Uchaguzi 2020 Mr. Much know na Kachero waamsha wenge upinzani: Vurugu zimeanza tayari

Kama Ni kweli, kwanini cheamani asiingie mzigoni mwenyewe ili apate hao wabunge 20? Mbona 2015 asilimia kubwa aliongea yeye na siyo White hair?
Kuna mista no makila kitu ndio kwasasa amekuwa nahodha. Yan anawavuruga mbaya kwa kigezo kuwa hana chakupoteza.

Aliyenipa mtonyo huu anasema wazee wanahaha kurekebisha mahusiano
 
Kabisa kaka. Tuangalie mechi Ila naona tinu pinzani imeshafungwa goli 4 kipindi hiki cha kwanza. Sijui watakuja na maajavu kama ya Man U ya Fergie kipindi hiki cha pili?

Halafu hata boli pozisheni wamezidiwa Sana halafu Wana majeruhi kibao.

Ila utawasikia, ooh refa kapendelea, ooh uwanja una mashimo Yan hawaishiwi hawa
Mwanzoni nilidhani unaweza kuwa unaaminika. Baada ya kusoma hapa, lol, kumbe imetoka kwa mbogamboga!!
 
Navuta taswira kuangalia mtifuano utakaotokea pale cheamani atapotaka kujilipa kibabe (kama ilivyo kawaida yake) ruzuku kiduchu watakayopata mwakani. Things'll never be the same after 28/10.
Umenikumbusha wale wadada wa kiingereza walioimba "things will never be the same again"
 
78EF5B9A-8494-40D5-BC90-D8D8A87C76F3.png
 
So BM alitaka Lissu na team yake wahamie kwake? Basi wakubaliane tu kwamba Uchaguzi huu wa 2020 yeye BM ampe support Lissu alafu ule mwingine wa 2025 Lissu nae ampe support BM just simple ni maelewano wote wapinzan.
 
Acha UZUSHI ZWAZWA wewe!

Wanabodi,

Tujiandae kusikia chochote kutoka kwenye viunga vya siasa za Upinzani. Bundi ametua kwenye mti wa mzambarau halafu akaruka na kwenda kutua mti wa msumbawanga (taja kabila).

Kule kwenye mti wa mzambarau, kachero hashikiki hatamaniki. Unaambiwa amevimba Kama koboko. Kasema Kama mbwai na iwe mbwai yeye ndie mpeperusha fulagi. Nyepesi anahahasa kutaka suluhu ila kachero hataki kusikia ukizingatia keshaingiza pensheni yake huko kununua mbolea na viatilifu vingine vya kuukuza mti wa mzambarau.

Kule kwenye mti wa msumbawanga, unaambiwa Mr. Know Ol hafuati maelekezo Wala utaratibu. Amesema yeye ni alwatan almaarufu. Yeye ndio kajiweka juu ya kila kitu na ndio maana inasemekana cheamani na KM wamesusa kimtindo. Mr No Everithingi anaonekana kuwa mzoefu wa mapambano ya kipontio Pilato ila n mwepesi mithili ya unyoya wa kuku yanapokuka masuala ya kikaisari. Cheamani alisikika akisema "mwaka huu Kama nitapata wabunge 20 itakuwa muujiza".

Haya jogoo ameshawika, upande wa pili wazee wa mchicha, matembele, sukumawiki na spinachi nasikia mambo yao kwatu. Wanateleza Kama wako kwenye mgongo wa ngisi. Sasa hivi wamekodisha mwewe wanampanda na amewaongezea umaarufu.

Tusubiri
 
Sina hakika. Huyu Machi No n kuwa yeye anawakrashi wenzake na kujiona anajua vyote na kuwa yeye n maarufu zaidi ya msumbawanga. Sidhani Kama umachi noo wake umepelekea kudhulumu uhai
Ndio yule kiongozi wa malaika mbinguni?
 
Wanabodi,

Tujiandae kusikia chochote kutoka kwenye viunga vya siasa za Upinzani. Bundi ametua kwenye mti wa mzambarau halafu akaruka na kwenda kutua mti wa msumbawanga (taja kabila).

Kule kwenye mti wa mzambarau, kachero hashikiki hatamaniki. Unaambiwa amevimba Kama koboko. Kasema Kama mbwai na iwe mbwai yeye ndie mpeperusha fulagi. Nyepesi anahahasa kutaka suluhu ila kachero hataki kusikia ukizingatia keshaingiza pensheni yake huko kununua mbolea na viatilifu vingine vya kuukuza mti wa mzambarau.

Kule kwenye mti wa msumbawanga, unaambiwa Mr. Know Ol hafuati maelekezo Wala utaratibu. Amesema yeye ni alwatan almaarufu. Yeye ndio kajiweka juu ya kila kitu na ndio maana inasemekana cheamani na KM wamesusa kimtindo. Mr No Everithingi anaonekana kuwa mzoefu wa mapambano ya kipontio Pilato ila n mwepesi mithili ya unyoya wa kuku yanapokuka masuala ya kikaisari. Cheamani alisikika akisema "mwaka huu Kama nitapata wabunge 20 itakuwa muujiza".

Haya jogoo ameshawika, upande wa pili wazee wa mchicha, matembele, sukumawiki na spinachi nasikia mambo yao kwatu. Wanateleza Kama wako kwenye mgongo wa ngisi. Sasa hivi wamekodisha mwewe wanampanda na amewaongezea umaarufu.

Tusubiri
Eti "Mpeperusha fulagi"
 
Back
Top Bottom