Pweza Dume
Member
- Apr 11, 2011
- 43
- 7
Miradi sijui ya mabasi yaendayo kasi, barabara za ghorofa na miradi ya umeme kila ninapoisikia nahisi kupata kipanda uso...
Miradi sijui ya mabasi yaendayo kasi, barabara za ghorofa na miradi ya umeme kila ninapoisikia nahisi kupata kipanda uso...
Mkataba wa ujenzi wa mabasi yaendayo kasi wasainiwa |
Thursday, 22 December 2011 19:08 |
Fredy Azzah <Mwananchi.co.tz> WAKALA wa Barabara nchini (Tanrods) na Kampuni ya ujenzi wa barabara ya M/S Strabag Internation GmbH ya Ujerumani, wamesaini mkataba wa ujenzi wa miundombinu ya usafiri wa mabasi yaendayo kasi kwa awamu ya kwanza wenye thamani ya Sh240.8 bilioni. Mtendaji Mkuu wa Tanrods, Patrick Mfugale, alisema kwa mujibu wa mkataba huo, awamu hiyo ya kwanza itajumuisha ujenzi wa barabara ya Morogoro kutoka Kimara mpaka Kivukoni Feri, barabara ya Kawawa kutoka Magomeni hadi Morocco na kutoka Fire hadi barabara ya makutano ya Nyerere (Kamata). Alisema kuwa ujenzi huo ambao unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 36 kuanzia sasa, utajumuisha vituo 29 vya kawaida vya mabasi hayo, vituo vikuu vitano, karakana mbili, ujenzi wa madaraja 3 ya watembea kwa miguu maeneo ya Ubungo, Kimara na Morocco. Alisema mkataba wa ujenzi wa mfumo huo wa barabara wenye urefu wa kilomita 20.9 unatekelezwa kwa fedha za mkopo kutoka Benki ya Dunia (WB) ambayo imetoa Sh150 bilioni. Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mradi wa Mabasi yaendayo Kasi jijini Dar es Salaam (DART) , Cosmas Takule, alisema mradi huo unakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi ya watu kukataa kuhama katika maeneo wanayotakiwa kuhama kupisha miundombinu ya mradi huo. Kuna watu wengine wanataka kulipwa fidia kubwa kuliko ilivyopangwa na wanafungua kesi mahakamani hali inayochelewesha mradi, alisema Takule. Waziri wa Ujenzi , Dk John Magufuli ambaye alishuhudia utiwaji saini wa mkataba huo, alimtaka mkandarasi anayejenga miundombinu hiyo, kuhakikisha anakamilisha ujenzi kwa wakati na ikibidi iwe kabla ya muda waliokubaliana. Dar es Salaam kuna msongamano mkubwa sana wa magari, ikibidi hakikisheni mnamaliza kazi kabla ya muda tuliokubaliana, alisema Dk Magufuli.Aliwataka pia watu wanaotakiwa kupisha ujenzi huo, kufanya hivyo haraka kwa kuwa wanachelewesha kumalizika kwa tatizo la foleni. |
LABDA MWANDISHI WA HABARI HII KACHANGANYA, HUU SIONDIO UMEISHAANZA TOKA MWEZI WA NANE MWAKA JANA NA RAISI ALIUFUNGUA?
Mkataba wa ujenzi wa mabasi yaendayo kasi wasainiwa
Thursday, 22 December 2011 19:08
Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli akiwaonyesha kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, michoro ya barabara za juu ambazo zitapunguza msongomano katika Jiji hilo. Picha na Zacharia Osanga
Fredy Azzah <Mwananchi.co.tz>
WAKALA wa Barabara nchini (Tanrods) na Kampuni ya ujenzi wa barabara ya M/S Strabag Internation GmbH ya Ujerumani, wamesaini mkataba wa ujenzi wa miundombinu ya usafiri wa mabasi yaendayo kasi kwa awamu ya kwanza wenye thamani ya Sh240.8 bilioni.
Mtendaji Mkuu wa Tanrods, Patrick Mfugale, alisema kwa mujibu wa mkataba huo, awamu hiyo ya kwanza itajumuisha ujenzi wa barabara ya Morogoro kutoka Kimara mpaka Kivukoni Feri, barabara ya Kawawa kutoka Magomeni hadi Morocco na kutoka Fire hadi barabara ya makutano ya Nyerere (Kamata).
Alisema kuwa ujenzi huo ambao unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 36 kuanzia sasa, utajumuisha vituo 29 vya kawaida vya mabasi hayo, vituo vikuu vitano, karakana mbili, ujenzi wa madaraja 3 ya watembea kwa miguu maeneo ya Ubungo, Kimara na Morocco.
Alisema mkataba wa ujenzi wa mfumo huo wa barabara wenye urefu wa kilomita 20.9 unatekelezwa kwa fedha za mkopo kutoka Benki ya Dunia (WB) ambayo imetoa Sh150 bilioni.
Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mradi wa Mabasi yaendayo Kasi jijini Dar es Salaam (DART) , Cosmas Takule, alisema mradi huo unakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi ya watu kukataa kuhama katika maeneo wanayotakiwa kuhama kupisha miundombinu ya mradi huo.
"Kuna watu wengine wanataka kulipwa fidia kubwa kuliko ilivyopangwa na wanafungua kesi mahakamani hali inayochelewesha mradi," alisema Takule.
Waziri wa Ujenzi , Dk John Magufuli ambaye alishuhudia utiwaji saini wa mkataba huo, alimtaka mkandarasi anayejenga miundombinu hiyo, kuhakikisha anakamilisha ujenzi kwa wakati na ikibidi iwe kabla ya muda waliokubaliana.
"Dar es Salaam kuna msongamano mkubwa sana wa magari, ikibidi hakikisheni mnamaliza kazi kabla ya muda tuliokubaliana," alisema Dk Magufuli.Aliwataka pia watu wanaotakiwa kupisha ujenzi huo, kufanya hivyo haraka kwa kuwa wanachelewesha kumalizika kwa tatizo la foleni.
Unalosema linawezekana lakini kumbuka pia katika kila kituo lazima kujengwe ama "underground tunnel" au "overhead passage" kwa ajili ya watu kuvuka kutoka upande wa kulia au kushoto.Barabara za bongo zina eneo kubwa katikakti, mfano kilwa raod, sam nujoma road pia haya mabasi hayahitaji barabara kubwa sana
Hicho ni kiinimacho kwa watz, jamaa alitaka sifa kwa kuahidi yasiyotekelezeka, mara reli, machnga complex, huu ni woga wa ki-kwere.
Huu mradi bado uko katika hatua za mwanzo za UJENZI. Ni juzi tu eneo la kituo kikuu (control centre) la haya mabasi ndio limekuwa cleared baada ya kuvunja zile nyumba za bandari pale Gerezani. Ujenzi utafanywa na Strabag AG kutoka German pesa ($ 200 Million) zimetolewa na World Bank. :A S-omg:Hata mimi nisaidieni kuelewa hii habari, inazidi kunichanginyi. Nimewahi kufika ulaya na kuona mabasi ya wenzetu yanavyotoa huduma na utaratibu wa ratiba zao za mabasi zilivyo. lakini hapa bongo nasikia tu mabasi yaendayo kasi sijui ni msamiati tu au ni tofauti na yale ya ulaya. je ya kwetu hapa tunaiga mfumo wa nchi gani, nikijua hiyo nchi naweza na mimi nika google walau tu kupata picha ya hayo mabasi na njia yanayopita.
Hata mimi nisaidieni kuelewa hii habari, inazidi kunichanginyi. Nimewahi kufika ulaya na kuona mabasi ya wenzetu yanavyotoa huduma na utaratibu wa ratiba zao za mabasi zilivyo. lakini hapa bongo nasikia tu mabasi yaendayo kasi sijui ni msamiati tu au ni tofauti na yale ya ulaya. je ya kwetu hapa tunaiga mfumo wa nchi gani, nikijua hiyo nchi naweza na mimi nika google walau tu kupata picha ya hayo mabasi na njia yanayopita.
MKUU MI NAONA LABDA MSAMIATI MABASI YAENDAYO KASI( BUS RAPID TRANSIT) AU (BRT) YA DAR ITAKUA DART( DAR ES SALAAM RAPID TRASNIT) MABASI YAENDAYO KASI HAINA MAANA SPEED ZAKE NI ZA KASI, INA MAANA MABASI HAYA NI YA HARAKA KWA KUWA YANA NJIA ZAO MAALUMU AMBAZO MAGARI MENGINE HAYARUHUSIWI KUPITA HIVYO KUYAFANYA MABASI HAYA YASIWE NA FOLENI NA KUWA YA HARAKA, , MABASI YATAKAYO TUMIKA NI EURO 5, UNAWEZA KUGOOGLE EURO 5 NI BASI LA AINA GANI, ILA LINAWEZA KUWA LA BRAND YOYOTE, MFANO BENZI BUS EURO 5, AU VOLVO, SIKU HIZI KUNA MCHINA NAE ANATENGENEZA MABASI MAZURI EURO 5 MFANO YUTONG, FOTON, KING KONG ETC. ANGALIA VIDEO HIZI ZA MABASI YAENDAYO KASI , ANGALIA NJIA ZAO, NDIO UTAELEWA KWA NINI WANAITA MABASI YAENDAYO KASI
Kwanini yasiende kasi/au mradi usifanikiwe wakati barabara zake hazitatumiwa na magari mengine ya kawaida?Mimi nadhani huu mradi hautafanikiwa kabisa kwa sababu Dar haikupangwa vizuri tangu hapo mwanzo. Sawa mabasi yatakuwepo lakini tegemeeni hayatakwenda kasi tunavyofikiria. Ni mwendo wa pole , kwani msongamano uko palepale kama kawa.