Mradi wa Fremu zinazojengwa Masai-Kawe kwenye uzio wa kambi ya Jeshi Lugalo ni wa nani?

JUAN MANUEL

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
3,620
2,000
Pale Kawe, kituo Cha Masai kabla hujafika ukwamani, uzio wa makazi ya JWTZ umevunjwa na zinajengwa fremu pale.

Swali langu: Ile ardhi ni mali ya umma, nani anajenga zile fremu? Je, ni jeshi lenyewe au kuna ofisa anatumia cheo chake kujenga fremu apige pesa kupitia mali ya umma?

Na hata kama zinajengwa na jeshi, haiwezekani jeshi kwa rasilimali zake zote lijiingize kwenye vimiradi vidogo kama hivi, kushindana na Raia wa kawaida.

Tunategemea jeshi lijenge viwanda, scheme kubwa za kilimo zinazotumia zana za kisasa, lianzishe miradi ya IT na artificial intelligence na sio biashara ya kupangisha fremu.

Hii kwa kweli haikubaliki, ni uchafuzi wa mazingira. Yale makazi yapewe hadhi yake, yabaki kama makazi ya wapiganaji na maofisa.

Haiwezekani mtu anajenga banda la kufuga kuku Masaki, Oysterbay, Upanga.
 
TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Feb 26, 2018
2,462
2,000
Wee umeona nani anaweza kufanya mradi wa AI kwenye ili jeshi???wacha tu wajenge frem wapangishe ndio walipofikia uwezo wao hapo.Hayo mambo ya AI mwachie US ,China na Russia bro sisi miradi yetu ni ile ile kupangisha frem,kufuga kuku basi.
 
Kimolah

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
436
500
Anayejenga kaangalie bango kama lipo ..lakini pia tambua ya kwamba eneo unalolisema limepakana na barabara ya umma ijulikanayo old bagamoyo road ambayo kwa bahati mbaya ( mifumo ya kimpango mji ) imekatisha katika eneo la jeshi . Ardhi unayoisema ni mali ya umma ujue kuwa ni kwa matumizi maalum hivyo umma hatuwezi kuitumia tu tunavyotaka ndio maana kuna 'time curfew ' , eneo lile la kamsitu pori pale pembeni ya kanisa la wasabato ,paliwahi ombewa pawe kituo cha daladala ,lile eneo lote mpaka chini mto mbezi ni mali ya jeshi la wananchi kambi ya lugalo, nadhani walikuwa katika majadiliano ili ku-declasify lile eneo ili liweze kutumika na umma kwa minajili ya kuwekwa hicho kituo (ambacho kwa sasa kama ni mwenyeji maeneo hayo kimesogezwa kule viwanja vya tanganyika packers) ,
nafikiri wamefanya hivyo sababu hayo maghorofa humo ndani wanaishi binadamu tu kama wengine na wana mahitaji ya kawaida kabisa, hivyo kinachofanyika hapo ni kurahisisha tu uwepo wa huduma za chap.
Suala la kujenga viwanda na scheme kubwa za kilimo kama unakumbana na taarifa ni vitu vinavyofanyika lakini huwezi sikia saana kwenye "shosho" media , pita pale mwenge JKT utaona kuna matrekta makubwa ya 115HP na attachments zake yalikuwa sabasaba maonyesho ..ni sehemu ya kuwezeshwa vikosi kuzalisha mali. Suala la uboreshwaji wa makazi ya maafisa na familia zao lilianza tangu kipindi cha anko JK (maana nae pia alishapita taasisi) ndio maana zile "kota" nyingi zilivunjwa na hayo maghorofa kujengwa pia familia zenye miradi ya kilimo na ufugaji mdogo ndani ya makambi zilitengwa sehemu maalum kwa ajili hiyo. Nadhani fikra ya banda la kuku masaki oysterbay limechukuliwa kwa mtizamo hasi ila fahamu kuwa kama banda tajwa ni la kisasa na viwango popote pale litajengwa, mfano kama hukuwa unajua, magogoni kuna mabanda achana na ya kuku, ya ndege aina mbalimbali na wanyama. Mimi binafsi sidhani jeshi linashindana na raia wa kawaida kwa kufanya ujenzi wa frame hapo kwenye uzio. Possibly wameona kuna uwezekano wa kuboresha na kitu kikafanyika na yawezekana ni sehemu ya miradi ya ngome saccos.
 
ras jeff kapita

JF-Expert Member
Jan 4, 2015
12,121
2,000
Pale Kawe, kituo Cha Masai kabla hujafika ukwamani, uzio wa makazi ya JWTZ umevunjwa na zinajengwa fremu pale.

Swali langu: Ile ardhi ni mali ya umma, nani anajenga zile fremu? Je, ni jeshi lenyewe au kuna ofisa anatumia cheo chake kujenga fremu apige pesa kupitia mali ya umma?

Na hata kama zinajengwa na jeshi, haiwezekani jeshi kwa rasilimali zake zote lijiingize kwenye vimiradi vidogo kama hivi, kushindana na Raia wa kawaida.

Tunategemea jeshi lijenge viwanda, scheme kubwa za kilimo zinazotumia zana za kisasa, lianzishe miradi ya IT na artificial intelligence na sio biashara ya kupangisha fremu.

Hii kwa kweli haikubaliki, ni uchafuzi wa mazingira. Yale makazi yapewe hadhi yake, yabaki kama makazi ya wapiganaji na maofisa.

Haiwezekani mtu anajenga banda la kufuga kuku Masaki, Oysterbay, Upanga.
Nakubaliana na ww Jeshi linatakiwa kuwa na Miradi mikubwa sana
 
Mightier

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
5,571
2,000
Pale Kawe, kituo Cha Masai kabla hujafika ukwamani, uzio wa makazi ya JWTZ umevunjwa na zinajengwa fremu pale.

Swali langu: Ile ardhi ni mali ya umma, nani anajenga zile fremu? Je, ni jeshi lenyewe au kuna ofisa anatumia cheo chake kujenga fremu apige pesa kupitia mali ya umma?

Na hata kama zinajengwa na jeshi, haiwezekani jeshi kwa rasilimali zake zote lijiingize kwenye vimiradi vidogo kama hivi, kushindana na Raia wa kawaida.

Tunategemea jeshi lijenge viwanda, scheme kubwa za kilimo zinazotumia zana za kisasa, lianzishe miradi ya IT na artificial intelligence na sio biashara ya kupangisha fremu.

Hii kwa kweli haikubaliki, ni uchafuzi wa mazingira. Yale makazi yapewe hadhi yake, yabaki kama makazi ya wapiganaji na maofisa.

Haiwezekani mtu anajenga banda la kufuga kuku Masaki, Oysterbay, Upanga.
Hata Mimi Ujenzi huo tena ambao unaenda Kasi mno si tu Umenisikitisha bali Umenishangaza pia.

Hata hivyo nimejiongeza kidogo Kimawazo kwamba Ujenzi huo licha tu ya Kupendezesha hilo eneo lakini pia Kiusalama utakuwa na Faida hasa kutokana na Historia mbaya ya Watu Kukabwa, Kujeruhiwa na Kuibiwa eneo hilo hasa kati ya Masai na Dawasco.

Ila naamini JWTZ chini ya CDF General Mabeyo na Wasaidizi wake wa Vikosi hasa hicho hawajakurupuka kuja na Umaamuzi wa Kiujasiriamali katika Kikosi chao.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom