Mradi wa bandari ya Tanga ulifia wapi?

Duh! Pole sana Leo Tanga na nyie mmeshukiwa na JF. Jamani swala la kuendelea bandari ni la serikali. Sasa uvivu wa wazigua na wabondei unatoka wapi? Hivi wanaweza kuwa wavivu halafu wakafyatua pisi kali ninazoziona Tanga?
 
Mnao sema tanga ni wavivu tunaomba na nyinyi mtaje mikoa yenu tuijue tuone maendeleo yenu tunaviwanda vitatu vya cement kaskazin yote inajenga kupitia tanga chokaa yote na gpsam inatoka tanga mafuta ya kujipaka podoa mamujii Asher's tanga jiwe la tanga stone la ulembo linatoka huku mafuta yote ya mikoa ya kaskazin yanapitia tanga nazi zote unazo jua huku ndo kwao
 
Duh! Pole sana Leo Tanga na nyie mmeshukiwa na JF. Jamani swala la kuendelea bandari ni la serikali. Sasa uvivu wa wazigua na wabondei unatoka wapi? Hivi wanaweza kuwa wavivu halafu wakafyatua pisi kali ninazoziona Tanga?
washamba tu wataje na kwao tujue wanataka mikoa yote iwe Kama dar
 
Tanga unakwenda dukani saa tano asubuhi kununua soda, unakuta mtoto mdogo anakwamba kaka Juma alalaaa.

Yaani Juma alivyokuwa mvivu kafungua tu duka halafu karudi kulala!. Unabaki kushangaa huyo mtu analalaje wakati muda huo ni joto kali.
Kafiri unapata tabu kule raha tu
 
kama imetupwa vile ? Mradi huu umefia wapi ?
Nilipokujibu hapo juu kifupi, nilikuwa sijasoma andiko lako lote hadi mwisho.

Sasa nimelisoma lote, na nina machache ninayoweza kukuchangia.

Awali ya yote, majibu ya maswali yako mengi kumbe umekwishayajibu mwenyewe, kwani unao ufahamu wa ujio wa bandari ya Bagamoyo, ambayo kwa kiasi kikubwa inakidhi hayo uliyoyataja juu ya bandari ya Mwambani, hata kama siyo yote.
Kwa hiyo, inaonekana unao ufahamu wa mambo yalivyogeuka toka Tanga hadi Bwagamoyo, lakini bado unauliza maswali, nadhani kwa kutaka tu watu wajadili mada yako. Siyo vibaya.

Nieleze wazi, niko upande wako. Nimechangia mara nyingi kwenye mada za namna hii zilizoletwa humu JF, nikiipambania Mwambani, kwa sababu najuwa ina manufaa makubwa zaidi, kama ulivyoelezea wewe kwenye mada yako, na hata zaidi; kama vile kwa Tanzania kutotegemea bandari ya Mombasa, huku tukiwa na powani ndefu kabisa. Hivi unajuwa kwamba asilimia karibu ya 7.2 ya mizigo inayopitia Mombasa kwenda nje ya Kenya ni ile inayokuja Tanzania? Uganda ikichukuwa zaidi ya asilimia 82?
Maajabu ni kuwa, hata tumewajengea barabara nzuri kabisa toka Holili, ikipitia Moshi/Arusha kwenda Singida na kuchepuka kuelekea Tabora na Burundi? Nchi yetu hii, imechukua mikopo WB, ili barabara ijengwe kupitisha mizigo inayotokea Mombasa kwenda Kaskazini mwa Tanzania, na hadi kuipeleka Burundi! Lakini tunashindwa kabisa kuendeleza/kujenga bandari ambayo ipo jirani kabisa na maeneo haya ili nchi yetu ipate faida zaidi!

Kuna watu hupenda sana hizi 'conspiracy theories' za kusema huenda tuna mapandikizi ndani ya nchi yetu yanayoshika nafasi za juu ku-'undermine' juhudi zetu kwa manufaa ya watu wengine. Mambo kama haya yanapojitokeza hivi, inakuwa ni vigumu sana kutowazia haya ma-'conspiracy' yanayosemwa mara kwa mara

Bagamoyo ni nzuri, lakini nadhani Mwambani ingekuwa nzuri zaidi. Na yaliyosemwa kilaghai na Kikwete wakati akiwatuliza watu wa Tanga juu ya kuwanyima ahadi yao ya bandari ya Mwambani, ni kwamba mpango huo ungeweza kuendelea kama mwanzo, eti kwamba watu binafsi watachukuwa jukumu la kuuendeleza. Huu ni ulaghai wa kijinga sana kuwaambia watu, ambao alikuwa amewapa matumaini makubwa juu ya bandari ile.

Nakusihi usiwe mvivu wa kurejea michango iliyomo humu JF, kwani kuna mambo mengi sana yalikwishaandikwa kuhusu haya yote unayotaka yajadiliwe tena.

Nimetiririka tu, kama kuna makosa, naomba radhi. Sikufanya masahihisho.
 
Tanga ilikufa mwaka 90 na kitu kweny miaka 2000 na kitu wagosi wa kaya waliimba ile kunani pale tanga mbona kila kitu kimekufa

Baadhi ya viwanda na wawekezaji walikimbia kenya hata anjari aliambiwa ahame dar akakataa akasema bora asiwekeze izi zote ni juhudi na hujuma

Inashangaza barabara ya kwanza ya lami ,shule ya kwanza, mahakama ya kwanza kila kitu kule ila nyerere alikuja kuua kabisa sababu tunajua aliona kule ni waislamu wengi kama Zanzibar

Na kupandikiza propaganda za kuwaita wavivu tunajua sisi wa ukanda wa bara tuna imani zetu na tamaduni zetu ndo maana leo wengine hawamtaki rais samia kisa mzenji
Pwani uvivu na utegemezi ndio asili yao..tangu enzi hizo mpaka sasa..hilo halijifici waarabu waliwaharibu akili..

#MaendeleoHayanaChama
 
sasa kama hiyo bandari ya Dar yenyewe imetushinda kuiendesha unataka tuliendee fupa lingine...tuendelee kucheza baikoko tu...
 
Huu Mradi kama unafufuliwa ukiangalia na bandari ya bomba la mafuta nalo pale chongoleni asee tanga naiona milestone
 
Msimsingizie Nyerere watu wa Tanga uvivu umewazidi. Na kupenda fitina zaidi kuliko kutanguliza ubinadamu, nongwa nyingi sana Tanga mjini.
Kwa sasa labour force hutoka popote,SGR ya dar moro na Bwawa la nyaźerere wengi wametoka bara kuja kisaki kufanya kazi.sasa hivi soko la nguvu kazi isiwe sababu,si tuhoji na tuangali Maslahi ya Taifa.
 
Back
Top Bottom