Mr. President ukifanya haya tu tutakukumbuka kwa miongo mingi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mr. President ukifanya haya tu tutakukumbuka kwa miongo mingi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mundali, Nov 28, 2011.

 1. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #1
  Nov 28, 2011
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Mheshimiwa Rais JK, ni miaka takribani sita sasa toka ulipoanza kutuongoza. Watu wako wanalia maisha magumu kila uchao. Mfumuko wa bei unaziji kupaa na migogoro haiishi. Sidhani kama ushauri wangu utauzingatia, lakini japo jaribu mojawapo katika haya.

  1. KODI.
  Hii ni roho ya Serikali yoyote duniani. Serikali yako haikusanyi kodi walau kufikia nusu ya kodi inavyostahili. Wekeza katika makusanyo ya kodi mbalimbali, kuanzia zile za serikali kuu hadi serikali za mitaa. Mosi safisha uoza kwa kuondoa wakusanya kodi wasio waaminifu na wala rushwa. Pili tengeneza data base ya wananchi wote, ili kila mtanzania ajulikane alipo na anachofanya. Tatu, unganisha mifumo yote ya fedha nchini kama vile mabenki, makampuni ya simu na kadhalika kwa ajili ya utambuzi wa transactions mbalimbali, kama deposits, withdrawals, money transfers n.k utajua walau mzunguko wa matrilioni ya mapesa kati ya watu wako kila siku. Hii matajiri hawataipenda lakini ndio njia nzuri ya kuzijua biashara za kujificha za raia wako. Inasikitisha sana mfanyabiashara mwenye uwezo wa kukodi frem moja kwa sh. 1,000,000/- kariakoo analipa kodi ya mapato sh. 95,000/- kwa mwaka!!!!!!!! Nchi inapoteza kodi kubwa sana pia kwa wafanyabiashara wakubwa. Ukifanya haya hakika ni baada ya mwaka mmoja tu hutaruka tena mamtoni kusaka misaada.
  2. SIMAMIA UWAJIBIKAJI
  Katika ziara zako kwenye mawizara kuna jambo moja hukuliona, nalo ni uwajibikaji. Wafanyakazi hususani wa sekta za umma wamekuwa hawawajibiki kwa kiwango cha kutisha na wamekuwa ni mahodari wa kutupia lawama wengine. Ratiba za kazi kwa wengi wao ziko hivi, anafika kazini na kusaini daftari la mahudhurio, saa 1.30 asubuhi, anapita kusalimia ofisi za wenzake mpaka saa 2.00 asubuhi, wanaanza story za matukio yaliyopita mpaka saa 3.00, anarudi mezani kwake mpaka saa 4.00 anaenda kunywa chai, anarudi kama akiwahi saa 5.00. Anapitia mafaili mawili kisha anaaga anakwenda site, huyo ndo harudi mpaka kesho. Mchana kutwa yuko kuchonga madili. kwa haki katika muda wa masaa nane ya kazi ni masaa mawili tu yanatumika kwa tija, hapo hatujaondoa siku za kuugua, kufiwa, kuuguza, sherehe n.k. tu masikini kwa sababu hatufanyi kazi.
  Ili kufanikiwa kutokomeza uoza huu ni lazima tufanye kazi tena kwa juhudi na maarifa. Ni lazima kuwepo na mipango kazi, taarifa za utekelezaji wa kila kazi kila siku. Na reward ama adhabu iwe ni jambo la lazima. Wajerumani wanatumia "Carrot and Stick", wajapani wana management system iitwayo Gemba Kaizen, nakushauri utumie katika serikali yako kupunguza "MUDA i.e west".
  3. TOKOMEZA RUSHWA
  Rushwa imeshamiri kwa kiasi cha kutisha, sasa ni kila mahali mpaka kwenye vyombo vya kidini. Rushwa hatari zaidi kwa afya imefikia kuwa ni maisha ya kawaida kwa sasa, yaani rushwa ya ngono. Hili unalijua sana labda hufahamu ni kwa vipi upambane nalo. Mosi badili mfumo wa kiutawala na kisheria wa TAKUKURU, isiwe chini ya ofisi yako bali iwajibike kwa bunge. Safisha wala rushwa ndani ya chombo hicho. TAKUKURU imekuwa ni bunduki ya mawindo ya madili ya fedha. Wenye pesa hawaguswi na chombo hiki. Mfano ni ubadhilifu unaofanyika katika halmashauri mbalimbali nchini kiasi kwamba miradi mingi ya maendeleo inafisadiwa wakati TAKUKURU wamezagaa kila mahali. Wanagawana return kisha wanajiachia tu mambo yajiendee kama yalivyo.
  Usalama wa taifa ndo wamelala kabisa kama ndugu zao polisi. Watu wanadiriki hata kufanya biashara ya wahamiaji haramu, na polisi wanatoa ulinzi. Wastaafishe wakuu wa vyombo hivyo, wateue wale waadilifu watakaoleta tija na kusafisha vyombo vyao hivyo.

  Mheshimiwa rais ukiweza timiza hayo, utashangaa mabadiliko ya kiuchumi yatakavyotokea.
  Wasalaam.
   
Loading...