Mradi wa mabasi yaendayo kasi(DART) , ni kielelezo tosha kuwa miradi ya aina hii haipumbazi wananchi(wapiga kura)

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,011
144,371
Mradi huu ulipuzinduliwa Agost 17,2015, wenzetu hawa waliamini kuwa mradi huu ungekuwa ni mtaji mkubwa kwa chama tawala(CCM) katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 hasa katika jiji la Dar-es-Salaam.

Kama haitoshi,ilipofika September 20,2015 yaliwasili mabasi 138 kwa ajili ya mradi huo na kuongeza hamasa ya hawa wenzetu kuwa CCM ina nafasi kubwa ya kushinda katika jiji la Dar-es-Salaam kutokana na kuanza kwa huu mradi.

Kwa ushahidi,pitia huu uzi usome comments za vijana wa Lumumba kama kina YEHODAYA na wengineo.

Uzinduzi wa Mradi wa Mabasi yaendayo Kasi(BRT) Dar - Agosti 17, 2015

Nakumbuka moja ya kauli iliyokuwa ikichagiza ujio wa mradi huu ni maelezo kwamba huu ulikuwa ni mradi mkubwa wa aina yake katika nchi za Afrika Mashariki(sisi tukiwa ndio wa kwanza kuwa na mradi wa aina hii).

Hata hivyo,licha ya mradi huu kuzinduliwa ikiwa ni takribani miezi 2 kabala ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015,bado jiji la Dar na Manispaa zake zilichukuliwa na UKAWA kwa kiasi kikubwa na ikiwa ni mra ya kwanza kwa wapinzani kushinda viti vingi vya udiwani na ubunge katika jiji hilo.

Hivyo hili ni funzo kwa hawa wenzetu wanaoamini hii miradi mikubwa ndio itawabeba mwaka 2020.

Niwaambie tu angali mapema kuwa,mkiweka kipaumbele kikubwa katika hii miradi kama flyovers,n.k na kusahau mambo yanayogusa wananchi moja kwa moja kama vile ajira, uchumi,n.k, basi mjue tu ya mwaka 2015 yatajiridua tena na safari hii itakuwa ni hatari zaidi unless Tume Huru isipatiakane.

Na pia muombe Kesi ya Kikatiba ya kutaka Tume Huru na ie ya kupinga sheria ya uchaguzi isifanikiwe.

Mkipuuza maneno haya majibu mtayapata 2020 kwani kura zitaongea ukweli bila kujali nani anatangazwa mshindi.
 
Hahaaaa wala sifikirii tena kuunga foleni ya kupiga kura katika maisha yangu , kwa upumbavu aliyofanya mgombea urais aliyepita et niachieni kura zangu watu tukamwachia mpaka leo hajatoa msimamo wake zaid ya kuunga mkono na kuendekea kuua upinzani kisayansi
 
WEWE NI MCHAWI....Nyie ni binadamu gani?
Nyie kila kitu kuponda..OFISI ZA MAKAO MAKUU TU YA CHAMA MMESHINDWA KUJENGA..hiki ni kiashiria tosha hata mngepewa nchi mnGewauzia hao WAZUNGU HATA huo BRT msingeweza kujenga
Halafu unaposema Dar ni ngome ya CHADEMA kwanini wananchi wamewapuuza kwa ssa kiasi kwamba VIONGOZI WENU wanawekwa mahabusu hakuna hata viashiria vya wakazi wa dar kupinga hili kwa vitendo?
 
WEWE NI MCHAWI....Nyie ni binadamu gani?
Nyie kila kitu kuponda..OFISI ZA MAKAO MAKUU TU YA CHAMA MMESHINDWA KUJENGA..hiki ni kiashiria tosha hata mngepewa nchi mnewauzia hao WAZUNGU
Ukweli ndio huo hata ukilialia.
 
Hakuna uchaguzi bali ccm itashibda kwa kutumia tume,polisi na Tiss,kama ya siha na kinondoni,kutegemea uchaguzi huru hilo halipo na kwenyekiti qa tume qa sasa ndo hovyo kabisa nd wamekutana na mtaalam wa tisa kailima kuhakikisha anafuata maelekezo anayopewa na wakubwa wake.Ma mases wengi ni makada wa ccm unategemea hago ya haki yatatoka wapi
 
Back
Top Bottom