Mradi wa one stop border Horohoro,Wakenya wamewazidi fikira watawala wetu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mradi wa one stop border Horohoro,Wakenya wamewazidi fikira watawala wetu.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by matongo manawa, Aug 9, 2012.

 1. m

  matongo manawa JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2012
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 336
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nimepita ktk mpaka wa Horohoro nikitokea Mombasa nikaona upande wa Kenya uko bize na ujenzi wa majengo na
  nyumba za watumishi kwa kasi kubwa afisa niliyeongea naye aliusifia sana mpango huo nami nikamwelewa kweli
  baada ya mradi kukamilika hakutakuwa tena na uchelewaji.

  Nikaja upande wa Tanzania ndo nikachoka,tofauti na Wakenya wanaokwenda kasi,
  Kwetu kuna jengo moja la ghorofa moja ambalo lina muda miezi Saba toka lianze kunengwa site ipo kama imekufa vifaa duni.

  Nikapenya penya nikampata staff mmoja wa pale mpakani nikamwuliza vipi mbona
  mradi wetu unasuasua wkt wenzetu wameanza juzi na inaonekana wako serious?
  Jamaa akaiuliza wewe huijui Tz?kila kitu sanaa wenzetu ona akanionesha upande wa Kenya eneo lote la mpaka wanalifance kwa tofari pili ujenzi wa ofisi unaenda
  sambamba na ujenzi wa nyumba za watumishi,hapa kwetu watumishi tulivunjiwa
  nyumba tukaambiwa tujitafutie makazi serikali yetu haitujali.

  Baada ya mazungumzo nikapanda zangu basi,
  Jirani na pale mpakani sikuona nyumba za kufaa hata kupanga watumishi,nikajiuliza
  wenzetu Wakenya wao wanapata wapi fikira chanya hizi?
  Wenzetu wanaona mbali,hata watawala wetu wakija kukagua mradi huu hawzioni
  changamoto hizi ambazo mimi mpita njia nimezibaini?
  Walikaa na watumishi kabla ya mradi wakapewa mahitaji Mahususi?

  Watanzania mbona tunataka kuwa nyuma kwa kila kitu?
   
 2. mndwadage

  mndwadage JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 345
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuu watawala wetu wamekata tamaa wanaongoza bora liende!
   
 3. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  bongo kila kitu ni hivyo sana..Ikulu tu imepakwa rangi miaka ya juzi juzi na kiongozi mmoja mkubwa sana wa serikali akaja na kujisifu "NA TUMEPAKA RANGI IKULU KWA HIYO WAPINZANI WATAENDELEA KUPAONA TU KWA MBAALI". so don't mind this is the TANZANIA TANZANIA NAKUPENDA KWA MOYO WOTE
   
Loading...