Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,500
- 46,028
Wenye uelewa na hili jambo la gesi yetu huko kusini kuuzwa kwa mabeberu au wachina wanieleshwe.
1.Kuuzwa huko kwa hiyo gesi kunamaanisha kwamba hiyo gesi si mali yetu tena na sisi tumebaki kama wateja tu?
2.Vitalu vyote vya kuzalisha gesi vimeuzwa tayari na hivyo hatuwezi kuwa na vitalu vyetu tofauti?
3.Hiyo gesi iliuzwa kwa kiasi gani cha fedha?
4.Iliuzwa kwa mabeberu gani? Wa Marekani, Ulaya au China?
5.Mradi wa mkubwa wa dola za kimarekani bilioni 30 wa gesi wa LNG ambao ulikwama kipind JPM na ambao unaonekana kupigiwa chapuo na Rais Suluhu sio sehemu ya gesi hiyo iliyouzwa?
Maswali haya yanatokana na kauli za wale wanaotaka mradi mpya wa umeme wa maji wa bwawa la Nyerere huko Selous ujengwe iwe mvua iwe jua pamoja na uwepo wa gesi nyingi huko kusini ambayo inaweza kuwa nishati mbadala ya kuzalisha umeme huku ikizalisha faida lukuki kuliko huo umeme wa maji.
Jambo lingine ni kwamba kama taifa tulikopa pesa nyingi kutoka nje kwa ajili bomba la gesi ambalo inasemekana matumizi yake hayajawahi kuvuka robo ya uwezo wake!
Kwa nini tuachane na uwekezaji huo wa msingi kabisa?