Kinumbo
JF-Expert Member
- Dec 8, 2019
- 2,742
- 4,931
Moja kwa moja kwenye dhumuni la mada hii, huu mradi wa mwendo kasi kutoka Kariakoo mpaka Mbagala umekuwa kero sana. Si asubuhi, mchana ama usiku ni kero mtindo mmoja, kero yenyewe ni kujitokeza foleni. Yaani huu mradi umefanya iwepo kamba ya maana si mchezo. Hivi hiyo kampuni ama serikali haioni huo usumbufu ili kutafuta njia mbadala.?
Foleni kuanzia pale uhasibu inakwenda mpaka kwa Azizi Ally kisha itapoa mpaka Misheni. Baada ya hapo utaitafuta foleni nyingine kuanzia Kizuiani mpaka Mbagala Rangi tatu hii kamba ndio hatari sasa. Foleni kutoka Kizuiani mpaka Mbagala rangi tatu unaweza ukalala kwenye usafiri mpaka ukaota ndoto kabisa.
Kero hii imesababisha baadhi ya wasafiri kushuka na kutembea kwa miguu kutoka Kizuiani mpaka Mbagala. Pia kwa kero hii imepelekea kupoteza mda mwingi sana.
Kwann Serikali ama wanao endesha mradi huu wasitafute ufumbuzi mbadala? Tofauti na barabara hizo zilizo kwenye mradi pembezoni mwa mji kuna barabara za vumbi wameshindwa nn kupitisha greda ili kusawazisha mashimo kisha zitumike kwa wakati huu ili kuondoa hii kadhia.