Mradi wa Bandari Bagamoyo bila uwazi wa ubovu wa mkataba, ni usaliti wa Bandari zilizopo

Hivi zile ndege za Mwendazake mnazoshangilia huku zikiendelea kulitia hasara taifa, mmeshawahi kudai uwazi kwenye ununuzi wake?

HIvi unadhani Lowassa ni kilaza namna hiyo?! Jombaa, that's politics... kama politics za Magu na CCM yake ya kutoa 50M kwa kila kijiji, na laptop kwa wanafunzi!!!

Moja ya hoja zinazotolewa na wapinzani wa Mradi wa Bandari ya Bagamoyo ni kwanini isijengwe Bandari ya Tanga!!! Sasa inakushangaza Lowassa akiwa Tanga kwenye kampeni kusema atasitisha Mradi wa Bandari ya Bagamoyo na serikali yake ku-focus Bandari ya Tanga?

Hivi nyie wafuasi wa Magu mmewahi kuoneshwa mkataba upi tangu taifa hili lianzishwe?! Of course, suala la uwazi wa mikataba limekuwa ni kilio cha muda mrefu hadi bungeni, lakini mbona hatuwaoni mkililia kuonesha mikataba kama ya SGR, ununuzi wa ndege, Mradi wa Bwawa la Nyerere, n.k?!

Hivi ni kweli hoja yenu ni kuona mkataba au mnajaribu ku-justify hoja za Magu na kujificha kwenye issue ya mkataba?!

Umetumia vigezo gani ku-conclude hiyo hoja yako?! Magu alipuuza hata miradi ya gas kule kusini, na akaishia kudanganya watu kwamba eti gas imeuzwa bila kutaja wauzaji ni nani, na waliouziwa ni akina, na serikali yake inachukua hatua zipi!!

Je, unataka kusema uwekezaji kwenye gas hauna faida wakati hadi sasa kuna kiasi kikubwa kabisa cha umeme tunaotumia unatokana na gas, wakati ni sehemu ndogo tu ya gas iliyochimbwa hadi sasa!!

Hiyo miradi mingi ni ipi?!

Tunashind
Nilipata muda nitajifunza vitu vichache kwako
 
Tunashindana na nchi ipi?! Fuatilia historia uone ndoto ya bandari ya Bagamoyo imeanza lini!!!
Mkuu Chige,

Unamuda mrefu sana ukiutetea huu mradi licha ya kuwa mpinzani, na wapinzani wengi tulionao leo wanaamini, kila kitakachoanzishwa na CCM, siyo kitu kizuri tu, katika hili umekuwa tofauti nao kabisa

Lakini, licha ya kuwa mtetezi wa mradi huu, Hujaweza kabisa kuainisha hasara ya uwekezaji wa matrion yetu kwenye bandari zetu mama kipindi vitakapokosa shehena ya mizigo

Ni kivipi Serikali itakavyokuwa ikihaha kupata mapato yake kutokana na bandari zetu zitakapokufa

Kwa kuwa Mh Raisi hayati Magufuli, alidokeza kuwa, baada ya mradi kukamilika kujengwa kwake, TRA na mamlaka zote za napato nchini, hazitaruhusiwa kutia miguu katika bandari hiyo

Lakini pia, hilujaweza kabisa kuainisha ukaribu wa bandari iliyopo Posta na itayojengwa hapo mbegani Bagamoyo kwamba, madhara yake ni yepi,

Kwa nini hujashauri kwamba, Kwa kuwa nchi yetu tunaeneno kubwa la mwambao wa bahari, ni vyema bandari hii inayotaka kujengwa Bagamoyo ikenda kujengwa angalau hata Saadani kule, ni mfano huo

Ukaribu wa Bandari hizi kati ya Dar na Bagsmoyo, ni kama kilomita zisizozidi 60 hivi, hauoni ni njia ya kuiuwa bandari yetu ya Dar?
 
Najiuliza kwanini Magufuli pamoja na kuwapenda kwake wachina na kuwaita marafiki wa kweli lakini bado aliukataa huu mradi wao, nadhani hapa lipo la kutafakari, tusiende kishabiki tu.
Angekuwa anawapenda kama unavyotaka kutuaminisha angewanyima mradi wa SGR?
 
