Mradi wa Bwawa la Nyerere tulijilisha upepo au ndiyo mwendelezo wa siasa chafu za kibepari?

Mqkamba kawekwa hapo Kama mtego huonmradi ukifeli ndio utampoteza makmba kwemy siasa

Mam mjanja kamuweka ili amalize kisiasa huyu makamba
Nape na Ridhiwani nao wapo kwa mtego? Huoni kuna pattern hapo?
 
Ndugu yangu MALCOM LUMUMBA

....Long time no see!!

Kwa heshima ya ndugu Jinga la Zamani alienialika, wacha nami niseme machache.

Hapa wacha niende moja kwa moja kwenye JNHPP ili nisiifanye post yangu kuwa ndefu maradufu..

Kwa hapa tulipofikia, hatuwezi kuendelea na yale mambo ya ku-abandon miradi mikubwa wakati tayari imeshameza mabilion ya pesa! Kwa maana nyingine, JNHPP Must Continue kwa sababu tayari pesa nyingi imeshaingia!!

Hata hivyo, wakati mradi huu unaanza binafsi niliupinga! Sikuupinga kwa sababu za kimazingira wala kwamba ni unsustainable lakini mimi ni muumini mkubwa wa Economic Multiplier Effect na Optimal Resources Allocation.

Dhana hii ya Multplier Effect nishaieleza sana huko nyuma! Na kwavile I believe in Multiplier Effect, kama ningewekewa option ya either JNHPP or LNG Project (Gas Industry) kama source ya uzalishaji umeme, I'll ALWAYS be in favor of the Gas Industry kwa sababu huko kuna HIGHER multplier effect kulinganisha na umeme wa maji!!

There's no match between the two!

Bidhaa Kuu kutoka JNHPP ni UMEME PEKEE, and there's little (if any) to no by-products zinazoweza kuzalishwa kupitia JNHPP! Kinyume chake, Bidhaa Kuu ya LNG Project ni Gas na sio umeme lakini hapo hapo unaweza pia kupata UMEME + TAKATAKA ZINGINE!

Kumbe basi, 99% ya Multiplier Effect inayoweza kupatikana kupitia JNHPP pia inaweza kupatikana kutoka LNG Project. Kinyume chake, mengi unayoweza kupata kupitia LNG Project HUWEZI KUYAPATA kupitia JNHPP!

JNHPP itatupatia tu UMEME utakosaidia ku-boost sekta zingine za kiuchumi na labda kufanya Electricity Export but only regionally. Multiplier Effect tunayotarajia hapa inaweza kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji kwa sababu tutakuwa na umeme wa uhakika.

Hata hivyo, YOTE hayo pia unaweza kuyapata kupitia LNG Project...

Wakati hali ni hiyo kwa KNHPP, LNG Project inaweza kukupatia AT LEAST yafuatayo:-

1. Umeme... Wakati Umeme sio Main Product from LNG Project, pale JNHPP umeme ndiyo MAIN PRODUCT itakayotokana na investment husika!

Kwa maana nyingine, faida yoyote ya kiuchumi INAYOWEZA kupatikana kwenye JNHPP Project ambayo umeme wake ndio Main Product, pia INAWEZA kupatikana, tena kwa ukubwa wa maradufu kutoka LNG Project kupitia umeme unaoweza kuzalishwa ingawaje sio Main Product!

Na kama tunasema LNG Project izalishe UMEME TU basi umeme huo unaweza kutumika kote Sub-Saharan Africa tena kwa miongo kadhaa wakati JNHPP Project haina uwezo hata ku-sustain hata uchumi kama wa South Africa!

In fact, hata Kenya ukiwaambia waachane na vyanzo VYOTE vya umeme walionao na watumie umeme kutoka JNHPP tena peke yao, bado umeme huo HUWEZI kuwatosha!!

Hapa ili nieleweke labda niseme hivi: Kwa sasa Umeme wa Gas uliopo kwenye Gridi ya Taifa ni almost 57% ya umeme WOTE huku hydropower ikichangia roughly 37%! Hata hivyo, 57% hiyo inatokana na less than 7.5 Trillion Cubic Feet of Gas ambazo ndizo zimeanza kuchimbwa kutoka Songongo, Mkoani Lindi na Madimba, mkoani Mtwara! U

Ukitoa hizo 7.5 Trillion Cubic Feet of gas ambazo zimeanza kuchimbwa, kuna almost 50 Trillion Cubic Feet of gas ambazo HAZIJAGUSWA! And remember, hiyo 57% ya umeme unaozalishwa sio unatokana na full capacity ya hizo 7.5 Trillion Cubic Feet za gas... hell no!

NInachotaka kusema ni kwamba, at full capacity, hizo 7.5 Trillion Cubic Feet zinaweza kuzalisha maradufu ya umeme utakaozalishwa na JNHPP na hapo bado zile 50 Trillion Cubic Feet HUJAZIGUSA!

2. Gas.. Hii ndiyo MAIN PRODUCT from the LNG Project. Hapo juu tumeshaona Umeme unavyoweza kuwa another product from the LNG Project, BUT...

(a) Gas For Export: LNG ni biashara kubwa sana duniani, na kwahiyo ni EXPORTABLE Product world-wide na sio tu regionally kama tunavyoweza kusafirisha the ONLY JNHPP Product!

Watu wanaposikia Lindi inataka kujengwa LNG Plant, akili yao wanadhani ni substitutes ya JNHPP! Kwamba, lengo ni tufanye gas processing kisha gas itumike kuzalisha umeme!

Kutokana na imani hiyo ndo maana unakuta Wafuasi wengi wa JPM wanapinga sana ule mradi kwa kile wanachodhani una lengo la kufuta JPM Legacy kwenye Bwawa la Nyerere!!!

Hapa ieleweke tu kwamba HAKUNA MJINGA ANAYEWEZA KUWEKEZA USD 30 BILLION for kwa ajili ya kuzalisha umeme kwa nchi maskini kama Tanzania! Hizo almost TRILLIONS 70 zinarudi rudi vipi ikiwa main product ni umeme?!

Hiyo investment inafanyika kwa sababu almost 50 Trillion Cubic Feet of UNDEVELOPED GAS ni Huge Opportunity for Export na sio eti kuzalisha umeme ili hatimae kuua Legacy ya JPM kwenye Bwawa la Nyerere!

(b) Gas For Domestic and Industrial Use:- Asikuambie mtu... this's a huge business opportunity!

Tuchukue mfano mdogo tu wa hii tenda ambayo ilitangazwa na TPDC...

TPDC-  Gas Infrastructure.jpg


Kabla hata hatujaingia huko kwenye gesi yenyewe, hebu tutafakari hiyo project! Yaani tunahitaji kiwanda kitakachoweza kuzalisha vifaa vifuatavyo:- HDPE pipes, HDPE fittings, Domestic Gas Meters and associated fittings, Commercial Gas Meters and associated fittings, and PRMS.

Na kwavile hiyo inaangukia kwenye Local Content, hiyo kazi inatakiwa kufanywa na Watanzania as per Sheria ya Mafuta na Gesi ya 2015!

Now tujiulize!!

Kama tunaamua gas infrastructure zifike hadi wilayani, hapo atakayepata tenda atalazimika kuzalisha hivyo vifaa kwa wingi gani, na angetoa ajira za moja kwa moja ngapi, indirect employment ngapi, na Wauza Mama Lishe wangeuza sahani ngapi za ubwabwa, ugali, chapati and everything else?

That's what we call: ECONOMIC MULTPLIER EFFECT! Gesi ipo LIndi na Mtwara lakini effect yake inasababisha kujengwa kwa kiwanda cha kutengeneza vifaa vya kujengea miundo mbinu ya usambazaji gesi! Hapo zitazalishwa aina ya ajira kama nilivyotaja hapo juu!

LNG Project inayopelekea kujengwa kiwanda tajwa hapo juu, effect yake itamkuta hadi muuza Mama Lishe, Muuza Genge, Mangi na Mpemba na maharage unga na mchele wao dukani, mkulima aliyezalisha hizo bidhaa, n.k kwa sababu pesa itakayotokana na hizo shughuli itakuwa inaenda moja kwa moja kwa wananchi na pesa hizo kuambukiza sekta zingine za kiuchumi na kijamii!

Hapo umeshazalisha tu vifaa tajwa... what next?

Hivyo vifaa vikishazalishwa ina maana itabidi iwepo kampuni nyingine/zingine za kutandaza hizo infrastructure Tanzania mzima! Kampuni hiyo nayo itatoa ajira za moja kwa moja, kwa vibarua na wauza Mama Lishe ambao pia wataambukiza sekta zingine kama nilivyotaja hapo juu!

Aidha, projects zote mbili... za kuzalisha vifaa na kusambaza miundombinu pia zitazalisha PAYE na Kodi zingine kwenda serikalini, na hatimae kuleta direct effect kwenye public services zitolewazo na serikali!

THAT'S WHAT WE CALL MULTIPLIER EFFECT in the national economy ambayo inapatikana hata kabla gesi yenyewe HUJAIGUSA!

Gesi imeshazalishwa, and ready for different uses! Je, miundo mbinu itaweza kufika kila mahali? HELL NO! This HELL NO is another business opportunity kwa sababu hatimae kutakuwa na new opportunity to Gas Vendors! Wenye uwezo watajenga Gas Fuelling Stations!

That's what we call Multiplier Effect!!

3. Gas By-Products:-

Nimeshajaza server tayari kwahiyo hapa niongee kidogo tu ingawaje kuna mengi zaidi ya kuongea!

Mali Ghafi zinazotokana na uchakataji wa gesi zinaweza kutumika kutengeneza bidhaa mbalimbali! Hapa tusiende mbali! Tayari kuna project ya USD 1.9 Billion kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanda cha Mbolea ambacho kinatarajia kutumia Gas By-Products!

Tanzania hii HAKUNA Kiwanda chenye thamani hata nusu ya hicho kiwanda!! Now tujuulize: Kiwanda kama hicho kinaweza kuzalisha direct and indirect employment to the company ngapi, Mama Lishe wangeuza kiasi gani kwa vibarua na wafanyakazi, PAYE and other taxes zingelipwa kiasi gani...

THAT'S WHAT WE CALL MULTIPLIER EFFECT!

Sio viwanda vya mbolea peke yake vinavyoweza kutumia Gas By-Products! Kuna at least 4 MORE products, including Plastic Products zinazoweza kuzalishwa kupitia Natural Gas By-Products!!!

FAIDA zote hizo nilizotaja hapo juu, HUWEZI KUZIPATA kupitia JNHPP!!

Sasa akina sisi tulikuwa tunapinga JNHPP kwa sababu tunaamini LNG Project inaweza ku-offer almost everything that can be offered by JNHPP but MANY MORE at much HIGHER VALUE than what JNHPP can offer!!!

Kwenye uchumi tunazungumzia dhana ya optimal allocation of resources!! Tunaambiwa resources, kwa muktadha huu pesa, ni SCARCE! Hivyo basi, kidogo utakachopata unatakiwa ku-allocate kule utakopata MAXIMUM RETURNS, and not just RETURNS!

LNG Project inaweza Kujenga JNHPP with our own money in less than 5 years lakini JNHPP KAMWE haiwezi kuwa na uwezo wa ku-fully finance LNG Project!! Kumbe basi, kama tunaamini Hydropower ni CHEAP source of electricity, bado tungeweza kujenga mradi huo kwa pesa zetu sisi wenyewe miaka michache tu baada ya kuanza kuzalisha gesi!

ALL IN ALL, should we expect CHEAP ELECTRICITY from JNHPP?!

Kwa maoni yangu, sioni hiyo cheap electricity inapatikana patikana vipi!!

Kwahiyo ndugu yangu Malcom, ule mpango wako wa kusambaza mashine za kusaga Tanzania mzima kwa sababu kuna umeme wa bei rahisi unakuja, man, ningekushauri pitia vizuri plans zako kwa sababu I strongly believe umeme wa bei rahisi HAUTAKUWEPO!!

WHY?

1. Mradi utatumia takribabi Sh 7 TRILLION. Hapo zijaweka riba za mabenki kwa sababu funding sources zingine zinatoka kwenye private banks!

Sasa kama tunadhani umeme utakuwa wa bei rahisi, who will pay hizo TZS 7 Trillions + Interests?! LAZIMA Watumiaji tulipe hizo gharama!!!

2. Watanzania tunadhani umeme utakaozalishwa pale ni MWINGI kweli kweli!!

Guys, kinachozalishwa pale sio kwamba Umeme Mwingi bali Umeme unazalishwa kwa ajili ya jamiii yenye Umaskini Mwingi!!

Kama nilivyosema hapo awali, Kenya ni nchi maskini tu! Lakini leo tuseme Kenya iachane na vyanzo vyote vya umeme inavyotumia hivi sasa na badala yake waanze kutumia umeme MWINGI utakazozalishwa pale JNHPP, katu Umeme huo HAUTAWATOSHA!!

Hata Tanzania kwenyewe, na umaskini wetu huu halafu tuseme tufunge vyanzo vyote vya umeme tulionao na tuanze kutumia tu Umeme MWINGI kutoka JNHPP... it'll take us less than 5 years kabla hatujaanza kuwa na uhaba wa kutisha wa umeme kwa sababu pale hakuna umeme mwingi bali tuna umaskini mwingi unaofanya less than 3000MW zionekane ni umeme mwingi!

Ninachojaribu kusema ni nini: Endapo uchumi wetu unaongeza kwa angalau 10% TU, umeme kutoka JNHPP + Available Sources HAUTAWEZA kuhimili uchumi huo ambao kimsingi na wenyewe utakuwa ni uchumi wa kimaskini tu!!!

Kwa maana nyingine, hata kabla hatujamaliza deni la TZS 7 Trillion za JNHPP basi kuna uwezekano mkubwa sana demand ya umeme nchini inaweza kuongezeka hapo mbeleni na kumeza umeme wote tulionao hivi sasa + Umeme wa JNHPP!

Demand ikiwa kubwa, watakachofanya TANESCO ni ku-DISCOURAGE Matumizi Makubwa ya Umeme! Una-discourage Matumizi Makubwa ya Umeme sio kwa kutoa elimu bubu watoazo kwenye ma-tv bali watafanya hivyo kwa kupandisha bei ya umeme ili hatimae muache matumizi holela ya umeme, kama mlivyoacha kutumia majiko ya umeme bila hata kutandikwa bakora!!

Na hapa tukumbushane kwamba, kama kweli tunaamini bei itakuwa ndogo basi ni hiyo bei ndogo ndiyo itakuwa chanzo cha kukaribisha bei kubwa! Umeme ukiwa nafuu, matumizi ya umeme yataongezeka! Watu watatupa majiko yao na pasi zao za mkaa kwa sababu umeme ni cheap!

Wafanyabiashara wataachana na mashine za kusaga zinazotumia mafuta na kuhamia mashine zinazotumia umeme kwa sababu umeme ni cheap!

Matumizi ya vifaa vya umeme yataongezeka kwa sababu umeme ni cheap!!! Huku Uswahilini ule ugomvi wa wapangaji kwamba tuwe tunazima mafriji na mafriza yetu, ugomvi huo utapungua kama sio kwisha kabisa kwa sababu umeme ni cheap, na watu watakuwa wanajiachia!!

OUTCOME?

Increased power consumption!! Njia ya kupambana na hilo? Nishasema hapo juu: discourage power consumption by increasing the price!!

IT'S SIMLE ECONOMY!

Is JNHPP White Elephant Project?

Yakitokea niliyosema hapo juu, HAIWEZI KUWA White Elephant Project lakini yasipotokea inaweza isiwe White Elephant Project lakini inaweza kuwa a STRUGGLING PROJECT!!

Tunahitaji uchumi mkubwa zaidi ili tuweze ku-consume hizo additional MW zitakazozalishwa! But don't forget, huo uchumi ukitokea itamaanisha NO MORE CHEAP ELECTRICITY kwa sababu power consumption itakuwa kubwa!!

