Mradi wa DARTS (MABASI YAENDAYO KASI) umewatenga walemavu

Mkurabitambo

JF-Expert Member
Feb 3, 2010
230
57
Habari wanajamvi;poleni na majukumu. Naandika ujumbe huu kwa masikitiko maana ndugu zetu walemavu wametegwa na mradi huu mpya. Ukiangalia mradi huu kuanzia Posta hadi Kimara hakuna hata mahali panapo mruhusu mlemavu kuvuka. Chukulia mfano mlemavu anakaa kati ya vituo viwili vya mabasi sema Ubungo hadi shekilango;hawezi kukatika hapo katikati hadi aende hadi kwenye kituo husika kwani barabara zote zimezibwa kushoto na kulia,sasa mlemavu mwenye baiskeli atawezaje kukatiza hapo au ndio hadi atembee kilo1 kwa ajili ya kutaka kuvuka barabara?

Nadhani kwa uelewa wangu mdogo wa miundombinu;kulipaswa kuwa na eneo maalumu kwa ajili ya vivuko vya watu na hasa walemavu vinginevyo mradi mzima utakuwa unamapungufu.
 
mkuu hebu tusubirie mradi ukamilike labda unaweza kupata majibu ya maswali yako mazuri,..
 
Back
Top Bottom