Uongo wa Mwendazake ulikuingia vizuri unajua mradi wa Bwawa la Mwalimu ni mkopo toka benki za Egypt na mkandarasi ni Arab Contractor, nani anajua kwenye huomradi tutalipa bei gani?
Hii ni balaa nyingine kubwa tuu kwa nchi yetu. Inasemekana mitambo inayowekwa huko siyo mipya bali imepigwa polish tu. Habari za kuaminika zinasema ni mitambo ya mwaka 1984 tunajengewa leo. Kama ni hivyo efficiency yake itakuwa hafifu sana na haitadumu.
 
Mkuu Chige,

Unamuda mrefu sana ukiutetea huu mradi licha ya kuwa mpinzani, na wapinzani wengi tulionao leo wanaamini, kila kitakachoanzishwa na CCM, siyo kitu kizuri tu, katika hili umekuwa tofauti nao kabisa
Man, labda tu hujawahi kuona posts zangu zingine, au labda kwavile mimi mara nyingi huwa sio muanzishaji wa mada bali nimekuwa mchangiaji zaidi kuliko kuanzisha!

Kwa mfano, SGR niliiunga mkono na hadi kesho naiunga mkono ingawaje tatizo langu kwenye SGR, ni mikakati ya kuifanya kuwa commercially viable!

Ni kutokana na hilo, ndo maana nimekuwa nikihoji ikiwa serikali ilifanya tathmini ya kutosha kuona ni kwanini transporters wameacha kutumia TAZARA na badala yake kutumia malori, ili tatizo litakaloonekana huko TAZARA lisijirudie upande wa SGR!
Lakini, licha ya kuwa mtetezi wa mradi huu, Hujaweza kabisa kuainisha hasara ya uwekezaji wa matrion yetu kwenye bandari zetu mama kipindi vitakapokosa shehena ya mizigo
Sina uhakika kama umeisoma thread yangu yote kuhusu huu mradi!

Ingawaje thread yangu ni ndefu sana lakini nilichoandika ni sehemu tu ya issue mzima, na ndo maana kwenye hiyo thread nimeweka part ya RECOMMENDATION ambayo sijaandika chochote, but NITAANDIKA wakati ukifika!!

Ninachofanya sasa ni kuonesha ni tu kwanini huu mradi ni muhimu sana kwetu, na kwanini isiwe Dar Port, Tanga Port, n.k!

Hapa najaribu ku-challenge hoja za wale wanaoona mradi hauna maana. Hoja za kusema "tukimpa Mchina tumekwish" as if kuna financier malaika kwetu!!!

Awe Mchina, Mjerumani, Mmarekani, au Mjapani... wote hawa ni wale wale!!! The problem, hao wengine KATU hawawezi kukujengea hiyo bandari... NEVER!

Hapa najaribu ku-challenge hoja za kijinga kama vile JK kautaka huu mradi kuwa B'moyo kwa sababu ni kwao as if watakaofaidika na huo mradi, hata kwa ajira ni Wakwere peke yao, ambao wewe na mimi tunajua wazi kwamba linapokuja suala la ajira, hao Wakwere hawatakuwamo hata among Top 20!!

Of course, Wakwere watafaidika kwa ardhi yao kupanda thamani, lakini hata Mchanga, Mpogolo, Mhehe, and anyone else leo anaweza kwenda kununua ardhi Bagamoyo kwa bei ya chini, na baadae akaja kuiuza kwa bei ya juu baada ya ardhi kupanda thamani kutokana na uwekezaji huo!!

AND REMEMBER, wala sio kwamba naamini kwa hivi hivi ilivyo mradi unatakiwa kutekelezwa, HELL NO, bado kuna mengine tunayotakiwa kufanya ili mradi uwe na manufaa kwa taifa!

