Mr II a.k.a Sugu kugombea ubunge Mbeya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mr II a.k.a Sugu kugombea ubunge Mbeya?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mzizi wa Mbuyu, Jul 1, 2010.

 1. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #1
  Jul 1, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Jana iliripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya Mr II atawania ubunge katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya CHADEMA, na jimbo analowania ni Mbeya mjini.....
  Kama ni kweli Sugu nazidi kumheshimu,.... kwani unafiki wa kujipendekeza CCM kwa wa sanii wetu umezidi, big up sugu.....ni haki yako ya msingi na ukizingatia awamu hii umenyanyaswa sana na Serikali hii ya JK na Mwamae Ridhiwani akiwa kinara wa kukupiga vita...!!
  Mwaga sera mkuu, mbeya ni watu waelewa sana wanaweza kukusogeza mjengoni......
   
 2. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ni uamuzi wa busara na ni haki yake ingawa wengi wanafikiri kugombea ubunge ni haki ya wanataaluma nyingine na wala si wanamuziki licha ya kuwepo kina Kapteni John Komba mjengoni hiyo hawaoni.
   
 3. l

  luhongedzo Member

  #3
  Jul 1, 2010
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dah big up mtu mzima ila naomba spika asije kuomba ushushiwe net kama utaingia na kuanza kusinzia kwenye sofa za mjengoni. kuna watu walikuja na moto mkali kama wa kifuu kumbe dawa yao ilikuwa maji, Waliingia kwa mikwala mingi mwishoe wakaishia na kupozwa kwa ruzuku na sasa wana-sinzia bungeni tena wanatuma maombi kwa spika eti waruhusiwe kuja na mashuka kwenye kikao
   
 4. k

  kichenchele JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2010
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 521
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Naam hongera sana Mr.II a.ka Sugu, uamuzi huo hauna shaka, kwanza ni haki yako kikatiba, mimi binafsi nakupongeza sana, ningetamani vijana wengi wenye upeo wajaribu kuikomboa nchi yao kwa kupitia milango mingine, maana huu mlango wa zamani umeshaoza na siku yoyote utakuja kuanguka japo watu wameushikilia ili usianguke tena wanahasira ile mbaya, naomba tukupe support kubwa . Vijana tukiacha kunung'unika na kuamua kufanya mambo kwa vitendo tunaweza kufanya mambo makubwa kwa Taifa letu, hizi sera za zidumu fikra za mwenyekiti enzi zake zimeshapita tokea enzi za akina KINJENKITILE NGWALE, sasa hatudnganyikiiiiii
   
 5. minda

  minda JF-Expert Member

  #5
  Jul 1, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  hongera sugu! japo bado ni mapema umetoa mfano mzuri wa uthubutu kwa vijana wa kitanzania na hasa wasanii wenzako kuwa bongo fleva na hip hop ulizoasisi siyo taasisi za kihuni bali ni sehemu muhimu kijamii atakayochangia kwa maendeleo ya nchi yetu.
   
 6. kmp

  kmp Member

  #6
  Jul 1, 2010
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hongera sana kaka joseph mbilinyi a.k.a uncle sugu.nakuunga mkono.mwendo ni ule ule antivirus mpaka mjengoni!
   
Loading...