Na isipotokea, ina maana Project Haitaweza kuzalisha pesa ya kutosha kulioa madeni yake, and hence becoming a STRUGGLING PROJECT!!

Yaani ndo ile inaitwa Ukichimama Nchale, Ukikimbia Nchale!! Sasa chagua mwenyee udungwe nchale wakati umesima au wakati unakimbia... MAUMIVU YAPO PALE PALE!!

Ndo vile tu umeme utaingizwa Grid ya Taifa lakini kama ingekuwa unakuwa distributed kipeke yake peke yake, watu wangeukimbia huo kama wanavyolikimbia Daraja la Kigamboni!!!
 
Ndugu yangu MALCOM LUMUMBA

....Long time no see!!

Kwa heshima ya ndugu Jinga la Zamani alienialika, wacha nami niseme machache.

Hapa wacha niende moja kwa moja ili nisiifanye post yangu kuwa ndefu maradufu..

Kwa hapa tulipofikia, hatuwezi kuendelea na yale mambo ya ku-abandon miradi mikubwa wakati tayari imeshameza mabilion ya pesa!

Hata hivyo, wakati mradi huu unaanza nilikuwa naupinga! Hapo kabla nilikuwa naupinga sio kwa sababu za kimazingira wala kwamba ni unsustainable lakini mimi ni muumini mkubwa wa Economic Multiplier Effect!

Dhana hii ya Multplier Effect nishaieleza sana huko nyuma! Na kwavile I believe in Multiplier Effect, kama ningewekewa option ya either JNHPP or Gas Industry kama source ya uzalishaji umeme, I'll ALWAYS be in favor of the Gas Industry kwa sababu huko kuna HIGHER multplier effect kulinganisha na umeme wa maji!!

Unachoweza kutoa kwenye umeme wa maji ni UMEME PEKEE wakati Sekta ya Gesi inatoa UMEME + TAKATAKA ZINGINE! Kwa maana nyingine, 99% ya Multiplier Effect inayoweza kupatikana kwenye umeme wa maji pia inaweza kupatikana kutoka kwenye gas industry. Kinyume chake, mengi unayoweza kupata kwenye Gas Industry HUWEZI KUPATA kwenye umeme wa maji!

Wakati Umeme wa Maji utakupatia tu Umeme utaosaidia uzalishaji kwenye sekta zingine, na labda kufanya electricity export but only regionally huku ukitegemea multiplier effect itakayotokana na uwezekano wa kuongezeka uzalishaji kutokana na kuwa na umeme wa uhakika, hayo YOTE pia unaweza kuyapata kwenye Gas Industry...

Kinyume chake, Gas Industry inaweza kukupatia:-

1. Umeme... Wakati Umeme sio Main Product from the Gas Industry, kwenye hydropower project umeme ndiyo MAIN PRODUCT itakayotokana na investment husika! Kwa maana nyingine, faida yoyote ya kiuchumi INAYOWEZA kupatikana kwenye JNHPP Project ambayo umeme wake ndio Main Product, pia INAWEZA kupatikana kwenye Gas Industry kupitia umeme unaoweza kuzalishwa ingawaje sio Main Product!

2. Gas.. Hii ndiyo MAIN PRODUCT from the Gas Industry. Hapo juu tumeshaona Umeme unavyoweza kuwa another product from the Gas Industry but...

(a) Gas For Export: LNG ni biashara kubwa sana duniani, na kwahiyo ni EXPORTABLE Product world-wide! Watu wanaposikia Lindi inataka kujengwa LNG Plant, akili yao wanadhani ni substitutes ya JNHPP! Kwamba, lengo ni tufanye gas processing kisha gas itumike kuzalisha umeme!

Kutokana na imani hiyo ndo maana unakuta Wafuasi wengi wa JPM wanapinga sana ule mradi kwa kile wanachodhani kwamba una lengo la kufuta JPM Legacy kwenye Bwawa la Nyerere!!!

Guys... HAKUNA MJINGA ANAYEWEZA KUWEKEZA USD 30 BILLION for Power Project kwa nchi maskini kama Tanzania! Hizo Trillion karibu 70 zinarudi rudi vipi ikiwa your main product ni umeme?!

Hiyo investment inafanyika kwa sababu almost 50 Trillion Cubic Feet of UNDEVELOPED GAS ni Huge Opportunity for Export na sio eti kuzalisha umeme ili hatimae kuua Legacy ya JPM kwenye Bwawa la Nyerere!


(b) Gas For Domestic and Industrial Use:- Asikuambie mtu... this's a huge business opportunity!

Tuchukue mfano mdogo tu wa hii tenda ambayo ilitangazwa na TPDC...

View attachment 2113381

Kabla hata hatujaingia huko kwenye gesi yenyewe, hebu tutafakari hiyo project! Yaani tunahitaji kiwanda kitakachoweza kuzalisha vitu vifuatavyo:- HDPE pipes, HDPE fittings, Domestic Gas Meters and associated fittings, Commercial Gas Meters and associated fittings, and PRMS.

Na kwavile hiyo inaangukia kwenye Local Content, hiyo kazi inatakiwa kufanywa na Watanzania as per Sheria ya Mafuta na Gesi ya 2015!

Now tujiulize!! Kama tunaamua gas infrastructure zifike hadi wilayani, hapo atakayepata tenda atalazimika kuzalisha hivyo vifaa kwa wingi gani, na angetoa ajira za moja kwa moja ngapi, indirect employment ngapi, na Wauza Mama Lishe wangeuza sahani ngapi za ubwabwa, ugali, chapati and everything else?

That's what we call: ECONOMIC MULTPLIER EFFECT! Gesi ipo LIndi au Mtwara lakini effect yake inasababisha kujengwa kwa kiwanda cha kutengeneza vifaa vya kujengea miundo mbinu ya usambazaji gesi! Hapo zitazalishwa aina ya ajira kama nilivyotaja hapo juu!

Effect ya kiwanda hiki itamkuta hadi muuza Mama Lishe, Muuza Nyanya, Mangi na Mpemba na maharage yao dukani, n.k kwa sababu pesa itakayotokana na hizo shughuli itakuwa inaenda moja kwa moja kwa wananchi na pesa hizo kuambukiza sekta zingine za kiuchumi na kijamii!

Hapo umeshazalisha vifaa tajwa... what next?

Hivyo vifaa vikishazalishwa ina maana itabidi iwepo kampuni nyingine/zingine za kutandaza hizo infrastructure Tanzania mzima! Kampuni hiyo nayo itatoa ajira za moja kwa moja, kwa vibarua na wauza Mama Lishe ambao pia wataambukiza sekta zingine kama nilivyotaja hapo juu!

Aidha, projects zote mbili... za kuzalisha vifaa na kusambaza miundombini pia zitazalisha PAYE na Kodi zingine kwenda serikalini, na hatimae kuleta direct effect kwenye public services!

THAT'S WHAT WE CALL MULTIPLIER EFFECT in the national economy ambayo inapatikana hata kabla gesi yenyewe HUJAIGUSA!

Gesi imeshazalishwa, and ready for different uses! Je, miundo mbinu itaweza kufika kila mahali? HELL NO! This HELL NO is another business opportunity kwa sababu hatimae kutakuwa na new opportunity to Gas Vendors! Wenye uwezo watajenga Gas Fuelling Stations!

That's what we call Multiplier Effect!!

3. Gas By-Products:-

Nimeshajaza server tayari kwahiyo hapa niongee kidogo tu! Mali Ghafi zinazotokana na uchakataji wa gesi zinaweza kutumika kutengeneza bidhaa mbalimbali! Hapa tusiende mbali! Tayari kuna project ya USD 1.9 Billion kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanda cha Mbolea ambacho kinatarajia kutumia Gas By-Products!

Tanzania hii HAKUNA Kiwanda chenye thamani hata nusu ya hicho kiwanda!! Now tujuulize: Kiwanda kama hicho kinaweza kuzalisha direct and indirect employment to the company ngapi, Mama Lishe wangeuza kiasi gani kwa vibarua na wafanyakazi, PAYE and other taxes zingelipwa kiasi gani...

THAT'S WHAT WE CALL MULTIPLIER EFFECT!