Hicho kipengele ni discussion ya baadae, na ndo maana thread yangu ina kipengele cha RECOMMENDATIONS ambacho sijaandika chochote, mbali nakuipandisha post ya ndugu yangu MALCOM LUMUMBA lakini I have a lot to say kwenye hicho kipengele!!
Ni kivipi Serikali itakavyokuwa ikihaha kupata mapato yake kutokana na bandari zetu zitakapokufa
Lengo la thread yangu ya sasa, na michango mingine ni kujibu hoja kama hizo ambazo, amini usiamini, watu wanazusha tu... ama kwa kutojua au kwa kujua!! Madai kwamba eti Mchina kapiga marufuku bandari zingine zisiendelezwe sio madai ya kweli.

REMEMBER: Awamu ya IV walianzisha mambo mawili kuhusu bandari; la kwanza Dar es salaam Maritime Gateway Project iliyolenga kuboresha Bandari ya Dar es salaam, na pili, Tanzania Ports Masterplan iliyolenga kuangalia bandari zingine nje ya Dar, na uwekezaji wa bandari mpya!!

Plan zote mbili hizo zimekuwa zikienda bega kwa bega!

Kwa mfano, mkataba wa upanuaji wa Bandari ya Dar es salaam ulisainiwa somewhere 2014 or 2015; wakati ule ule uliosaniwa Framework Agreement ya Bandari ya Bagamoyo!

Kama habari za kwamba Mchina amesema bandari zingine zisiendelezwe zingekuwa za kweli, basi mkataba wa upanuzi wa Bandari ya Dar es salaam usingekuwepo! Sote sisi tumeshuhudia Bandari ya Mtwara ilivyokuwa inaboreshwa!

Lau kama habari za marufuku zingekuwa za kweli, basi ule uboreshaji wa Bandari ya Mtwara usingekuwepo kwa sababu ulifanyika kipind kile kile!!

Lakini KUBWA ZAIDI, plan ya Bandari ya Bagamoyo sio kuifanya kuwa competitor wa bandari zingine! Bandari ya Bagamoyo iliandaliwa strategies zingine kabisa ili kuwa commercially viable, na miongoni mwa hizo strategies ni pamoja na:-

1. Kujenga Industrial City (Free Economic Zone) for export: Kwamba, endapo Industrial City ikiwa successful, kutakuwa na shehena kubwa ya bidhaa for export, na exportation ingefanyika kupitia Bagamoyo Port.

2. Transshipment Port:- Transshipment ports ni aina ya bandari zinazopokea mega ships ambazo haziwezi kutia nanga pale Dar es salaam! Kinachofanyika ni kwamba, Megaship X from China or Japan itashindilia shehena kubwa sana, mathalani zinazoelekea Afrika.

Kwavile meli ni kubwa sana, haitaweza kutia nanga popote kwenye ukanda huu bali Bagamoyo!! Sasa meli kutoka Msumbiji, Kenya, Djibout, na hata Kusini na Magharibi mwa Afrika, zingekuwa zinafuata mizigo yao Bagamoyo badala ya kwenda moja kwa moja China!!

Na hata sasa ndicho kinachofanyika!

Meli nyingi unazoona hata kama zina mzigo kutoka China haina maana zimeenda kubeba mzigo moja kwa moja kutoka China bali mara nyingi mega ships zinachukua mzigo kutoka China hadi Singapore, na hizi meli tunazoona huku, zinaenda kuchukulia mzigo Singapore au bandari nyingine yoyote inayotumika kama transshipment port!
Kwa kuwa Mh Raisi hayati Magufuli, alidokeza kuwa, baada ya mradi kukamilika kujengwa kwake, TRA na mamlaka zote za napato nchini, hazitaruhusiwa kutia miguu katika bandari hiyo
Nasema hivi: SIO KWELI!!

Duniani KOTE kodi ni mali ya serikali. Mchina anachoweza kufanya ni kuomba msamaha wa kodi ya mapato, na incentives zingine!!

Yaani, assume wewe binafsi unapitisha mzigo wako pale Bagamoyo! Kitakachotokea ni kwamba, kodi kama import na VAT lazima ziende serikalini!!!

Sasa kwavile Mchina anatoa huduma zake hapo bandarini, kama vile kupakia na kupakua mizigo, ku-handle meli, na pia kuhifadhi mizigo, na mambo mengine, yeye atalipwa na wateja kutokana na hizo huduma!

