Mradi wa Bagamoyo na Mundelezo wa kundi la "CCM" kuendelea kuila nchi kwa mrija

winnerian

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
334
530
Ikumbuke kwamba mambo mengi yanayopitishwa na bunge au kwa lugha raisi "kikundi laghai cha CCM" yanapita kwa njia moja kuu. Njia hii ni kuwahonga mabilioni ya pesa wabunge, individually yaani mmoja mmoja, na hatimae wote wanakuwa kitu kimoja. Wakishakuwa kitu kimoja wanaanza kuimba wimbo mmoja kwa sauti kubwa na ule wimbo unaonekana kuwa halali kwa nchi ilihali wanaenda kutumbukiza nchi katika shimo refu tulisiloweza kutoka hata tufanyaje.

Tumeliona hili toka kipindi cha Kikwete kwenye mkataba wa gesi na kudhihirishiwa na kauli za aliefuata baada yake; hayati John Pombe Magufuli, kwamba "kwenye gesi tumepigwa, na siwezi kufufua makaburi". Na mpaka leo hii kwenye gesi tumebaki wapigwaji na kikundi kile kile laghai cha CCM. Mikataba ya madini pia ilifanyika hivi tukabaki tumepigwa. Mradi wa trillions kutoa billion kwa kila mbunge au kwa wale vinara sio issue sana.

Sasa wimbo anauanzisha Spika wa bunge Ayubu Ndugai pamoja na kamati zake laghai kwenye wimbo wa bandari ya bagamoyo natahadharisha tu kwamba kuna hela ndefu inayoenda kupigwa na wabunge wote waliopo bungeni ukijumlisha na wale watoto wa kambo na baada ya hapo ni kupitisha kila kitu kuwaachia wachina waje kukututawala na kuvuna mavuno katika shamba la bibi. Tanzania bado itabiki shamba la bibi bila kuwa na mfumo wa bora wa utawala unawazuia watu wenye uwezo mdogo wa fikira kuwaongoza wengi.

Pengine deni la nchi limekuwa kubwa sana na halivumiliki tena hivyo wanataka kutafuta mahali pa kupunguzia uzito kwa kuuza kipande cha nchi chenye maslahi kwa Taifa. Magufuli alikopa kwa speed ya mwanga kila mtu analijiua hilo na kusababisha deni la nje la taifa kukua kwa kasi kama mchicha wa kizungu. Sasa wakati mnapofikiria kuuza nchi tambueni kwamba hata ninyi mtakufa na mtaacha mali zote zikiliwa na kufaidisha wale wote wenye hualali nazo.

Ni hisia zangu zinazotokana na yaliyotokea mubashara kipindi cha nyuma na hata cha mbele.
 
Ipo siku nawahakikishia mtanikumbuka, na ninajua mtanikumbuka kwa mazuri na sio mabaya maana nimesakirifaizi maisha yangu kwa ajili ya Watanzania masikini.
 
Back
Top Bottom