Sio viwanda vya mbolea peke yake vinavyoweza kutumia Gas By-Products! Kuna at least 4 MORE products, including Plastic Products zinazoweza kuzalishwa kupitia Natural Gas By-Products!!!

FAIDA zote hizo nilizotaja hapo juu, HUWEZI KUZIPATA kwenye Hydropower Projects!!!

Sasa akina sisi tulikuwa tunapinga JNHPP kwa sababu tunaamini Gas Industry inaweza ku-offer more and more than JNHPP can!!!

Kwenye uchumi tunazungumzia dhana ya optimal allocation of resources!! Tunaambiwa resources, kwa muktadha huu pesa, ni SCARCE! Hivyo basi, kidogo utakachopata unatakiwa ku-allocate kule utakopata MAXIMUM RETURNS, and not just RETURNS!

LNG Project inaweza Kujenga JNHPP with our own money in less than 5 years lakini JNHPP KAMWE haiwezi kuwa na uwezo wa ku-fully finance LNG Project!! Kumbe basi, kama tunaamini Hydropower ni CHEAP source of electricity, bado tungeweza kujenga mradi huo kwa pesa zetu sisi wenyewe miaka michache tu baada ya kuanza kuzalisha gesi!

ALL IN ALL, should we expect CHEAP ELECTRICITY from JNHPP?!

Kama mnaamini kutakuwa na umeme wa bei rahisi kutoka JNHPP, basi tutakuwa TUNAJIDANFANYA SANA!! Kwahiyo ndugu yangu Malcom, ule mpango wako wa kusambaza mashine za kusaga Tanzania mzima kwa sababu kuna umeme wa bei rahisi unakuja, man, achana na huo mpango kwa sababu umeme wa bei rahisi HAUTAKUWEPO!!

WHY?

1. Mradi utatumia takribabi Sh 7 TRILLION. Hapo zijaweka riba za mabenki kwa sababu funding sources zingine zinatoka kwenye private banks!

Sasa kama tunadhani umeme utakuwa wa bei rahisi, who will pay hizo TZS 7 Trillions + Interests?! LAZIMA Watumiaji tulipe hizo gharama!!!

2. Watanzania tunadhani umeme utakaozalishwa pale ni MWINGI kweli kweli!!

Guys, kinachozalishwa pale sio kwamba Umeme Mwingi bali Umeme unaozalishwa kwenye jamiii yenye Umaskini Mwingi!! Kenya ni nchi maskini tu! Lakini leo tuseme Kenya iachane na vyanzo vyote vya umeme inavyotumia sasa na badala waanze kutumia umeme MWINGI utakazozalishwa pale JNHPP, katu Umeme huo Huwezi Kuwatosha!!

Hata Tanzania kwenyewe, na umaskini wetu huu halafu tuseme tufunge vyanzo vyote vya umeme tulionao na tuanze kutumia tu Umeme MWINGI kutoka JNHPP... it'll take us less than 3 years kabla hatujaanza kuwa na uhaba wa kutisha wa umeme!!

Ninachojaribu kusema ni nini: Endapo uchumi wetu unaongeza kwa angalau kwa 10% TU, umeme kutoka JNHPP + Available Sources HAUTAWEZA kuhimili uchumi huo ambao kimsingi na wenyewe utakuwa ni uchumi wa kimaskini tu!!!

Kwa maana nyingine, hata kabla hatujamaliza deni la TZS 7 Trillion za JNHPP basi kuna uwezekano mkubwa sana demand ya umeme nchini inaweza kumeza umeme wote tulionao hivi sasa + Umeme utakaozalishwa na JNHPP!

Demand ikiwa kubwa, watakachofanya TANESCO ni ku-DISCOURAGE Matumizi Makubwa ya Umeme! Una-discourage Matumizi Makubwa ya Umeme sio kwa kutoa elimu bubu watoazo kwenye ma-tv bali watafanya hivyo kwa kupandisha bei ya umeme ili hatimae muache matumizi holela ya umeme, kama mlivyoacha kutumia majiko ya umeme bila hata kutandikwa bakora!!

Na hapa tukumbushane kwamba, kama kweli tunaamini bei itakuwa ndogo basi ni hiyo bei ndogo ndiyo itakuwa chanzo cha kukaribisha bei kubwa! Umeme ukiwa nafuu, matumizi ya umeme yataongezeka! Watu watatupa majiko yao na pasi zao za mkaa kwa sababu umeme ni cheap!

Wafanyabiashara wataachana na mashine za kusaga zinazotumia mafuta kwa sababu umeme ni cheap!

Matumizi ya vifaa vya umeme yataongezeka kwa sababu umeme ni cheap!!! Kule Uswahili ule ugomvi wa wapangaji kwamba wawe wanazima mafriji na mafriza yao utapungua kama sio kwisha kabisa kwa sababu umeme ni cheap, na watu watakuwa wanajiachia!!

OUTCOME?

More demand for power led from increased power consumption!! Njia ya kupambana na hilo? Nishasema hapo juu: discourage power consumption by increasing the price!!

IT'S SIMLE ECONOMY!

Is JNHPP White Elephant Project?

Yakitokea niliyosema hapo juu, HAIWEZI KUWA White Elephant Project lakini yasipotokea inaweza isiwe White Elephant Project lakini inaweza kuwa a STRUGGLING PROJECT!!

Tunahitaji uchumi mkubwa zaidi ili tuweze ku-consume hizo additional MW zitakazozalishwa! But don't forget, huo uchumi ukitokea itamaanisha NO MORE CHEAP ELECTRICITY kwa sababu power consumption itakuwa kubwa!!

Na isipotokea, ina maana Project Haitaweza kuzalisha pesa ya kutosha kulioa madeni yake, and hence becoming a STRUGGLING PROJECT!!

Yaani ndo ile inaitwa Ukichimama Nchale, Ukikimbia Nchale!! Sasa chagua mwenyee udungwe nchale wakati umesima au wakati unakimbia... MAUMIVU YAPO PALE PALE!!

Ndo vile tu umeme utaingizwa Grid ya Taifa lakini kama ingekuwa unakuwa distributed kipeke yake peke yake, watu wangeukimbia huo kama wanavyolikimbia Daraja la Kigamboni!!!
Nimefurahi kukuona hapa kaka mkubwa, nikimalizana na pirika ntatulia nisome vizuri. Thank you for your time, I believe there's a lot to learn from your post.
 
Mkulu, Nina hamu sana kujua madhara ya miradi ya HEP kwa mazingira.

Lingine ni kuwa, kama kule jangwani Misri wanatumia Aswan dam with very little effect of evaporation. What about the place where there is a double maxima rainfall!!?
Wewe hujui km miti zaidi ya milioni moja kwa eneo la ukubwa wa mkoa wote wa Dar imekatwa kupisha ujenzi!!?

Unajua athari za kutokuwepo vegetation cover na uhusiano wake na climate hasa rainfall formation? Go back to school usinichoshe.
 
Wewe hujui km miti zaidi ya milioni moja kwa eneo la ukubwa wa mkoa wote wa Dar imekatwa kupisha ujenzi!!?

Unajua athari za kutokuwepo vegetation cover na uhusiano wake na climate hasa rainfall formation? Go back to school usinichoshe.

Zingine ni story tu mkuu wangu.

Here are the facts and figures:
Project Catchment Area: 1,590sqkM
Length of the dam: approx. 100km
Width of the dam: approx. 700m
Area of the dam: approx. 70kM
Height of the dam: approx. 130m

NB: The area of Dar region is 1,200sqkM.

Say again the size of land of which deforestation took place!!!?
Also understand the meaning of "catchment area".

Also you can walk through the below site for more insight.
 
Mkuu

Huu mradi unapigwa sana vita na lile genge na sasa hivi ni kama umepotezewa hivi. Wako busy kumtafutia Mchechu position.

Utaendelea lakini utafanyiwa sana figisu same to SGR unavyopigwa pancha.

Kama Taifa 10% zinaturudisha sana nyuma, zinakwamisha maendeleo ya nchi zote mbili. Tanzania Bara na Tanzania Visiwani.