Anacholipwa ni MAPATO, ambayo under normal conditions, atatakiwa alipe Income Tax!!

Sasa kwa kawaida, Mchina huwa anaomba kusamehewa hii income tax.

Ngoja nikuulize jambo moja!! Assume wewe umenunua eneo lote Kariakoo kwa pesa yako mwenyewe! Ukavunja majengo yote, kisha ukawekeza biashara zako mwenyewe! Hadi unafungua biashara yako, serikali haijakupa hata senti 5!! Je, hiyo itawafanya TRA wasije kuchukuwa kodi yao kutoka kwako?

ANYWAY, labda niseme jambo moja!! Kwa baadhi ya nchi, inapotokea situation kama Bandari ya Bagamoyo, kwamba mjenzi kajenga kwa pesa yake, na anapewa muda wa kuiendesha, linapokuja suala la ukusanyaji kodi, wanaweza kukubaliana kwamba existing government institution( kama vile TRA) iendelee na kazi yake ya kukusanya kodi hapo, au wanaweza kukubaliana kuanzisha agency itakayokusanya kodi eneo husika!! Kodi hii ikikusanywa, ya serikali, itaenda serikalini!

HOWEVER, kwavile uzoefu unaonesha Wachina (in fact, wawekezaji WOTE, na sio Wachina pekee) huwa na tabia ya kuomba favor hii na ile, kwa mfano kusamehemewa kodi fulani fulani, basi hiyo nayo ndo maada niliyoiweka kipolo kujadili, kwamba tunaweza kusamehe nini, na kugoma kusamehe nini hadi tufikie kwenye win-win state!!!
Lakini pia, hilujaweza kabisa kuainisha ukaribu wa bandari iliyopo Posta na itayojengwa hapo mbegani Bagamoyo kwamba, madhara yake ni yepi,
Jibu lipo kwenye hayo maelezo hapo juu, lakini ni suala linalohitaji thread inayojitegemea!!
Kwa nini hujashauri kwamba, Kwa kuwa nchi yetu tunaeneno kubwa la mwambao wa bahari, ni vyema bandari hii inayotaka kujengwa Bagamoyo ikenda kujengwa angalau hata Saadani kule, ni mfano huo
Hili linahitaji technical argument, jambo ambalo siwezi kuwa na uwezo nalo! Hata hivyo, as far as I know, kabla watu hawajafikia maamuzi ya wapi kujenga, walituma wataalamu wao kwanza!!! Wachina sio Wajinga watoe favor Bagamoyo kwa sababu tu kwa JK wakati favorable conditions zote zipo Saadan!!
Ukaribu wa Bandari hizi kati ya Dar na Bagsmoyo, ni kama kilomita zisizozidi 60 hivi, hauoni ni njia ya kuiuwa bandari yetu ya Dar?
Jibu nimeshatoa hapo juu, hizi hazikusudiwi kuwa competing ports!! Lakini hata kama zinakuwa competing ports, kwani tatizo lipo wapi?! Kwanini tunaamini itakayokuja kufa ni Bandari ya Dar na isife Bandari ya "Mchina"? Kwanini Watendaji wa Bandari ya Dar wasifanye kazi bora maradufu ili hatimae Shippers wapendelee Bandari ya Dar badala ya Bagamoyo?!!

Tena ngoja ni kuambie!! Tanzania na nchi ZOTE, again, NCHI ZOTE zinazotumia Bandari ya Dar ni nchi maskini kweli kweli! Nchi kuwa maskini kweli kweli maana yake hata imports na exports za nchi hizo ni ndogo kweli kweli!

Lakini pamoja na umaskini huo, pamoja na kuwa na imports and exports ndogo kweli kweli, lakini eti inafikia wakati Bandari ya Dar es salaam inaelemewa!!! Hivi shehena gani inayopitia Dar hadi ifanye wakati mwingine bandari ielemewe?!

Ninachotaka kusema ni kwambani umaskini wetu wa kutupwa ndio unaotufanya tuamini Bandari ya Dar inatosha, kiasi kwamba ikija nyingine basi tunaamini Bandari ya Dar itakosa mzigo!

