Elections 2010 Mr. Sugu ashinda kura za maoni ubunge CHADEMA - Mbeya mjini

Teh Teh Teh

Member
Nov 13, 2009
41
9
Joseph Mbilinyi, Mr. Sugu, maarufu kwa jina hilo, ukipenda Mr.II. Ameshinda katika kura za maoni yaliyofanyika Mbeya Mjini za CHADEMA za kumtafuta Mgombea wa Ubunge kwa tiketi ya CHADEMA.

Ameibuka kwa kupata kura 175 akifatwa na Mponzi aliyepata kura 125 huku Gwakisa akiachwa mbali kwa kura 6.

Jana Jiji la Mbeya lilirindima kwa furaha kubwa hali iliyotafsiriwa kuwa ni ushindi kwa CHADEMA.

CCM ina hali ngumu leo kuweza kumchagua ni nani ambaye anaweza kuchukua Jimbo hilo, ambalo tayari CHADEMA -Mbeya wametupa karata yao vizuri.

Mr. Sugu amefungua ukurasa mpya lwa kuweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza maarufu kugombea Ubunge kupitia CHADEMA.

Hongera sana Mr. Sugu.
Hongereni CHADEMA.
 
Safi sana It is time for change lads dunia haikuumbwa imenyooka imeumbwa duara
 
At least mtu kama huyu akisema anataka kwenda ku fight status quo mtu unaweza kuamini.
 
Kituko.
Suala la uadilifu na umakini ndani ya CHADEMA halina mjadala. Mr. Sugu ni mtu makini, mwenye upeo. ni mzaliwa wa Mbeya, amekulia Mbeya. Nyumba yao ipo Mbeya. Ana uwezo mkubwa wa kujenga hoja. suala la uwezo wa Mr, Sugu halina mjadala.
 
Whichever kwani Komba na Hadja Kopo walichaguliwa kivipi si kwa kukata viuno.

Two wrongs do not make a right, kama kuna watu walichaguliwa kwa kukata viuno hili halihalalishi wengine wachaguliwe kwa kukata viuno.

Not to say kwamba Sugu ni mkata viuno, au hana uwezo, lakini swali la kuulizia uwezo wake ni legit na linahitaji a thorough examination.
 
Wapiga kura wake ndio wanaomjua uwezo wake ndio maana wamamchagua wewe kinakuwasha nini.
 
Wapiga kura wake ndio wanaomjua uwezo wake ndio maana wamamchagua wewe kinakuwasha nini.

Si kweli kwamba wapiga kura wake tu ndio wanaomjua uwezo wake. Kuna watu wamefanya naye kazi, wamerekodi naye studio, wameishi naye etc.

Ingawa ni kweli kwamba wapiga kura wake tu - wakazi wa jimbo lake wenye sifa za kupiga kura- ndio watakaokuwa na nafasi ya kumpigia kura,si kweli kwamba ni wao tu ndio wana haki ya kumchambua. Ingekuwa hivyo magazeti ya Dar yenye waandishi na wsomaji waishio Dar yasingechambua chaguzi za majimbo ya mikoani na uongozi wa mikoani.

Usitake ku force king, hapa ni JF, kila mtu anajadiliwa, na kuna mapanga fulani, kama hili la Kiranga, hayana mfungamano na upande wowote.

Kama Mr II ana uwezo semeni uwezo wake hapa, kusema wapiga kura wake tu ndio wana haki ya kusema ni kuonyesha huna la kusema.

Unajuaje kama mimi si mpiga kura wake? Unajuaje kama hapa hamna wapiga kura wa jimbo lake ?
 
Wapiga kura wake ndio wanaomjua uwezo wake ndio maana wamamchagua wewe kinakuwasha nini.

sio vibaya tuki-share kwani ataenda kuwakilisha wananchi wote si wakazi wa mbeya mjini tu..............
 
Hongera Mr II, nakutakia safari njema katika siasa za Tanzania. Naimani mapambano yanaendelea, na hiyo ni ishara tosha kabisa kuwa mwaka huu siyo kawaida. "kaa chini wewe, nikae vipi nimesimama" dah nakumbuka enzi hizo!!
 
Jamani Mbeya msituangushe jimbo lende kwa upinzani hilo...kila la kheri wapinzani wote.
 
Ni akina wale wale tu........Hana tofauti na Ms Banji! Kawatukana watu matusi ya nguoni kisha tumfurahua! Ningesikitika kupata mbunge asiye na morals Kama huyo
 
Two wrongs do not make a right, kama kuna watu walichaguliwa kwa kukata viuno hili halihalalishi wengine wachaguliwe kwa kukata viuno.

Not to say kwamba Sugu ni mkata viuno, au hana uwezo, lakini swali la kuulizia uwezo wake ni legit na linahitaji a thorough examination.
kamanda, sugu is more than mwimbaji.. he has insight na he is strategic, take it from me

he may not have all teh paperworks we usually value, but he is a right person especially now we are in transition phase
 
Mbona hii habari imewekwa kwenye jukwaa hili ni utani au ni kweli........!!!!
 
Back
Top Bottom