Mradi uliofungwa jana, USAID SCMS na DELIVER uliajiri wafanyakazi zaidi 140 wakiwemo wanachama-PPF

mxyo16

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
1,243
758
Ndugu wadau, huu mradi wa usambazaji wa dawa na uhifadhi uliodhaminiwa na USAID, na kufanya kazi kubwa sana kwa ushirikiano na wizara ya afya, MSD, TFDA, MUHAS, nk....kujenga uwezo wa wafanyakazi, kuboresha miundo mbinu na mifumo kuwa ya kisasa katika sekta yetu ya afya Tanzania nzima bara na visiwani.

Katika maisha ya huu mradi waliajiriwa karibu wafanyakazi 150, kwa mikataba. kwahiyo kwa kufungwa huu mradi jana wengi wa hawa wazalendo watakua hawana kazi, wengi wao ni umri kati ya 30-50 na wamelipa kodi vizuri tu (PAYE) kwa miaka yote hiyo na kuchangia katika mifuko ya NSSF na PPF.

Kwakazi waliyo kuwa nayo kubwa na kufanya kazi chini ya miradi ya USAID sidhani kama hata walikua na nafasi ya kujijenga maisha yao binafsi. katika miradi hii mingi hakuna uzembe wa kukwepa majukumu...kazi ni masaa zaidi ya 40 kwa wiki na mafanikio yanaonekana. KUTOKANA NA STRICT POLICIES ZA MRADI, RULES NA PROCEDURES ZA DONNOR...

Kwa jinsi yoyote hawa ni wazalendo na mashujaa kama walivyo mashujaa wengine wale wanao fanya kazi za kimkataba kama wafanyao kwenye machimbo ya madini.

Kati ya hawa 150, sio wote watakao pata kazi hapa karibuni kwa jinsi hali ilivyo halisi hapa Tanzania....

MIFUKO YA HIFADHI MNAWASAIDIAJE MASHUJAA WETU HAWA kwa mchango wao miaka 10 katika sector ya afya.....

Muwape mafao wakaanzishe miradi na kutoa ajira mashambani na viwandani......Bank zetu hazitoi mikopo kwa start ups, wanatoa kwa wale waliokuwa tayari wameanzisha miradi...na hii ndio fursa kwa hawa 150 kuanzisha miradi...Naomba kuwakilisha.

CC Mheshimiwa Rais DR. JPM
CC WAKURUGENZI MIFUKO YA NSSF NA PPF
CC Waheshimiwa wabunge
CC WADAU WOTE
 
Back
Top Bottom