Kwenye gas wajanja washaweka % zao kwenye kila mauzo yanayofanyika kutoka kwa supplier wa gas kwenda kwa Tanesco.

Gas iko Tanzania lakini hatuimiliki, inamilikiwa na kampuni fulani ya kibepari, Kampuni husika inafanya kuiuzia hiyo gas Tanesco.

Hayati Magufuli aliachana na umeme wa gas akaegemea upande wa maji zaidi sababu maji hatuuziwi kama ilivyo kwenye gas.

Ndiyo maana unaona sasa wanahamisha magori kwa gia ya kusafisha vinu vya gas (Tanesco) na kutuwekea mgao wa umeme kutuaminisha kwamba gas ni muhimu kuliko maji.


Kwa yaliyotokea kwenye mkataba wa Beker Botts yamechagiza kupunguza makali ya drama hiyo.

Bepari anaamini Africa ni bara la giza (Dark Continent) pamoja na kujitutumua kwetu katika utafutaji wa vyanzo vya uhakika vya nishati tajwa, bado tuko giza.

Bepari kwa kushirikiana watu wachache tuliowaamini kama viongozi anahakikisha tutaendelea kubaki na giza letu kwa vizazi na vizazi.

Naamini ili Nchi yeyote iwe na maendeleo hasa kwenye nyanja ya viwanda na teknolojia ni lazima kuwepo na nishati ya umeme wa uhakika , JNHPP ni nishati ya uhakika.

Tanzania ina geographical Location nzuri ambayo inaiwezesha nchi yetu kupata mvua za kutosha kabisa kwa mwaka.

Hivyo tukiacha siasa za matumbo na kutumika naamini umeme wa maji ni mwarobani thabiti wa kutatua changamoto zetu za kiuchumi na za kijamii.

Shukrani!
 
Zingine ni story tu mkuu wangu.

Here are the facts and figures:
Project Catchment Area: 1,590sqkM
Length of the dam: approx. 100km
Width of the dam: approx. 700m
Area of the dam: approx. 70kM
Height of the dam: approx. 130m

NB: The area of Dar region is 1,200sqkM.

The say again the size of land of which deforestation took place!!!
Also understand the meaning of "catchment area".

Also you can walk through the below site for more insight.
Now, this is how you dispel a lackadaisical propaganda: Numbers do not lie.
 
Ndugu yangu MALCOM LUMUMBA

Bidhaa Kuu kutoka JNHPP ni UMEME PEKEE, and there's little (if any) to no by-products zinazoweza kuzalishwa kupitia JNHPP! Kinyume chake, Bidhaa Kuu ya LNG Project ni Gas na sio umeme lakini hapo hapo unaweza pia kupata UMEME + TAKATAKA ZINGINE!
Kaka CHIGE nimetulia na kusoma vizuri huu mchango wako na nikiri nimejiufunza mengi sana. From Economic Stand-Point, you have made Hell of an argument. Kweli nakumbuka mwaka 2018 uliwahi kulizungumzia sana hili kule INTERNATIONAL FORUM. Hivyo kutoka kwenye haya uliyoyasema, mimi naomba niulize tu suala lifuatalo:

Hata kama huu mradi wa JNHPP hauna manufaa makubwa kiuchumi (The Multiplier Economic Effect) kama ilivyo gesi, kuna haji gani yoyote ya kufanya hujuma ??? Nasema haya kwasababu kauli kutoka juu zimekuwa nyingi sana, zinazokinzana na kubadilika-badilika. Kama gesi nayo ni njia sahihi, kwanini basi tusifanye miradi yote kwa pamoja: Kwani hatuwezi kuwa na JNHPP na miradi ya umeme wa gesi pia ???

Ikumbukwe kama ulivyosema, The Multiplier Effect: Hayo mashirika ya gesi yanazo faida nyingi zaidi kibiashara kutoka kwenye gesi. Gesi ina matumizi mengi kwa dunia hii ya leo zaidi ya ufuaji umeme. Gesi pekee inasaidia katika utengenezaji wa Petro-Chemicals ambazo hutumika kutengeneza bidhaa muhimu kama plastiki, rangi, mbolea na madawa ya binadamu na mengineyo. Au ni lazima hayo mashirika yauze pia gesi kwa TANESCO ili tuweze kufua umeme ???

Lakini pia, binafsi naona hakuna shida yoyote ile Tanzania yetu inaweza kupata kwa kuwa na umeme wa maji, gesi, upepo au nyuklia. Tena hili litakuwa jambo jema kabisa. Kama nilivyosema hapo juu kuhusu Tennessee Valley Authority (TVA), wana vyanzo vingi vya nishati. Wana umeme wa maji, gesi, upepo na nyuklia na hawapati tatizo lolote: Kwanini kwetu huku tatizo ndiyo lionekane sana. Kwani ???
 
Mi nauliza tu, na nitakuwa nayliza kila siku asubuhi na jioni kwa kila uzi wa bwawa la Nyerere. Crane la tani 26 liko wapi?
 
Ndugu yangu MALCOM LUMUMBA,

Amini usiamini, suala la Hujuma dhidi ya JNHPP ni Propaganda tu. Hakuna hujuma yoyote!! Ni saa chache tu zilizopita nilikutana na post moja ikizungumzia hilo suala la hujuma, na mtoa hoja hiyo akadai, kama si hujuma dhidi ya JNHPP basi kwa sasa Bwawa lingekuwa tayari.

Hapo hapo nikagundua mtoa mada HAKUWA NA TAARIFA SAHIHI. Wakati mradi unaanza, ilitarajiwa mradi ungekamilika na kuwa operational by June 2022. Kwa maana nyingine, hata kabla ya hiyo June 2022 haijafika, mtoa mada anaamini kama isingekuwa hujuma, hivi sasa mradi ingekuwa umeshakamilika!

Wakati mwingine watu huwa wanachanganya madesa kutokana na taarifa kama hizi, especially wanapoishia kusoma heading:-

Mradi kuchelewa.png

Hiyo habari ni ya November 2021. Sasa watu wakiona habari kama hiyo wanakimbilia kusema "Kuna hujuma"! Lakini kisome kipande hicho cha habari kisha linganisha na CAG REport ya 2019/2020

Kama si kuchelea kuifanya post kuwa ndefu basi ningeweka angalau SECTION mzima ya taarifa husika. Hata hivyo, unaweza kufanya your own assignemnt kuhusu: Annual General Report of the CAG For the Financial Year 2019/2020.

Chapter 6, Page 117 ya taarifa hiyo ya CAG inazungumzia JNHPP. Aidha, subsction "c" on Page 121 utakutana na haya maneno:-
This means that with the construction of one instead of two diversion tunnels, the discharge capacity has been reduced by 11.9% (from 7000m3/second, which was originally planned, to 6170m3/s which was actually constructed). This eventually led to project delay for five months as a result of the coffer dam overtopping and subsequent flooding of the diversion tunnel. This effect could be avoided if due care had been taken in implementing the two-diversion tunnels design by excavating one tunnel after another.

Unaona hapo Ripoti ya CAG ya 2019/2020 ilizungumzia mradi ku-delay kwa miezi 5, na sababu ndo hizo hizo zilizotajwa kwenye habari ya Habari Leo ya Nov 2021.

Hapo unapata picha gani! Wakati mdau yule akiamini kwa sasa ulitakiwa uwe umekamilika, kumbe taarifa sahihi ilibidi uwe umekamilika by June 2022 lakini bado pia ikatokea tena delay ya 5 MONTHS!!

Kinachoendelea hivi sasa ni hofu isiyo na maana yoyote kwa sababu hata ukiwauliza walio field, wanakuambia ujenzi unaendelea! Na kama ambavyo nilisema hapo kabla Legacy Defenders wanachanganya sana madesa! Kwa akili yao wao wanadhani LNG Project ni Power Generation Project inayolenga kuua Legacy ya JPM kupitia JNHPP kumbe ni vitu viwili tofauti!
Lakini pia, binafsi naona hakuna shida yoyote ile Tanzania yetu inaweza kupata kwa kuwa na umeme wa maji, gesi, upepo au nyuklia. Tena hili litakuwa jambo jema kabisa. Kama nilivyosema hapo juu kuhusu Tennessee Valley Authority (TVA), wana vyanzo vingi vya nishati. Wana umeme wa maji, gesi, upepo na nyuklia na hawapati tatizo lolote: Kwanini kwetu huku tatizo ndiyo lionekane sana. Kwani ???
Nakubaliana na wewe kwa 100%! Dunia ya leo, popote utakapoenda duniani wanazungumzia suala la Energy Mix kwa sababu No One Source is Enough especially dunia ya leo inayokumbwa na mabadiliko ya hali ya nchi!

