Mradi wa kukusanya hela za Rushwa kwa CCM kwenye uchaguzi wa 2015 huu hapa, tayari waanza.

Ikwanja

JF-Expert Member
Jul 12, 2011
2,082
581
Ndugu wana JF, Jana serikali ya magamba kupitia jeshi la zimamoto wameanzisha mradi wa kukusanya mihela kwa ajili ya uchaguzi ujao, hapa naambatanisha ninachomaanisha ili wote kama bado hamjaona muone.

My Take.

Hivi kwenye suala la zima moto kipi cha muhimu, sticker au Fire extinguisher? maana naona sasa tutakuwa tunalipia sticker kulingana na ukubwa wa gari yaani CC. halafu wanasingizia kuwa kutakuwa kunafanyika inspection pale fire ndo wakupatie hiyo sticker, jamanii huo si wizi mchana kweupe kweli, Hivi ni huduma gani ambayo tunalazimika kulipia kwa gharama zote hizi kama sio kwa ajili ya hela ya kampeni? hivi huo ukaguzi watakuwa wanakagua nini? why all these forces wakati huu?

Nchi hii ni lini wizi na justification za uongo zitaacha? naomba wazalendo tulipigie kelele hili suala.

nawasilisha
 

Attachments

  • scan.pdf
    470.9 KB · Views: 1,012
Tunapigwa kote kote ndugu yangu mpaka akili itusogee. Wanajaribu kuchukua kila kinachowezekana na ninaamini itafikia siku tutakuwa hatuna chochote maana vyote tutakuwa tumewapa wao na hapo ndipo tutakuwa watumwa rasmi! Ukiwauliza watakwambia hicho nacho ni chanzo kipya cha mapato wakati kwenye madini wanachukua asilimia 3 tu! Ni aibu kubwa!
 
Hivi kikosi cha kuzima moto Tanzania huwa kipo? Zaidi ya kujua kuwa wako pale Jangwani / Kariakao katika mji wote wa Dar es salaam, sina uhakika na kazi yao. Badala ya kujenga vituo vingine vya Fire (Kama Ubungo, Tabata, Mbezi na Temeke) wamekuja na janja ya kula hela za bure. Njia nyingine za kumnyonya mnyonge.
 
Hivi hakuna jinsi tunaweza kuzuia huu ujinga? Tsh 40k for sticker is too much.
 
Ndugu wana JF, Jana serikali ya magamba kupitia jeshi la zimamoto wameanzisha mradi wa kukusanya mihela kwa ajili ya uchaguzi ujao, hapa naambatanisha ninachomaanisha ili wote kama bado hamjaona muone.

My Take.

Hivi kwenye suala la zima moto kipi cha muhimu, sticker au Fire extinguisher? maana naona sasa tutakuwa tunalipia sticker kulingana na ukubwa wa gari yaani CC. halafu wanasingizia kuwa kutakuwa kunafanyika inspection pale fire ndo wakupatie hiyo sticker, jamanii huo si wizi mchana kweupe kweli, Hivi ni huduma gani ambayo tunalazimika kulipia kwa gharama zote hizi kama sio kwa ajili ya hela ya kampeni? hivi huo ukaguzi watakuwa wanakagua nini? why all these forces wakati huu?

Nchi hii ni lini wizi na justification za uongo zitaacha? naomba wazalendo tulipigie kelele hili suala.

nawasilisha

kwanza ni kudownload: done

pili ngoja nisome uzi wako, na baada ya hapo nikasome nilichodownload, ili mods wakiushukia uzi, niwe tayari ninao mzigo.
 
kweli serikali dhaifu!!! hivi haiwezi kufikiria njia nyingine ya kukusanya mapato pasipo hii milolongo ya kodi?
 
Serikali ikiwa dhaifu na rais dhaifu basi kila kitu dhaifu
 
Piga chini 2015 wezi hawa pesa zote hizi wanaenda kujilipa mishahara minono na posho ,siasa ni mchezo mchafu huku madaktari na walimu hawana pesa za kuwalipa
 
Mnafikili hawa wagonjwa, pesa ya kwenda kubadilisha damu wataipata wapi? Tukubali tumeshaingia choo cha KJ (Kubwa Jinga), kilichobaki ni kuwa wapole mpaka 2015, au kama vp tuingie mtaani kama Arabs...
 
​na bado mpaka jamaa wa bagamoyo aondoke ikulu mengi tutayaona nchi haina kiongozi
 
Miaka ya nyuma nilikuwa na daladala yangu na Idara ya usalama barabarani wakapitisha agizo kuwa kila mwenye gari lazima aweke fire exitinguisher na dereva wangu kaniambia kuwa amepata moja kanyaboya hiyo inafaa. Ndugu zangu kila polisi traffic alipokagua alisema tuendelee na kazi kwa sababu shida viongozi wetu si ufanisi bali utekelezaji hata kama sio real. Wanakata pesa direct unapoenda kulipia Road licence nauliza ni nani anakagua hizo fire exitinguishers ili kuthibitisha kama zinafanya kazi??? Leave this country into the hands of wrong people is a big problem, they will charge money but they will not educate their people importance of the equipmets. Stay and you will see chamtema kuni yake.
 
Yaani ukalipie ndo ukaguliwe?????? Ndo fikra zao zimeishia hapo kweli walio andaa mkakati huu..........halafu usipokidhi????
Nilidhani unaelekezwa jinsi ya kupambana na moto,kifaa kinakaguliwa halafu ndo ukalipie.....kumbe ni kulipia halafu kukaguliwa; yaani money first....serikali kweli ndo maamuzi haya and we expect citizens to be obedient without force????

Is not this a serious joke???


Akili ndogo kuongoza akili kubwa..........If I may ask; Hivi kabla ya kufanya maamuzi na kutoa matangazo kama haya huwa wanakaa na ku picture the public reaction au ndo liwalo na liwe??????

I think aliyechoka si lazima aseme ila speed ya utendaji kazi pia inaweza kuwa good indicator!!!!!!!!!!!!

We are wise enough to see and judge come 2015....all the best to you all decision makers
 
Duh! Wangetuambia kwanza nchi hii ina zimamoto ngapi, ziko wapi, kwa nini hazifanyi kazi za uokozi.

Sio kutuchangisha kizembe zembe tu.
 
hilo ni eneo ambalo nao fire staff individually watafaidi baada ya trafic polici kuwa wanakuala pekeyao. mimi ninchoshangaa ukaguzi tuu 40k, hakuna msaaada mwingine. let us all say no to this wizi wa mchana.

hivi kwanza hii sheria ilipitia wapi, au ndo kama ya social security funds?
 
Back
Top Bottom