But am telling you, ingawaje Afrika Kusini na yenyewe ni maskini tu, lakini ikitokea uchumi wa nchi mbili TU kati ya zile zinazotumia Dar zikawa na uchumi angalau nusu ya uchumi wa Afrika Kusini, trust me, hapo ndipo utakapokuja kugundua Bandari ya Dar si lolote si chochote!!!

Kenya na majirani zake pamoja na viuchumi vyao vile, lakini meli wanazopokea Mombasa ni karibu mara mbili ya tunazopokea Dar.

REMEMBER, kuna uhusiano wa karibu sana kati ya idadi ya meli inazofunga kwenye bandari x (tofauti na transshipment ports), na uchumi wa nchi unazotumia bandari husika!!!
 
Kwa hiyo mlishausaini tayari siyo?
Hapo kwenye bold, ni akina nani?! Nilichotaka kusema hapo ni kwamba kilichokuwepo hadi JK anaondoka ni framework agreement.

Framework agreement sio mkataba, na ndo maana huwezi kusikia serikali imevunja mkataba bali utaendelea kusikia serikali bado hawajakubaliana na Mchina, kwa sababu ndo hasa inavyokuwa inaposainiwa framework agreement!

Na ile framework agreement ilipewa mwaka mmoja... which means, endapo baada ya huo mwaka pande zote wangekubaliana na hiyo framework, ndipo mkataba ungesainiwa!!

And as far as I know, it's just an initial framework agreement. Rejea majadiliano ya makinikia kama ulifuatilia kwa ukaribu uone framework agreement ilisainiwa wakati gani na mkataba ulisainiwa wakati gani
 
Kuna watu wanafikiria kwamba hatuwezi kuishi na kufanya maendeleo single-handed bila kumtegemea mzungu au mchina.......hizi ni akili za kiswahilina na huwezi shangaa aina ya watu walioasisi na wanaoendelea kuupigia debe huu mradi wa kingese....
 
Naona kama Rais mwanamke amepata akili kuliko wa-tz wote! Hii ndo hali ya kawaida kwa viongozi wa kiafrika. Wakipata madaraka tu, wanaamini wana akili kuliko wengine wote, hata ktk hali ya Rais wetu anayefahamu wazi ana urais wa urithi.

Rais anaelekea kujifanya kuwa ni Rais wa mageuzi ktk kila kitu, hata mambo ambayo yana mifano mibovu kwa nchi zingine. Badala ya kuanzisha miradi na mipango mizuri ya kwake, yeye amekuwa ni mtu wa kufufua yaliyokataliwa na taifa hili. Tunakubali bandari, mkataba ni upi?
Lini mtajifunza kupunguza unafiki wenu na kujitia kulia lia machozi ya mamba,labda niwahoji swali dogo: hivi miradi yote mikubwa nchini iliyo anzishwa awamu ya tano na JPM kuna mradi gani Magufuli aliwahi kuuweka adharani akawaomba wananchi waujadiri na kutoa maoni yao - lini? Chukulia mfano wa ovyo kabisa unao husu Mradi wa Ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa kijijini mwake,je,aliwahi kuomba maoni ya Watanzania kabla hajaujenga?

Kama majibu ni hapana, kwa nini Watanzania hatujiulizi kwa nini Magufuli na like mind wenzake walilivalia njuga suala la mradi wa Bagamoyo ili upigwe chini - it was a well organised crusade wenye lengo laku-demonize Wachina, anarudia rudia propaganda zile zile za mataifa ya magharibi kuhusu ujio na uwekezaji wa Wachina barani Afrika - Magufuli alikazania kuzumgumzia vipengere vya mkataba ambavyo anavichukulia ni kandamizi, lakini Magufuli huyo huyo hawaelezi Wananchi kwa nini Wachina waliweka masharti hayo - kazi ilikuwa ni lawama mwanzo mwisho!! Crusade ya Magufuli na wenzake na Govt media kuhusu mradi wa Bagamoyo ilifanikiwa kuwazuga Wananchi kwa kuwageuzia kibao Wachina ili waonekane wana lengo la kufirisi Taifa letu kwa kutuibia kila kitu - lakini ukichunguza kwa umakini utagunduwa kwamba kumbe tuhuma nyingi kuhusu mradi huu ni za uongo na ulaghai mtupu - ukweli was mambo Wachina hawana lengo baya kwa Taifa letu wanacho taka wao ni kuwa na uhakika kwamba fedha zao wanazo wekeza kwenye mradi wa ujenzi wa Badari ziweze kurudishwa ndani ya muda walio jiwekea including profit.

