MR II aka 'Sugu' Sasa Awa Mheshimiwa, Awa Mbunge wa Mbeya Mjini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MR II aka 'Sugu' Sasa Awa Mheshimiwa, Awa Mbunge wa Mbeya Mjini

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MziziMkavu, Nov 2, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 2, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280


  [​IMG]
  Msanii mkongwe wa Bongo Flava MR II aka "Sugu" amekuwa mbunge wa Mbeya Mjini Tuesday, November 02, 2010 2:47 AM
  Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Joseph Mbilinyi aka MR II au maarufu kwa jina la Sugu ameshinda uchaguzi wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya CHADEMA kwa kumbwaga vibaya mgombea wa CCM na wagombea wengine. Joseph Mbilinyi aka MR II amepanda chati na sasa atakuwa akijulikana kama Mheshimiwa Joseph Mbilinyi baada ya kufanikiwa kuingia kwenye bunge la kutunga sheria la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  MR II alishinda uchaguzi wa Mbeya Mjini kwa kuwabwaga vibaya wapinzani wake, Benson Mpesya wa CCM, Prince Mwaihojo, wa CUF, Tokolasi Kasuluari wa DP na Aggabo Mwakatobe wa NCCR.

  Msimamizi wa jimbo hilo alimtangaza MR II kuwa ni mshindi wa jimbo hilo baada ya kupata kura 46,411 huku mpinzani wake mkubwa toka CCM, Benson Mpesya akifuatia kwa mbali akiwa na kura 24,327.

  MR II anatarajiwa kuwa mtetezi mkubwa wa maendeleo ya jimbo lake na wasanii wa muziki wa Bongo Flava nchini.

  Wakati wa kampeni, kundi la muziki wa kizazi kipya la Wagosi wa Kaya kutoka Tanga, lilitoka na kitu kipya kiitwacho ‘Sugu Nenda Bungeni’, kikiwa ni maalum kwa ajili ya kumpigia debe aingie Bungeni.

  Wakiongea na Nifahamishe.Com wakati wa kampeni, Wagosi wa Kaya walisema kuwa Walisema kuwa wanamfahamu vilivyo Sugu kwa jinsi alivyo mpigania haki na mtetezi wa wanyonge hivyo wanaamini akiwa bungeni atakuwa na nafasi kubwa ya kuwatetea wananchi wa Mbeya na wasanii wa muziki nchini.
  Chanzo: NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.
   
 2. r

  rmb JF-Expert Member

  #2
  Nov 2, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 224
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hongera sana nenda katetee haki za vijana
   
 3. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #3
  Nov 2, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Baada ya kukurukakara za uchaguzi nitaandaa ujumbe kwa timu mpya ya wabunge wa chadema. Huu ni mwendelezo mzuri wa jitihada za kuwang'oa mafisadi wote nchini. Hongea Mr. II.
   
 4. Kiraka

  Kiraka JF-Expert Member

  #4
  Nov 2, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 2,551
  Likes Received: 613
  Trophy Points: 280
  Hongera sana Mr II, kama kawaida yao,
  wamebana wameachia!!
   
 5. E

  Elias Ezekia Member

  #5
  Nov 2, 2010
  Joined: May 11, 2010
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh. Mbilinyi. Sasa anaingia ulingoni. Tunataraji apigane kwa nguvu ili aweze kuwa First Eleven katika timu ya Kisiasa iitwayo CHADEMA ndani ya ligi kuu itwayo Bunge.
   
 6. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #6
  Nov 2, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hongera mr 11 kama kawaida wamebana mwishowe wameachiaaa
   
 7. t

  twombeya New Member

  #7
  Nov 2, 2010
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  congratulation fantastic ... Mbeya lead for changer im tired with thieves and ccm
   
 8. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #8
  Nov 2, 2010
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Sasa wasanii mavi watakoma..si walikuwa wanajifanya kumponda sugu..
   
 9. J

  Jackob Member

  #9
  Nov 2, 2010
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmmmh!!! Sipati picha kilichotokea Mbeya.
   
Loading...