Wewe ulitolea mfano wa sustainability ya TVA, and YOU'RE RIGHT lakini tusisahau wenzetu wapo more discipline. Wale hawawezi kufanya shughuli za kibinadamu kiholela pembeni mwa TVA lakini sisi tunaweza sana!

Na kimsingi, mimi siipingi JNHPP as JNHPP bali napinga issue mzima ya nishati ilivyokuwa handled. Seems like JPM aliaminishwa kwamba JNHPP ndo Alpha and Omega!! Matokeo yake nini?!

Baada ya kuwa tumeshavuta gesi kutoka Mtwara to Kinyerezi, Serikali ya JK ilikusudia kujenga 4 Power Generations Plants pale Kinyerezi! Lakini kwavile muda wake ulishaisha, akajenga tu Kinyerezi I, akaacha Kinyerezi II ikiwa kwenye mchakato.

JPM ilibidi sasa amalizie Kinyerezi II, III, na IV ili ku-guarantee umeme wa kutosha at least in the next few years. Hata hivyo, serikali ikafanya tu ile KInyerezi II ambayo mchakato wake ulishaanza, na III & IV zikapigwa chini na kuhamia kwenye Bwawa la Nyerere! Na kuna kila dalili JPM alikuwa misled kwa kuambiwa "umeme tulio nao unatosha" ndo maana akaamua kuachana kabisa na Kinyerezi bila kujua kwamba "umeme unatosha under ideal conditions."

Kwahiyo YES, hata baada ya kuona umuhimu wa JNHPP bado hatukutakiwa kuachana na vyanzo vingine ambavyo leo ukivigusia tu, utaambiwa FISADI au Unatumwa na Mafisadi ili wauze gesi kwa sababu watu wanaamini JNHPP ndo Alpha & Omega!!
 
Wazungu husema hivi "Once is an accident, Twice is a Coincidence, but Thrice is a Pattern".

Hapa namaanisha nini, duniani kote ambako miradi ya namna hii yenye lengo la kuwakwamua wananchi kwenye lindi la umasikini lazima kuwepo na malalamiko.

Tena nimefuatilia kwa umakini na kufahamu kwamba malalamiko hayo ni lazima yafanane. Mbaya zaidi makundi ya wanaoleta haya malalamiko huwa ni ya watu wa aina ileile, tena huja na sababu zilezile.

Ukifuatilia kwa umakini, utatambua kwamba mfanano wa hawa watu ni mkubwa sana hadi utakubaliana na ule msemo wa kiingereza kwamba "History does not repeat itself, but people do repeat themselves".

Fanya utafiti wako binafsi, utakubaliana na nilichokiandika hapa.

Muda ni mchache, leo hii ntazungumzia nchi tatu ambazo ni Marekani, Ethiopia na Tanzania. Ambako kote katika nyakati tofauti kumekuwa na miradi mikubwa ya kuzalisha umeme wa maji ambao kwa mkono wa serikali, ambayo imelenga kuzalisha umeme wa gharama nafuu kwa wananchi huku miradi hiyo ikiendeshwa na serikali.

Hapa nazungumzia miradi ya The Tennessee valley Hydro-electric Power Projects (TVA), The Grand Ethiopian Rennaisance Dam (GERD) na Julius Nyerere Hydro- Power Project (JHPP).

Nimefuatilia kwa karibu nimeona kwenye hii miradi ya TVA, GERD na JNHPP ni lazima utakutana na majina kama WHITE-ELEPHANTS, DEBT-RIDDEN PROJECTS, UNSUSTAINABLE ENERGY SOURCE, ENVIROMENTAL HAZARDOUS, GOVERNMENT MONOPOLY, UNCOMPETITIVE SOEs na SOCIALIST EMBARKED PROJECT.

Mpaka sasa sijafahamu kwanini tokea kule Marekani, Ethiopia hadi Tanzania mambo yafanane hivi. Imetokea TVA (Once=An Accident), Imetokea GERD (Twice= A Coincidence) na Imetokea Tanzania (Thrice= A Pattern).

Pia sehemu nyinginezo yanaendelea kutoka tu, mpaka najiuliza nini hiki. Labda, huenda ni mawazo yangu hafifu tu, ambapo wazungu husema "A figment of your own imagination"

HEBU TUANGALIE MRADI WA UMEME CHINI YA TENNESSEE VALLEY AUTHORITY

Raisi Franklin Delano Roosevelt alianzisha The Tennessee Valley Authority (TVA) mwaka 1933 ili kuwezesha Marekani izalishe umeme wa bei ndogo ambao utasaidia majimbo kama saba ambayo yanazunguka lile eneo.

Lengo kubwa ni kusaidia kiuchumi ukanda ambao uliachwa nyumba kimandeleo, kutoa ajira kwa vijana na kusukuma uchumi wa viwanda eneo hilo.

Tokea mwaka 1933 mpaka sasa Marekani imefanikiwa kutengeneza mabwawa 50 ambayo yanasaidia kuzalisha umeme wa bei ndogo unaotumika kuendesha viwanda na uchumi wa majimbo karibia saba ya eneo ambalo bonde la Tennessee limepita.

Ila huwezi amini mpaka leo hii mwaka 2022, wanaharakati wa kimazingira wanapinga huu mradi kwa kusema unaleta madhara.

Wakati nasoma shule kuhusu huu mradi, tuliambiwa kwamba ulipigwa vita sana na makampuni binafsi ya umeme, wanasiasa, wanaharakati na wanasheria.

Ambapo walitumia mbinu mbalimbali kufanikisha hujuma dhidi ya huu mradi lakini hawakufanikiwa. Sababu kubwa ni kwamba raia wengi wa Marekani walikuwa ni watu wanaojielewa mno, siyo wajinga wanaopelekeshwa bila kufahamu linaloendelea (Dumbed-Down Citizenry) nchini kwao.

Upinzani haukishia kwenye uanzishwaji wa huu mradi mwaka 1933, mwaka 1936 mmoja wa wamiliki wa hisa kwenye kampuni binafsi la umeme THE ALABAMA POWER COMPANY aitwaye ASHWANDER alipeleka kesi mahakamani kuzuia serikali kuuza umeme kupitia The Tennessee Valley Authority (TVA) akisema kwamba serikali haitakiwi kabisa kuuza umeme hivyo kuna uvunjifu wa katiba ya Marekani.

Unaweza kutafuta kesi ya: Ashwander V Tennessee Valley Authority (1936)

Mahakama ya juu ya Marekani ilikataa na kusema uzalishaji huu wa umeme siyo wa faida tu, bali ulilenga kutoa huduma kwa kukuza uchumi wa eneo ambalo lilikuwa nyuma kimaendeleo na kuimarisha ulinzi wa nchi kwasababu viwanda vya silaha vilikuwepo eneo hilo.

Hivyo mabwanyeye wakapigwa chini na serikali inauza umeme kwa raia mpaka leo hii. Ikumbukwe inayofanya hivi ni serikali ya Kibeberu ya ulimwengu wa kwanza na siyo serikali ya Kijamaa ya ulimwengu wa tatu.

Wamarekani zaidi ya milioni 9 wanapata huduma ya umeme nafuu kutoka kwenye miradi 29 ya umeme wa maji kutoka Tennessee Valley Authority (TVA).

Kubwa zaidi ni kwamba huduma ya umeme kwenye majimbo hayo yanayopitiwa na bonde la Tennessee ni moja kati ya umeme wenye gharama nchini Marekani, kama siyo ndiyo wenye gharama nafuu zaidi kwenye nchi hiyo.

