Mradi wa mabasi ya mwendokasi bado kizungumkuti

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
Licha ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuagiza mradi wa mabasi yaendayo haraka uwe umeanza kazi tangu mwezi uliopita, hakuna dalili kama huduma hiyo ya usafiri itatolewa jijini hapa katika siku za karibuni.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo Desemba 19 mwaka jana aliposema mradi huo uwe umeanza kazi ifikapo Januari 11, lakini ilishindikana kutokana kukosekana mwafaka wa tozo ya nauli.

Chanzo: Mwananchi
 
Watu wanakaidi maagizo ya wakubwa zao..hilo la mabasi lililotolewa na Waziri Mkuu.....lile la Mh.Rais la kuacha mipasho bungeni...nk..nk.Hapa kazi tu.Nahisi iko namna.
 
Mradi umekufa kabla haujaanza...


Wabuni mradi mwingine maana wanajua kubuni tu kusimamia Utekelezaji hawawezi.
 
Hii nayo ni historia ya tanzania. Inabidi tuiandike watoto wetu wasome. Haiwezekeni kila siku tuaambiwa mpaka mwezi ujao. Mwezi ukifika tunaambiwa tena mpaka mwezi ujao. Na yakianza safari hayo mabasi wajue kuwa sisi tunataka nauri ya chini. Wakumbuke kuwa mafuta yanazidi kushuka bei. Habari ya 1200~1400 hatutaki kabisaa
 
Back
Top Bottom