Mr. Lukuvi - This is too much bwana! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mr. Lukuvi - This is too much bwana!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Katikomile, May 26, 2009.

 1. Katikomile

  Katikomile JF-Expert Member

  #1
  May 26, 2009
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 473
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Mkuu wa mkoa wa Dar, Mh. William Lukuvi ametoa tamko kwamba kuanzia mwaka kesho haitaruhusiwa mwanafunzi wa wilaya fulani kusoma shule iliyotofauti na shule zilizopo ndani ya wilaya aliyomo mwanafunzi husika!

  Kwa mazingira ya Dar es Salaam ambapo wakzi wengi ni wakuja na hivyo wapangaji ni wengi, leo Temeke, kesho Ilala keshokutwa Kinondoni kutegemeana na hali ya kodi ya pango. Does he need kumwamisha mtoto kila unapohamia new home?

  Je mkuu wa Wilaya ya Temeke anaishi Temeke kweli? Ilala je? na wakuu wote wa idara za serikali na taasisi ngazi ya wilaya na halmashauri wanaishi ndani ya wilaya zao kweli ama wote wamejibana ndani ya Kinondoni na kupelekea kodi kuwa juu sana ndani ya wilaya ya Kinondoni

  Nafikiri mkuu wa kaya yetu ya Dar anahisi bado yuko Dodoma ambapo ukiwa Bahi, wewe ni Bahi tu au ukiwa Chamwino basi wewe ni Chamwino tu!

  NI MTAZAMO TU LAKINI
   
 2. Katibukata

  Katibukata Senior Member

  #2
  May 26, 2009
  Joined: Dec 27, 2007
  Messages: 183
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nadhani hizi ni mbio za sakafuni! Na kama si mbio za sakafuni basi hajashauriwa vizuri. Sina nia ya kubeza utendaji wa mkuu huyu ila nadhani ni 'kasi mpya'.

  Natumai Mh. Lukuvi utabadilisha uamuzi wako vinginevyo itakuwa ngumu kutekelezeka.Sijui nia yako ni kuwasaidia wananchi wa kawaida wasio na magari ya kuwapeleka watoto wao shule au ni kupunguza msongamano wa magari mijini au ni huruma kwa wamliki wa daladala kwa kuwa wanafunzi wanalipa pesa kidogo??
   
 3. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #3
  May 26, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Huyu bwana kama walivyo wengi wa maswahiba wa Jakaya ana deficit ya elimu as a result anakurupuka tu na matamshi; mfano ni ule alipowataka watu wa Mbagara wazoee mlio wa mabomu kama wenzao wa kipawa walivyozoea ngurumo za ndege!! Matamshi ya huyu bwana ni maji ya moto hayachomi nyumba!! Haijui DSM ndio maana ana papala!!DSM sio Isimani mkuu!!
   
 4. Katikomile

  Katikomile JF-Expert Member

  #4
  May 26, 2009
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 473
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Inaonesha bado hajalielewa vizuri jiji kwani toka amekuja ni kupokea misaada ya mbagala.
   
 5. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #5
  May 26, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kama katoa habari hii, huwezi kuzishangaa hizi kauli za wanasiasa, ukiangalia profile yake haiwezi kukupa taabu kukubaliana na upeo wake wa kutathmini mambo. Huyu hana tofauti na kina Tambwe Hiza. Eti amekubwa Naibu/Waziri kwa zaidi ya miaka 10, halafu mnategemea Tanzania ibadilishwe na watu kama hawa!

  Badala ya kuweka mikakati ya kukabiliana na kukwama kwa mfumo wa usafiri Dar wanafikiria mambo ya kipuuzi kama haya. Basi nao waajiriwa wate wawe wanaishi sehemu ofisi zao zilipo!
   
 6. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #6
  May 26, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Tangu alivyochaguliwaga jamani nilisema hichi nacho ni kimeo kingine, ni top ten kati ya viongozi wanaowaza baada ya kuongea nchini
   
 7. Katikomile

  Katikomile JF-Expert Member

  #7
  May 26, 2009
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 473
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  IQ yake ikoje kwanza? Hivi ofisi ya mkuu wa mkoa haina washauri? nini kazi ya RAS?
   
