ya kati na TAZARA, mpaka tuamini SGR itakuwa na ufanisi kuliko hizi zilizopo? Sioni majibu ya maana zaidi ya propaganda mfu. Nilisema iwapo watu wanaamini hiyo SGR itakuwa na ufanisi,ni kipi kinafanya huu mradi wa mwendo kasi uendeshwe kwa ufanisi duni, wakati abiria ni wa kumwaga?
Kinachofanya mradi wa mwendo kasi usijiendeshe kwa ufanisi wakati abiria wa kumwaga ndicho kitakafanya SGR isijiendeshe kwa ufanisi!

Uvivu, ufisadi na ujinga wa mwafrika
 
Kinachofanya mradi wa mwendo kasi usijiendeshe kwa ufanisi wakati abiria wa kumwaga ndicho kitakafanya SGR isijiendeshe kwa ufanisi!

Uvivu, ufisadi na ujinga wa mwafrika
Kwa muundo, mifumo na desturi za serikali inaweza kuwekeza na kuendesha miradi hiyo kibiashara kweli? Nina mashaka. Katika mazingira ya soko huru na ushindani sidhani ,huko nyuma tulishindwa leo tutaweza kweli. Tungeenda na utaratibu wa PPP ingewezekana.
 
Back
Top Bottom