Kitakachoshangaza watu werevu ni kwamba PROPAGANDA CHAFU na UZANDIKI dhidi ya mradi huu hazijaisha tokea mwaka 1936. Raisi Dwight Eisenhower alishawahi kuutukana huu mradi kwa kuuita maneno kama "Ujamaa nyemelevu" (Creeping Socialism), ilhali mamilioni ya Wamarekani ni wanufaika.

Maneno kama haya hayatakiwi kabisa kutoka kwenye kinywa cha mkuu wa nchi mwenye lengo la kuwakwamua kiuchumi raia wa kawaida, kwasababu faida za mradi ni dhahiri kwa watu wote.

Lengo la Raisi Eisenhower lilikuwa siyo kupinga UJAMAA bali ni kubinafsisha (TVA), lakini akakumbana na upinzani mkubwa kutoka kwa wazalendo wa kimarekani na mwishowe akawa mpole.

Kilichomshangaza zaidi ni kwamba waliompinga ni wenzake kutoka REPUBLICAN PARTY ambao husifika kwa kuchukia UJAMAA hasa pale ambapo serikali yenyewe hufanya biashara. Nini kilipelekea Raisi na jopo la wataalamu wake kupingwa hivi ???

Sasa kubwa na baya zaidi dhidi ya mradi huu ni lile la mwaka 2013, ambapo Raisi Barrack Obama aliandaa muswada ili kubinafsisha The Tennessee Valley Authority (TVA) kwa watu binafsi.

Moja ya sababu kubwa ambayo Raisi Obama na washauri wake waliitoa ni kwamba mamlaka ya Tennessee Valley (TVA) ina madeni makubwa ambayo ni mzigo kwa serikali.

Walikuwa na hoja nzito sana maana ukweli ni kwamba mamlaka hiyo (TVA) ina madeni makubwa ambayo ni takribani dola za kimarekani bilioni 25.

Lakini hili halikuwa sababu ya kusema kwamba serikali ibinafsishe shirika hili la kiserikali na kuwaumiza raia wapatao milioni 9 kwa kupanda kwa gharama za umeme.

Sababu ya pili ambayo Raisi Obama na washauri wake waliitoa ili kufanikisha ubinafsishwaji wa The Tennessee Valley Authority (TVA) ni ile ambayo hata kwetu huku inatusumbua ya kutunza mazingira.

TVA mbali na miradi 29 ya umeme wa maji, imeongeza pia miradi 12 ya umeme wa makaa ya mawe, miradi 3 ya umeme wa nyuklia, miradi 15 ya umeme wa gesi na mradi 1 wa umeme wa upepo.

Inasemekana TVA inahitaji dola za kimarekani bilioni 25 ili kupunguza uchafuzi wa mazingira unaosababisha na huu mradi hasa kutoka kwenye vinu vya makaa ya mawe. Hivyo ili serikali isiingie kwenye hizi gharama zisizo za msingi, basi ni kheri ibinafsishe tu shirika hili.

Kuna nchi fulani hivi viongozi wake, wasomi na wafanyabiashara wanapenda kuzungumza kauli kama hizi za Raisi Barrack Obama na Dwight Eisenhower, bila shaka ndugu msomaji utakuwa unaifahamu.

Hivyo njia rahisi kwa Serikali ya Raisi Obama, kukwepa deni kubwa la TVA na gharama za marekebisho, wakaona ni bora wauze hii SOE (State Owned Enterprise).

Ila ukweli mchungu ni kwamba wangefanya hivyo ina maana gharama za umeme kwa wananchi wa Marekani zaidi ya milioni 9 ingepanda sana na wangeathiri biashara nyingi na maisha ya raia wa kawaida.

Mbali na madhaifu yake mengi, Marekani ni taifa ambalo raia wake wengi wanajielewa mno.

Wahafidhina wa chama cha REPUBLICAN hasa wawakilishi kutoka majimbo hayo, pamoja na watu binafsi walipinga kwa nguvu mswada ambao ungefanikisha ubinafsishwaji wa kiholela wa hii mamlaka ambayo lengo lake kuu ni kutoa huduma kwa raia na kuimarisha ulinzi wa nchi.

HEBU TURUDI NCHINI TANZANIA SASA, TUANGALIE TANESCO NA JNHPP

Bunge la Marekani lilichofanya ni kukataa mamalaka isiuzwe na kuiwekea ukomo wa deni, ambayo mamlaka haitakiwi kuvuka, ambapo ukomo ni dola za kimarekani bilioni 30.

Hivyo madeni hayapo tu kwenye shirika letu la TANESCO lakini hata TVA wana madeni tena yanakera. Sisemi haya kusema TANESCO inafanya vizuri, la hasha kuna mambo mengi ya ajabu yanafanyika.

Lakini naamini wakijipanga vizuri na kupunguza siasa tunaweza kufika sehemu nzuri sana. Mbona TVA wafananya vizuri na bado ni shirika la serikali ???

Jambo jingine ambalo nalisikia sana nchini Tanzania ni hilo la kusema umeme wa maji siyo endelev. Mimi siyo mtaalamu lakini naweza kufahamu wapi nadanganywa, kiukweli hili linanipa ukakasi mkubwa sana.

Mradi wa TVA umeanza mwaka 1933 na upo hadi leo hii, utasemaje kwamba umeme wa maji siyo endelevu jamani ???

Unaweza kumtukana Raisi Magufuli kwamba ni mjinga, lakini kumbuka huu mpango wa JNHPP umekuwepo tokea enzi za Mzee Nyerere, Mzee Mwinyi na Mzee Mkapa, ina maana hawa wote na wataalamu wao walikuwa ni wajinga kabisa wasitambue kwamba Hydro-Electric Power is not sustainable source of energy ??? Aidha ni kweli sisi watanzania ni watu wajinga sana pamoja na viongozi wetu, AU kuna kitu kinachoendelea nyuma ya pazia sisi raia wa kawaida hatukioni.

Jambo kubwa zaidi la kujiuliza hapa: Ni kwamba kama mradi wa TVA ambao manufaa yake yanaonekana kwa mamilioni ya wananchi wa Marekani unapigwa vita kali hivi, tena hadi na viongozi wa serikali wakiwemo maraisi, sisi huku kwetu Tanzania tusipingwe kweli ???

Mwaka jana miezi ya mwishoni nilikuwa nafuatilia wanaharakati mitandaoni, nikasikia baadhi wakisema mamilioni ya miti yamekatwa na uharibifu mkubwa wa mazingira umefanyika kwenye mradi wa JNHPP ndiyo maana mvua zimegoma Tanzania.

Lakini, wengine wanasema kwamba JNHPP ni tembo mweupe (A White Elephant Project). Majibu ya Waziri Makamba, yamakuwa yakibadilika-badilika. Lakini naamini, ukweli tutaufahamu tu.

Wanaharakati wetu wangepinga huu mradi (JNHPP) peke yake sisi tungeelewa labda na binafsi ningesema hebu tujifanyie tathmini. Lakini hakuna mradi wowote mkubwa ambao umewahi kufanyika nchini Tanzania bila kupata upinzani mkubwa:

Uwe ni mradi wa msaada, uwekezaji au mkopo. Nasema hili kwa UJASIRI WOTE, kama upo naomba nitajiwe ili nijifunze.

Ukifuatilia kinachoendelea kwa wanasiasa wetu kuna sababu nyingi sana zinazoletwa ambazo hazina kichwa wala miguu.

Wengi wetu ni UJINGA, WOGA, BENDERA FUATA UPEPO lakini kubwa ni ULAJI TU wa watu wachache ambao wamevaa ngozi ya kutunza mazingira, kulinda katiba, matumizi ya mbinu za kisasa za kisayansi na kibiashara kuendesha sekta ya nishati nchini. Lakini ni hivi: UKWELI UKO KAMA MIMBA, HUWEZI KUUFICHA MILELE. Tutafamu tu...

NAMALIZIA NA ETHIOPIA, MRADI WA THE GRAND ETHIOPIAN RENNAISANCE DAM

Ingekuwa Tanzania ndiyo nchi pekee ndiyo inayopigwa vita kwa kuanzisha mradi kama huu ningesema, basi tujifanyie tathmini kidogo.

