Mradi wa kufua umeme wa maji wa Julius Nyerere katika maporomoko ya mto rufiji unaotekelezwa na Serikali uliasisiwa na Baba wa Taifa mwaka 1975

elivina shambuni

JF-Expert Member
May 31, 2018
461
295
1566835938329.png

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Awamu ya Tano inatekeleza kwa vitendo Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere katika Maporomoko ya Mto Rufiji unaojulikana kama Julius Nyerere HydroPower Project ambao uliasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere mnamo mwaka 1975.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) mara baada kufanya ziara ya kikazi Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dar es Salaam na kujionea kitabu cha Tanzania News Review cha mwaka 1977 kinachoainisha kuwa, Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere ndiye Muasisi wa mradi huo.

Dkt. Mwanjelwa amesema, Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli imekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza masuala yenye maslahi kwa taifa yaliyoasisiwa na Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere.

“Hakika ule usemi wa zidumu fikra za Mwalimu Nyerere umetekelezwa kwa vitendo na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika ujenzi wa mradi huu,” amefafanua Dkt. Mwanjelwa.

Aidha, Dkt Mwanjelwa ameitaka Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa kuwa na utaratibu mzuri wa kuuhabarisha umma juu ya taarifa muhimu za kihistoria ambazo si za siri ili watanzania wajue maamuzi mbalimbali ya kizalendo yaliyofanywa na viongozi wao kwa mustakabali wa maendeleo ya Taifa.

Naye, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi amemhakikishia Dkt. Mwanjelwa kuwa Idara yake itaendelea kutunza vizuri na kwa uadilifu mkubwa nyaraka muhimu za nchi za kabla na baada ya uhuru kwani nyaraka hizo ni rejea muhimu katika utendaji kazi wa Serikali.

Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere katika Maporomoko ya Mto Rufiji unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2022 na utakuwa ukifua megawati 2,115 kwa siku.
 
Hii ni project inayoungwa mkono na watanzania wengi, hata wapinzani huwezi kusikia wakiikosoa sana, hua nawashangaa 'praise team' wanaposema wapinzani wanapinga kilakitu wakati kiuhalisia wapinzani wanapinga miradi isiyo na tija kama chato airport na ununuzi wa madege ya serikali.
 
Upo Tanzania kweli wewe au unaishi ughaibuni? Watu wamepinga hapa akina Zito et el leo unasema wapinzani wanaunga mkono
 
Kwahiyo teknolojia ya 1977 tunataka kuitumia kwenye karne ya 21 ba tunajisifu? Aliyeturoga kafa.
 
View attachment 1190608

Unapokuwa na Kiongozi Mkuu mwenye uelewa finyu lakini unaa mamlaka makubwa ya kiimla madhara yake ni makubwa sana.

Imefika wakati hata wasaidizi wake wasomi na degrees zao wamebaki kusifia tu sawa na wale ambao hawajasoma.
Katika miradi yote mradi utakaotutia umaskini vizazi na vizazi ni huo wa Stiglers Gorge. Bila kuzingatia sababu za WWF kuhusu kuvuruga ecosystems na World Heritage site kuna sababu 3 za nguvu kwa nini Stiglers Gorge ni wastage of money kwa nchi ya Tanzania; (1) Maji yapatayo 36% yaliyokuwapo mwaka 1980 wakati feasibility study ilifanyika sasa hivi hayapo (2) Umeme wa kutegemea maji siyo wa kuaminika kwenye karne hii kutokana na mabadiliko ya tabia nchi (3) Hata Mtera na Kihansi zilipojengwa miaka ya 1980s na 1990s tuliambiwa zingekuwa ni suluhisho la umeme lakini zimeahindwa. Lakini tunaambiwa bwawa linajaa matope hivyo hata kimo cha maji kinakuwa kidogo.
(4) Kuna ongezeko kubwa la watu wanaoishi pembezoni mwa mto unakoanzia na unakopita hivyo basi kuongezeka kwa shughuli za kibinadamu kama kilimo na mifugo.

Kweli Baba wa Taifa ndiye muasisi na mbunifu wa mradi wa Stiglers Gorge lakini hata kama angekuwa hai kufika leo angebadili mawazo ya utekelezaji kwa vile alikuwa ana shaurika.

Tutajenga Stigler Gorge kwa bei mara 3 ya hiyo wanayoitaja na hatuwezi kupata hizo Megawati 2100. Tutaendelea kulipa mkopo kutoka kwa nchi wahisani tulizokopa vizazi na vizazi.
 
Upo Tanzania kweli wewe au unaishi ughaibuni? Watu wamepinga hapa akina Zito et el leo unasema wapinzani wanaunga mkono

Ni dhahiri hawakupinga tu, bali waliweka na sababu kwa kuwa si vichaa, je walioipinga walisemaje?
 
Unapokuwa na Kiongozi Mkuu mwenye uelewa finyu lakini unaa mamlaka makubwa ya kiimla madhara yake ni makubwa sana.

Imefika wakati hata wasaidizi wake wasomi na degrees zao wamebaki kusifia tu sawa na wale ambao hawajasoma.
Katika miradi yote mradi utakaotutia umaskini vizazi na vizazi ni huo wa Stiglers Gorge. Bila kuzingatia sababu za WWF kuhusu kuvuruga ecosystems na World Heritage site kuna sababu 3 za nguvu kwa nini Stiglers Gorge ni wastage of money kwa nchi ya Tanzania; (1) Maji yapatayo 36% yaliyokuwapo mwaka 1980 wakati feasibility study ilifanyika sasa hivi hayapo (2) Umeme wa kutegemea maji siyo wa kuaminika kwenye karne hii kutokana na mabadiliko ya tabia nchi (3) Hata Mtera na Kihansi zilipojengwa miaka ya 1980s na 1990s tuliambiwa zingekuwa ni suluhisho la umeme lakini zimeahindwa. Lakini tunaambiwa bwawa linajaa matope hivyo hata kimo cha maji kinakuwa kidogo.
(4) Kuna ongezeko kubwa la watu wanaoishi pembezoni mwa mto unakoanzia na unakopita hivyo basi kuongezeka kwa shughuli za kibinadamu kama kilimo na mifugo.

Kweli Baba wa Taifa ndiye muasisi na mbunifu wa mradi wa Stiglers Gorge lakini hata kama angekuwa hai kufika leo angebadili mawazo ya utekelezaji kwa vile alikuwa ana shaurika.

Tutajenga Stigler Gorge kwa bei mara 3 ya hiyo wanayoitaja na hatuwezi kupata hizo Megawati 2100. Tutaendelea kulipa mkopo kutoka kwa nchi wahisani tulizokopa vizazi na vizazi.
Tatizo propaganda za awamu hii ni kubwa kuliko hata kipindi cha Nyerere mwenyewe.

Labda watueleze pia sababu zilizomfanya ajenge mabwawa mengi mdogo mdogo kwa gharama kubwa na kuacha hili moja ambalo lilikuwa na uwezo wa kututosheleza na ziada kwa miaka yote mpaka Leo. Au hiyo haipo kwenye Idara ya Taifa ya Kumbukumbu....!?
 
Hii ni project inayoungwa mkono na watanzania wengi, hata wapinzani huwezi kusikia wakiikosoa sana, hua nawashangaa 'praise team' wanaposema wapinzani wanapinga kilakitu wakati kiuhalisia wapinzani wanapinga miradi isiyo na tija kama chato airport na ununuzi wa madege ya serikali.
Bora umeongea mkuu
 
Back
Top Bottom