Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,319
- 72,747
Waziri mkuu Majaliwa wiki kadhaa zilizopita alipotembelea mradi wa mabasi yaendayo kasi Dsm alitoa tamko kali sana tena kwa mbwembwe kuwa Mradi huo utaanza tar 10/januari.
Pamoja na hayo tumeshuhudia CEO wa mradi huo akiondolewa kwa fedheha kama ilivyo serikali ya sasa kuwaondoa watu kwa sifa bila kuchunguza jambo kulingana na kanuni chini ya falsafa ya hapakazitu.
Jambo la ajabu ni kuwa tamko hilo la PM ni kama limetupwa pembeni maana hata dalili za kuanza halipo na hata mgogoro wa nauli haujapata ufumbuzi.
Jee hii ni ishara gani kwa PM kufuatana na kundi la waandishi na kutoa matamko mazito lakini hayatekelezwi na kila kitu ni business as usual? Hivi sio kuwa tunarudi kulekule?