Ila hadi kule kwa ndugu zetu Ethiopia yametokea machafuko makubwa sana kupinga uanzishwaji wa The Grand Ethiopia Rennaisance Dam (GERD) ambalo litakuwa msaada mkubwa sana kwa mamilioni ya wahabeshi nchini humo.

Upinzani umekuwa mkubwa imefika kipindi kwamba Raisi wa Marekani Donald Trump akaweka bayana kabisa kwamba Misri inaweza kulipua bwana hilo" Egypt might blow up the dam".

WIKILEAKS wanasema kwamba, mradi huu ukimalika hautaisaidia Ethiopia peke yake kuzalisha umeme wa bei ndogo, bali utazalishwa umeme mwingi (Megawatts 5,250) ambao utauzwa hadi nchi jirani kama Sudan na serikali ya Sadani inafahamu hili vizuri kabisa.

Sasa ukifuatilia kwa umakini, kuna wanasiasa wakubwa ambao walisema wazi kwamba mradi wa GERD, hauna manufaa na ni tembo mweupe ( A WHITE ELEPHANT). Moja kati ya watu waliowahi kusema hivi ni Raisi Isaias Afwerki wa Eritrea.

Lakini mradi huu ukikamilika, umeme wa gharama nafuu utafika hadi nchini kwake. Watanzania tujiulize kitu hapa: Kama umeme wa maji siyo wa muda mrefu (Not Sustainable), hivi iweje serikali ya Uchina itupe zaidi ya dola za Kimarekani bilioni 1, ambazo ni sawa na trilioni mbili za kitanzania au zaidi kwenye mradi ?

Asasi za kiraia (NGOs) nazo haziko nyuma katika kutuonesha madhara ya mradi huu wa GERD. NGO maarufu iitwayo INTERNATIONAL RIVERS kutoka California, nchini Marekani iliandaa ripoti kubwa kabisa kuonesha madhara ya mradi huo kwenye mazingira. Wakaenda mbali zaidi na kusema kwamba bwana hili linaweza kuchangia mabadiliko ya hali ya nchi.

Ikumbukwe hawa ndugu zetu wamezungumza sana juu ya miradi ya umeme wa maji nchini Tanzania na Ethiopia.

MWISHO KABISA: MAONI YA WANAZUONI KUHUSU SIASA ZA UMEME NA MABWAWA

Kama umefuatilia siasa za Afrika kwa muda mrefu, utatambua kwamba huu mchezo haujaanza na Tanzania wala Ethiopia. Prof Mike Muller ambaye ni mhandisi kutoka chuo cha Witswatersrand Afrika Kusini, amawahi kuandika na kusema siasa za kupinga miradi mikubwa ya umeme wa maji zilianza mapema nchini Misri kipindi cha Gamal Abdi Nasser ambapo alitaka kujenga bwawa la Aswan (ASWAH HIGH DAM) ambalo lingezalisha MegaWatts 2,100.

Prof Asit K. Biswas amtaalamu wa maji na mazingira, ambaye ndiye anaongoza kwa kufanyiwa rejea za kitaalamu linapokuja suala za mazingira na maji, akishirikiana na Prof Cecilia Tortajada waliandika chapisho ambalo limesema kwamba mradi wa BWAWA LA ASWAN una madhara makubwa kwenye mazingira.

Lakini ukweli ni kwamba wataalamu mradi huo ulipokamilika mwaka 1970, ulikidhi nusu ya mahitaji ya umeme nchini Misri.

Ikimbukwe kwamba siasa za ASWAN HIGH DAM ziliwahi kupelekea Misri ivamiwe kijeshi na Uingereza, Ufaransa na Israeli. Nasser alisema alitaifisha Mfereji wa Suez kwasababu maji yake ni muhimu kwa ujenzi wa bwawa la Aswan.

Nasser aliomba msaada kwa serikali ya Raisi Eisenhower ili kujenga bwana la Aswan, lakini Eisenhower aligoma.

Raisi Kennedy alikosoa sana haya maamuzi ya kuvuruga miradi ya Afrika akisema hivi "When we abruptly abandoned the Aswan Dam in Egypt, the Russians went ahead to finance it. While we starve the Development loan Fund, the Sino-Soviet bloc has already passed us in economic assistance to selected key areas" Hili ndilo lilitokea bwawa lilijengwa na Warusi.

Maajabu barani Afrika huwa hayaishi kabisa: Kinachotushangaza wengi wetu leo hii ni kwamba Misri ambao miaka ya nyumba walionewa katika kujengwa bwawa la Aswan (ASWAN HIGH DAM), leo hii wao nao wakishirikiana na mataifa makubwa nje, wanaharakati na asasi kubwa za kiraia, wanafanya hujuma kubwa sana dhidi ya mradi wa GERD nchini Ethiopia.

NB 1: Siasa kama hizi, zilionekana pia kule nchini GHANA kipindi cha marehemu Nkhrumah ambapo alikuwa anataka kujenga bwawa la AKASOMBO (The Akasombo Dam) ili kuzalisha umeme.

Uliundwa mtandao mkubwa sana wa watu ndani na nje ya nchi ili kumzuia. Muda ni mchache sana siwezi kuzungumza kilichotokea.

NB 2: Fanya utafiti wako kuhusu miradi mikubwa ya uzalishaji wa umeme kupitia maji (TVA, GERD, JNHPP) pia hata ASWAN HIGH DAM na AKASOMBO DAM utatambua kwamba siasa zake zinafanana.

Wahusika ni walewale, wakitumia mbinu zilezile, sema tu huja wakiwa wamevaa vingago (Masks) tofauti-tofati. Kiufupi hizi siasa zinachezwa sana kitaalamu na wengi wetu tunafuata upepo bila kufanya tafiti binafsi.

Mimi siyo mtaalamu sana wa haya mambo, hivyo naomba wale wajuvi wanisaidie zaidi kuelewa. Nitafurahi kurekebishwa na kuelekezwa pale ambapo nimepotoka na kutofahamu kinachoendelea.

CC: JokaKuu , Nguruvi3 , UmkhontoweSizwe , TUJITEGEMEE
Ndugu msomi umesahau mradi mkubwa wa INGA 1&2 ya DRC ambayo ingeweza kutoa umeme kwa nusu yote ya Afrika lakini mabeberu wameuua kabisa huo mradi,,,,Ona leo mabeberu wanazungumzia Russia kuivamia Ukraine kwa swala au sababu moja tu kubwa ambayo ni bomba la gesi kutoka Urusi hadi Ujerumani kupitia Ukraine. Kwa ufupi mabeberu hawapendi wafrika muwe na enough and reliable energy especially electricity ili kuwachelewesha kimaendeleo na kibaya na kuwarahisishia mabeberu huwatumia wafrika wenyewe kwani mzungu haji moja kwa moja kutusimamisha,,,Kumbuka ati Nape alipinga mradi wa bwawa la Nyerere kwa kigezo cha kipuuzi cha uharibifu wa mazingira,,Magufuli aliwaona mabeb eru kwa jicho la ndani sana Mungu amuweke mahali pema pepona na tutamkumbuka sana
 
Mkuu huku tunakorudi hatutapiga hatua, ni sawa na kukanyaga mafuta mengi wakati gari iko kwenye free gear!
Hiyo power master plan yenyewe mwendazake aliibadilisha akaweka huo mradi..
Mjadala nadhani ungekua kwamba;
※ Kwanini aliamua kufinance hiyo project kwa mikopo ya kibiashara tena ya muda mfupi na riba kubwa. Juzi tumeambiwa marejesho yameshaanza na project haijakamilika ikabidi tutumie mkopo mwingine kulipa huo mkopo kitu ambacho nakiona kama ukichaa!
Jambo usilojua ni kuwa kama Magufuli angekuwepo leo hii... huo mradi kitambo sana ungekuwa umekamilika... so hao walioamua kuhujumu ndo uwaulize kwanini hawajaumaliza ili mradi uanze kulipa deni la mkopo waliokopa... simple logic... acheni uchawi... Magu was a National Hero.
 
Back
Top Bottom