Mr II awachomea wasanii wanaoipigia debe CCM;Ataka wananchi kutohudhuria matamashayao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mr II awachomea wasanii wanaoipigia debe CCM;Ataka wananchi kutohudhuria matamashayao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Feb 28, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Feb 28, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  MBUNGE wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi, maarufu kama Mr.II (CHADEMA) amewataka Watanzania kuwahukumu wasanii wa miziki hapa nchini ambao wamekuwa wakikipigia debe Chama cha Mapinduzi (CCM), kwa kutoingia kwenye matamasha yao.
  Mbunge huyo amesema, wapo wasanii ambao wamekuwa wakiishabikia CCM kuwabeza wananchi na kwamba wasanii wa namna hiyo ambao wanafahamika wanapaswa kuhukumiwa kwa wananchi kutoingia katika maonyesho wanayoyafanya kwenye maeneo yao.
  Mbilinyi aliyasema hayo juzi mjini Musoma mkoani Mara, wakati alipozungumza na halaiki ya watu waliojitokeza kwenye maandamano makubwa ya CHADEMA, yaliyofanyika katika viwanja vya Mkendo mjini hapa.
  “Ndugu zangu wapo wasanii wanawasaliti wananchi kwa kukodiwa na CCM wakati wa kampeni...wasanii hawa msiwe mnaenda na kulipa kwenye matamasha ama maonesho yao.
  “Kama wanakula meza moja na CCM ina maana hawawapendi Watanzania, hukumu yao ni ya kutokwenda wala kununua miziki yao, si mnawajua lakini?” alihoji Sugu ambaye aliwahi kutikisa anga la muziki miaka ya nyuma.
  Aidha, mbunge huyo alisema wasanii wanaoshirikiana na CCM hawawatakii mema wananchi na kwamba watu hao ni sawa na wasaliti wakubwa, hivyo wanatakiwa wahukumiwe kwa staili ya kususiwa kazi zao.
  Katika mkutano huo ambao ulifurika maelfu ya watu, Sugu ambaye aliitwa na wananchi kupanda jukwaani kuwapa mistari (kuwaimbia muziki), alihitimisha mkutano huo mkubwa kwa kuimba nyimbo zake kadhaa.
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Feb 28, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  WELL SAID,hawa wasanii inatakiwa wadhulumiwe zaidi na wahindi ili akili ziwarudi.
   
 3. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #3
  Feb 28, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Ni kweli kunatakiwa kuwe na boycott ili wapate somo.
   
 4. K

  Kapeche Member

  #4
  Feb 28, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  No, is not fair kuwazuia watu na interest zao! tuko huru kushabikia chama tukitakacho, hata kama wamekodiwa ni sababu ya njaa zao. Usiwahukumu wasanii wetu bado wanatafuta, au sababu ameshakuwa mbunge hana shida ya kupanda jukwaani ndio maana anafanya hivyo? Waliipigia CCM kampeni kwa malipo tena makubwa, waache wasanii wetu watoke na wao
   
 5. n

  nyantella JF-Expert Member

  #5
  Feb 28, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Mr. II that is not fair!!

  Uliahidi kuwatetea wasanii wote bila kubagua sasa unawasaliti, ni ajira tu na siasa ni siasa na hata unayosema unajua tu sii ya kweli. Ile ni ajira tu!! Mbona Marando humsememi anavyo mtetea nanihii kwenye kesi yake? Acha vijana wapate rizki, umeisha sahau mara hii?. CCDM mnaenda kubaya mtawagawa Wataanzania!!, acha kila mtu aamue afanye na nani kazi mwisho wa yote anaye stahili atatwala tuu, kama ni Chadema fine lakini unachofanya sii sawa na wananchi wapuuze hayo maoni yako. Ofcourse una uhakika wa kula ila na wewe ungesusiwa kazi zako!!
   
 6. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #6
  Feb 28, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Wengi wa Wasanii nchi za Magharibi hata kama ni wapenzi wa chama chochote hawaendi kwenye kila campaign za uchaguzi kila kona kufanikisha idadi ya watu kuwa wengi sababu watacheza na kuimba nyimbo halafu viongozi wanahutubia; Angalia Miaka 34 ya CCM pale Dodoma hakuna watu waliokwenda sababu hakuna matumbuizo kwa wanaCCM; hawakulipwa hao wasanii.
   
 7. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #7
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kuna mtu hapa aliisha wahi kusema kuwa akili ya sugu ni kama ya chura, anaruka ruka tu bila kutizama mwelekeo. Yaani ameisha shindwa hata kabla hajaanza siasa, Mungu akurehemu Sugu RIP
   
 8. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #8
  Feb 28, 2011
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Duh! ukisikia kuchemsha ndio kama hivi!
   
 9. LD

  LD JF-Expert Member

  #9
  Feb 28, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mi sio mwana siasa mzuri, lakini kwa hili....................
  Naonga mkono hoja yako mkuu!!
   
 10. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #10
  Feb 28, 2011
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,761
  Trophy Points: 280

  You miss a point comrade,

  Sugu is a politician! That is it! Unategemea awafagilie wanaosupport mbaya wake CCM?

  Kiukweli, lets be real. Hili swala inategemea unaliangalia kwa mtizamo upi. Wasanii wengine bwana wanaendeshwa kama gari bovu. Utawakuta wanaiimbia CCM..harafu hao hao kesho wanalalamika kwamba kazi zao zinaibiwa na serikali haichukui hatua (kama kupitisha strong intellectual property laws). Mi nasema hivi..hawa wasanii..ambao leo wanaimbia CCM wakati wanajua fika kwamba CCM is not advancing their cause sidhani kama ni wa kuhurumiwa.

  By the way, it is a non starter kuwatetea eti ni njaa inawasumbua. Hivi tunaweza kujustify wananchi wanaouza kadi ya kupiga kura kusudi wapewe tshirts na kofia? jamani...lazima tufike mahali tufanye maamuzi magumu! Tutasingizia njaa mpaka lini? Tuache unafiki. Kama hukubaliani na CCM....please...get out of it. Tuache kusingizia njaa. Kila mtu ana njaa. Lakini haitufanyi kuwasupport mafisadi simply because tunataka tupate mlo wa leo. Na kesho je?
   
 11. anti-fisadi

  anti-fisadi JF-Expert Member

  #11
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Big up sugu, hii ndio spirit..ni kusonga mbele bila kuangalia nyuma. Ole wao wageukao nyuma..

  Haiwezekani msanii katika uelewa wa kawaida akaungane na mafisadi na kuwapigia debe kwenye kampeni zao haf mimi adui ya mafisadi nikamuunge mkono huyo mwanamuziki. Hainijii akilini,kwani hapo lao n moja, kumshabikia mnyoonyaji wa mali za umma!?
  Ni bora wakae chonjo kipindi hicho..sio kupotezea na hao mafioso
   
Loading...