Baadhi ya Watanzania tulivyo wa ajabu na ukosefu wa msimamo, hakuna aliye kuwa na ujasiri wa kumu-confront Magufuli na kumu hoji iweje leo useme vibaya mradi wa Bagamoyo wakati yeye alikuwa ni member wa Cabinet ya Jakaya Kikwete wakati mradi huo unapitishwa - mbona alikaa kimya? Je,Magufuli alitaka kuileza Dunia kwamba Jakaya alikurupuka tu hakuwa na Washauri wabobezi kwenye Mega projects kama za ujenzi wa modern Ports au? Magufuli hakuwaeleza wananchi kwamba mradi mzima ni wa uwekezaji na sio kwamba Wachina wange ingia ubia na Serikali ya Tanzania katika Ujenzi na uendeshaji wa Bandari ya Bagamoyo, Serikali haitachangia chochote kifedha na material katika ujenzi zaidi ya kuwakodisha aridhi basi, cha ajabu inaelekea Magufuli na akina Kakoko walitaka Bandari ikikamilika tu wakabidhiwe wao kuiendesha Wachina wawekwe pembeni - kwa maneno mengine wavune ambacho hawakupanda ili waendeleza mambo yao ya ndio sivyo ambayo tulikuwa tuna ya shuhudia TPA miaka nenda rudi - mwisho wa siku Wachina washindwe kurudisha gharama zao za ujenzi/uwekezaji kwenye Bandari ya Bagamoyo - wafanyiwe umafia wa kuporwa Bandari walio ijenga kwa jasho na fedha zao wenyewe!!

Binafsi nampongeza sana Madam President kwa ku-revisit mradi huu wenye umuhimu wa kipekee kwa maendeleo mapana ya Taifa letu, mradi ukifufuliwa Tanzania itanufahika sana sio kwa Bandari tu bali na ujenzi wa Industrial Park kuzunguka Bandari yenyewe ambao uta generating ajira nyingi kwa vijana - katika ujenzi wa Bandari ya B'moyo Watanzania wote tumuunge mkono mama Samia, tusiwa ruhusu Watanzania wachache wanao kuwa driven na itikadi za vyama vya upinzani watake kukwanisha mradi mkubwa wenye manufaa kwa Taifa.
 
Kwa hiyo unaamini mradi wa Bagamoyo utatupeleka Mbinguni. Yaani Yesu akirudi atasimama Bagamoyo! Unavyoandika ni kama mtu bwege asiyejua kulinganisha miradi. Unawezaje kulinganisha mradi wa Bagamoyo, unaopangwa kuwa biashara ya umoja na wawekezaji na miradi ya kujenga barabara, kujenga airport, kujenga sgr, nk. miradi ambayo hatuna ubia na hatutegemei kugawana faida na mjenzi mwingine?
 
Barikiwa mkuu kwa hoja kuntu
 
Ndiyo mkuu, Mkataba upo lakini wenye utata, na mkataba wenye utataa..!, na waliousema unautata, sio sisi wananchi wa kawaida, ni viongozi wetu, ili kuthibitisha uwongo wa viongozi hawa...! basi uwekwe wazi, la sivyo sisi tunaita ni mkataba usiozingatia maslahi ya nchi!
Ni vyema tukajua, Matumaini ya mafanikio ya kitu chochote, ni kuzingatia sana ubora wa tenda na mkataba wake, kwa hiyo, ni vyema mikataba yetu iwe inapitiwa na bunge tena kwa uwazi na kisha kwenye chama cha wanasheria kwa mapitio mengine ya kisheria zaidi
 
Mkataba huu usiposomwa waziwazi, Basi nchi yetu kwenye kipengele cha katiba, ni mhimu itamke haya mambo, Hii nchi ni yetu sote
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom