Mradi wa nyumba za kuuza (PSPF, PPF, NSSF) wa Buyuni Dar es Salaam

KASRI

Member
May 2, 2009
93
22
Salaam wana JF!
Kuna mradi mkubwa wa kujenga nyumba za kuuza unaoratibiwa na PSPF, PPF nadhani na NSSF uliopo eneo liitwalo Buyuni - Chanika jijini Dar es Salaam. Ninamiliki kiwanja eneo hilo pia na Hati ninayo. Nimefika eneo hilo leo nikakuta nimezungukwa na nyumba zilizokwisha anza kujengwa na hayo mashirika. Niliowakuta eneo hilo kwa leo wakaniambia huwa wanajenga kiwanja chochote kilichowazi/hakijaendelezwa.
Kwa mwenye kufahamu juu ya hili naomba kufahamishwa.
Nawasilisha
 
Du umenitisha!!! maana tuna kiwanja na sie huko. Sidhani kama wana mamlaka ya kufanya hivyo bila hata kututaarifu. Any way ntaenda na mimi kesho huko.
 
salaam wana jf!
Kuna mradi mkubwa wa kujenga nyumba za kuuza unaoratibiwa na pspf, ppf nadhani na nssf uliopo eneo liitwalo buyuni - chanika jijini dar es salaam. Ninamiliki kiwanja eneo hilo pia na hati ninayo. Nimefika eneo hilo leo nikakuta nimezungukwa na nyumba zilizokwisha anza kujengwa na hayo mashirika. Niliowakuta eneo hilo kwa leo wakaniambia huwa wanajenga kiwanja chochote kilichowazi/hakijaendelezwa.
Kwa mwenye kufahamu juu ya hili naomba kufahamishwa.
Nawasilisha

hizo nyumba ni nzuri?
Utaratibu wa kuzinunua ukoje?
Bei zake zikoje?
Na lini wataanza kuuza?
Asante!
 
Du umenitisha!!! maana tuna kiwanja na sie huko. Sidhani kama wana mamlaka ya kufanya hivyo bila hata kututaarifu. Any way ntaenda na mimi kesho huko.

Sawa mkuu, ukipata taarifa rasmi naomba tushirikishane maana kama tetesi nlizosikia ni kweli basi wengi tutaumia.
 
hizo nyumba ni nzuri?
Utaratibu wa kuzinunua ukoje?
Bei zake zikoje?
Na lini wataanza kuuza?
Asante!

Sina taarifa zaidi kuhusu hizo nyumba ila nimeziona physically nyingi zimeshapauliwa nadhani wako kwenye finishing sasa. Zipo za 2 bedroom, 3 bedroom. Kimsingi ni eneo ambalo litakuwa na watu wengi siku zijazo. Pia ipo shule ya kanisa (masista) katoliki wanaijenga kwa kasi ya ajabu - hii inanipa moyo kuwa hata huduma za jamii muhimu (maji, umeme, hospitali, barabara, makanisa, misikiti nk) zitapatikana mapema.
 
Wana viwanja vyao wala hawagusi kiwanja cha mtu...subiria zikiisha ukaombe kununua zipo kama 800 hivi!

Kaa utulie na kiwanja chako!!
 
Wana viwanja vyao wala hawagusi kiwanja cha mtu...subiria zikiisha ukaombe kununua zipo kama 800 hivi!

Kaa utulie na kiwanja chako!!

Asante Skills4ever kwa kunipa moyo maana nilihisi naingia kwenye mgogoro wa ardhi karibuni.
 
Back
Top Bottom