 8. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #8
  May 26, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Jamani tumpe muda......maana najua atakuwa amekutana na kushauriana na wadau wote na watendaji wenzake kuhusiana na hili...tumpe muda tujue amejipangaje kwa hilo...........hapo ndio tutampa ugumu wake .....kwenye implementation.
   
 9. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #9
  May 26, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Jamaa anataka kustaafishwa kazi na umma kama Mapuri alivyostaafishwa siasa na wanahabari. Ni kati ya watu ambao kama ingetishwa kura ya kutokuwa na imani naye sasa hivi, angeibuka kidedea kuliko JK alivyoshinda 2005. Yetu macho, kama ikatokea mabadiliko yoyote ya Ma DC, yeye yumo out!
   
 10. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #10
  May 26, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Mkuu, binafsi wewe unataka kumpa muda kiasi gani?
   
 11. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #11
  May 26, 2009
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  tusiwahukumu viongozi sawa wakati wote...hata nyerere pamoja na kuungwa mkono kwa mengi kuna wakati alikuwa anaharibu...mimi ni katika wale wanaohoji uwezo wa huyu bwana kiutendaji...
  lakini kwahili la kuhakikisha wanafunzi wanasomea kwenye wilaya zao lina tija kiasi fulani, na kama ataweza kulisimamia itakuwa ni jambo zuri...kumbuka kila mtu alichangia ujenzi wa shule katika eneo/wilaya yake...lakini bado wizara imekuwa ikiwachagua wanafunzi kujiunga na shule zilizo nje ya wilaya wanazoishi...kuhusu suala usafiri Dar atakuwa amewasaidia sana watoto wetu ambao wanapata tabu sana na mnajua gharama za usafiri zinaendelea kupanda...suala muhimu hapa ni:
  -kuboresha mazingira ya shule zote za serikali ikiwa ni pamoja na mitaala na miundo mbinu, ili watoto waliosoma shule za masaki wakikutana na wale wa TMK au gongo la mboto wasitofautiane sana...kila mtu anapenda mtoto wake apate elimu nzuri...
  -walimu waboreshewe maslahi yao ili mwalimu akiambiwa akafundishe mbagala asione unyonge...
  -idadi ya shule iendane na idadi ya walimu...sio mbagala shule ina mwalimu mmoja wakati ilala walimu wapo waziada...

  nazani katika haya yamo yakuzingatia...wakati mwingine kumchukia mtu tuuuu hakusaidii kama aliyemuweka anampenda....yuko wapi Mataka...mtakuja kuwalaumu bure zeutamu kumba hoja mnawapa wenyewe....
   
 12. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #12
  May 26, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Waboreshe public transport, vinginevyo kila mtu atanunua gari. Ukiuliza mikakati ya muda mrefu ni yapi kuhusu usafirishaji jijini, wala hutoambulia kitu.
   
 13. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #13
  May 26, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hapa kuna kujitia ubize usiokuwapo. Watu wasiojua kufanya kazi wanataka kujipangia ubize ilimradi waonekane wanafanya kitu tu katika kutapatapa.

  Hivi katika priorities hii nayo ni priority?

  Anaweza kutuonyesha hili litasaidiaje taifa?

  Anaweza kutuhakikishia kwamba kuna uwiano mzuri wa wanafunzi waliopo katika kila wilaya na shule zilizopo katika wilaya hizo?

  Je vipi kuhusu dhana nzima ya kuwachanganya watanzania katika ku cement umoja wa kitaifa, kama wanafunzi wa wilaya moja tu watasoma katika wilaya yao hiyo hiyo haoni kuna hatari ya watu kuwa parochial na kutojichanganya?

  Kuna research gani iliyofanywa na pilot program gani iliyoendeshwa kuonyesha manufaa ya "ubunifu huu" kabla ya kuingia kichwa kichwa ?
   
 14. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #14
  May 26, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  1.Je hiyo sheria ni kwa wanafunzi wa shule za serikali tu au na private nayo lazima usome wilayani mwako? Hiyo haija wekwa wazi.

