Mr. President Kindly Surprise Me!

Mwataka kurudisha ardhi, maeneo ya migodi na viwanja vya wazi sawa tu!
Je hapatikani mtu wa kurudisha fedha zetu zilizo nje ya nchi kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu. Badala ya kukimbizana na kuwa omba omba, nawashangaa tu! JK atupe mtu wa aina hiyo, si watu wa kufukia mashimo tu,muda wao uishe bora liende.
 
Kumbe Prof A Tibaijuka kapotea ramani maana swala la integrity ni history fulani hivi kwa JK na sisiem. CHADEMA wanazungumzia uadilifu, hiyo ni bora maana ukombozi wetu si serikari ya mafisadi bila mipango ya kukomboa mwananchi wa kawaida. Bali ni matumizi mazuri ya lasilimali zetu bila wizi na dhuluma kwa urithi wetu wa asili hasa madini. The resources for our development.
 
Huyu mama Tibaijuka kaifanyia nini Tanzania. Tuna ushahidi wa miradi aliyopeleka Kenya, ina maana watanzania tulikuwa hatuitaki?

Hoja haina mashiko hii; kwani Mama Tibaijuka alikuwa anamiliki UN? Wacha hizo !
 
Idiot. Ukitaka kufahamu mambo kwa undani rejea makala ya Jenerali Ulimwengu kaika gazeti la The East African wiki kadhaa zilizopita.

Mkuu Companero, kama kweli mheshimiwa rais anataka kutushangaza angeacha baadhi ya viti vya wizara muhimu wazi kwa muda na kuamua kusaka kwa udi na uvumba mabadiliko ya katiba ambayo yatafuta ulazima wa mawaziri kuwa wabunge. Kazi ya waziri ni bora ikafanywa na watu wasio na kofia ya ubunge ili kuwapa muda zaidi kuwekeza juhudi katika kazi za wizara husika na kuepuka mgongano wa maslahi.

Ila akishindwa hayo, basi ateue wataalamu kuwa wabunge na kisha awape uwaziri katika maeneo nyeti.

Kingine, rekodi ya Magufuli wizara ya ardhi na ya ile ya Ujenzi kabla ya hapo siyo nzuri. Yeye anaPR nzuri tu inayomfanya aonenake mchapakazi ila alivyokuwa Ujenzi waliacha madeni mengi tu kwa papara zake na hata ardhi sakata la mauzo ya nyumba za serikali na utwaaji wa viwanja vya watu bado hayajapatiwa ufumbuzi.

Prof. Tibaijuka ajira yake UN-Habitat iliishaje?

Kuna mawaziri wengine wa zamani bomu tu ambao Mh. Kikwete angefaa awapige chini kuanzia akina Mkullo, Membe, Ngeleja, Ghasia, Simba, pamoja na manaibu na makatibu wakuu lukuki

Great! Candid to your nation! Nimefurahi kukusoma, maana kuna watu wengi tunadanganyika na kauli nzuri! Hata Lowasa alikuwa anafuatilia vizuri na kuhimiza maendeleo, kama vile Mrema na Magufuli walivyokuwa wanafanya. Lakini kwa matokeo tofauti. Wote watatu ni wachapa kazi kikweli kweli. Ulimbikizaji binafsi unawatofautisha. Kinachowaunganisha ni kuvuruga kanuni na sheria na kutowatendea haki wale ambao mali zao zinakuwa njiani - yaani any obstructions zinavunjwa tu! Hivi ndivyo Magufuli alimvunjia yule Mhindi pale Mwanza na baadae kumwezesha kuvuna fidia kubwa ya mamilioni. Hivyo ndivyo alivyoweza kulazimisha barabara ya lami kwake, na sitaki niendelee.

Prof Tibaijuka amebobea katika maswala ya Human Settlements yaani, ardhi, majumba, maendeleo ya miji na uchumi wa miji. Huyu ndiye tegemeo la kufufua Wizara ya Ardhi. Huyu ataweza kurekebisha mipango yetu ya ukuuaji wa miji, ataleta tunu zile alizozilea kule UN-Habitat, hata yale matumaini aliyotupandikisha Raisi aliyeporwa Slaa juu ya nyumba za bei nafuu, yatafufuliwa na huyu Mama. Soma maandiko yake ni mengi, ndipo utaamini tunu gani tuliyo nayo sisi watz. Lakini ninasita kama atapewa hio kazi. Sioni katika jina lake, sioni katika maono ya Mh na wala watendaji wake kwamba watampa. Huyu anafuata taratibu kuliko wale watatu nilowataja.
 
Minister for Economic Upgrading. Prof. Anna Kajumulo Tibaijuka
Minister for Constitutional Changes: Dr. Harrison Mwakyembe
Minister for Land Reclaiming: John Pombe Magufuli (PhD)

mbona mnapenda kuumiza vichwa vyenu, napenda kuwahakikishia kuwa kutakuwa hakuna la ajabu katika baraza la kikwete...pamoja ameshinda kwa kuchakachua, angerudisha imani ya wananchi kama angewachagua Ole sendeka kuwa waziri mkuu na Mwakyembe kuwa waziri serikali za mitaa bila kumsahau Magufuli kuwa miundombinu na Anna Tibaijuka ardhi na maendeleo ya makazi. otherwise sioni kama kuna hata mmojawapo atawapa. Otherwise, sina imani kabisa kuona marekebisho yoyote ya msingi.. nina uhakika Kapuya, Mohamed Khatibu na Kawambwa wanarudi barazani!!!! bila kumsahau Mkullo kuwa waziri wa fedha!!
 
Zakumi...usirudi moja kwa moja. Beba boksi kwanza ilhali bado kijana. Mimi niko bongo sasa hivi na hakuna mpango. Mavumbi, pollution, mbu, harufu mbaya ya takataka na vikwapa, makororongo, na adha nyinginezo ambazo binadamu hastahili kuzi experience ndizo zinazotawala. Hakuna cha bongo Nyu Yoki wala nini.

Kama unapiga boksi lako Target...wewe endelea nalo tu. Ukipata tax return unarudi bongo kusalimia halafu huyo unasepa.

Hayo ndio umeyanusa na kuyaona Udasa Club na Samaki Samaki unapovinjari kwa sana?
 
I beg to differ, huyu ndio alihakikisha zoezi la kuuza nyumba za serikali linafanikiwa, sasa leo ndio anaweza to reclaime.

Walimn'goa meno maana ilikuwa ni kipindi cha kuelekea uchaguzi ila nia, uwezo na nguvu za ku-reclaim bado anazo!
 
Back
Top Bottom