  2.Kama kuna shule bora zaidi kwa mwanangu wilaya nyingine kwa nini nimnyime haki ya elimu bora kwa kumweka shule ambayo haitampa kile ninacho kitaka kwa ajili ya mwanangu?

  3.Je huku kulazimisha mtoto kusoma wilaya moja na makazi yake ni kwa faida ya nani haswa? Je ni kwa wanafunzi, je wazazi au nani haswa?

  4.Jijini Dar wenye makazi permanent ni wachache. Wengi wetu tuna tegemea kupanga. Kwa maana hiyo mtu anakaa pale anapo ona unafuu, sasa ikibidi ahame wilaya dasi kila wakati na pia tabu tena ya kumu hamisha mtoto shule? Pia wengi hatuna usafiri kwa hiyo mtu unaweza kuhama hama kutokana na ajira yako na unafuu wa usafiri.
   
 15. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #15
  May 26, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  The creeping communist collectivism convalescing a cajoling contemporary conundrum.
   
 16. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #16
  May 26, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  chicanery cacophony cantenkerously cliche-isque camaraderie concocting coccoons.
   
 17. Robweme

  Robweme Senior Member

  #17
  May 26, 2009
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 178
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jamani,huyu jamaa katoka shambaaa au sio,lakini hata kama katoka shamba basi elimu yake ingemsaidia kujua tatizo nini kwanini watu wawe kinondoni mtoto asome ilala.Naomba ni mshauri."Wiliam, tatizo ni kwamba wakazi wengi wa Dar es Salaam wanaishi kwa kupanga nyumba.Hivyo kutegemea wapi ni rahisi kwa upande wa nyumba na usafiri basi mtu anaamua kukaa pale, lakini si kwamba kila atakapo hama basi aamishe na mtoto shule,mbona mtoto atasoma shule saba mpaka amalize darasa la saba.Kwahiyo, basi wiliam unataka kufanya maisha ya watu yawe magumu na uchaguzi unakaribia angalia usije ukamkwaza bosi wako uchaguzi ujao.Nadhani kwa ufupi wiliam umenipata,hakuna anayependa awe kinondoni mtoto asome mbagala, ni mipango ya mungu.:confused:
   
 18. F

  Froida JF-Expert Member

  #18
  May 26, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Ajifunze kuthamini haki za binadamu hawezi kuwawekea mipaka wanafunzi ambao sheria mama inawaruhusu kuishi mahala popote ili mradi hawavunji sheria,ajitahidi kusafisha mji kwanza
   
 19. Katikomile

  Katikomile JF-Expert Member

  #19
  May 27, 2009
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 473
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45

  Sasa ndugu yangu MTAZAMOWANGU, unataka hii forum ya JF ifungwe au? Make hapa si kumhukumu mtu wala kumchukia mtu, ni kujenga hoja na kuijadili kama hii ya ndugu yako Lukuvi, ili kama aliteleza ajirekebishe. Mimi si mwanasiasa na sioti wala kutarajia kwenda huko, so sioni kwa nini nimchukie Mh. Lukuvi. Wec are not always perfect, kama alikurupuka au alishauriwa vibaya tujadili hapa, my thread has nothing to do with JEALOUSY to Hon. Lukuvi!!!!!!!!!!!

  Unaposema wanafunzi kusomea kwenye wilaya zao lina tija fulani nina wasiwasi kama umewahi kuhishi jijini Dar na kujionea hali halisi. Si kila mtu kajenga nyumba yake hapa. Wengi ni wapangaji wa kuhamahama. Na si kila mzazi anampeleka mwanae St. Manispaaa (Shule za kata), wengine wanapendelea St. Fulani, ilimradi kuna ubora wa elimu.

  Huu ndio mtazamo wangu mimi kwa Lukuvi
   
 20. Katikomile

  Katikomile JF-Expert Member

  #20
  May 27, 2009
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 473
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Taarifa haikufafanua kama ni shule za serikali au privately owned schools.
   
Loading...