Mr Blue ndiye msanii mwenye uwezo mkubwa kwenye stage kuliko wasanii wote wa bongo fleva Tanzania?

maisha ni kupanda na kushuka
jana tulishuka cheki leo tunapanda
nimepata idea ya kusambaza kanda
nimepata show za kenya na uganda
burundi na rwanda
hatari sana huyu bwana mdogo
 
Unamjua diamond platinumz wewe?ambaye Rita paulse akiwa kwenye BSS anamtumia Kama reference ya stage master artist kwa washiriki.
Achana nae huyo kavuta bange mbichi, kwa sasa ukitaka kulinganisha wasanii Bongo sharti useme "ukimtoa Diamond" kumlinganisha Diamond na wasanii wengine wa Bongo ni zaidi ya matusi. Diamond kawazidi sio muziki tu hadi umalaya hakuna anayemfikia.
 
Naomba nitangaze rasmi kuwa Mr Blue is a King of Bongo flavour on stage akifuatiwa na kichwa kimoja cha enzi kinaitwa PIG BLACK hawa jamaa wakisimama pamoja stejini unaweza omba show isiishe.
Kwenye stage ni king...hatari sana...
 
Unamjua diamond platinumz wewe?ambaye Rita paulse akiwa kwenye BSS anamtumia Kama reference ya stage master artist kwa washiriki.
Hayo ni maoni yako mimi nasema na ukweli uko mweupo Mr blue ni moto wa kuotea mbali
 
Achana nae huyo kavuta bange mbichi, kwa sasa ukitaka kulinganisha wasanii Bongo sharti useme "ukimtoa Diamond" kumlinganisha Diamond na wasanii wengine wa Bongo ni zaidi ya matusi. Diamond kawazidi sio muziki tu hadi umalaya hakuna anayemfikia.
Wewe endelea kubisha lakini kwa sasa kwenye stage kama unafatilia hata matamasha sidhani kama Diamond anaweza kuwa na pumzi ya Mr blue hata mara moja...Mimi ni shabiki wa Diamond lakini kwenye kuimba na mashabiki+pumzi stegini Diamond hawezi kumfikia Blue.... Diamond ana mshinda mambo mengi Blue lakini si kwenye hili ninalo lijadili..
 
Pumzi? unajua idadi ya nyimbo anazo perform Diamond na Mr. Blue? Diamond muda mwingi anaimba na kucheza kwa step sawa na madancer wake,pumzi anayotumia huwezi linganisha na Mr. Blue. Blue anaweza kuwa mzuri stajini sikatai ila sio kwa kusema ni bora kuliko wasanii wote, hata Rostam hawafikii kwa perfomance na pumzi jukwaani.
 
Mada ni ya Mr. Blue kwanini unaleta wengine??
Kama humkubali si unapita kimya kimya tu halafu unaenda kuanzisha uzi wa kumsifia umpendaye.

Ndio maana wengi hufeli mtihani.
 
Unamjua diamond platinumz wewe?ambaye Rita paulse akiwa kwenye BSS anamtumia Kama reference ya stage master artist kwa washiriki.
Alafu kumbe we jamaa ni shabiki limbukeni wa wavaa vikuku.

Maana hapa anazungumziwa byser wewe unaanza kuwaingiza wakina daimondi.
 
Jamaa naskia anakubalika japo mimi nasikilizaga nyimbo zake zile za mwanzo kama mapozi nk
Hizi zingine simuelewi
Mkuu hata Mboga 7 huielewi? Binafsi kwa Bongo hii wanaume wa nguvu wa Bongo flavour ni Mr. Blue, sir. Nature na Q-Chillah. Wengine miyeyusho tu
 
Wasalaam wana jamvi

Pamoja kuwa tumezawadiwa wasanii wengi sana wa muziki wa kizazi kipya nchini lakini ni wachache sana ambao kila mtu angependa kuwasikiliza au kuwasubiria watafanya nini wakiwa kwenye stage au wakiwa mbele ya mashabiki.....
Wasanii wetu wengi ni wajuvi wa kuimba kwenye radio tuu lakini wakiwa kwenye matamasha hutamani kuendelea kuwasikiliza kwani wengi wao pamoja na kuwa na nyimbo zinzo tamba lakini wakiwa kwenye stage wanakuwa wamepoa sana na huwaboa mashabiki sana tena sana na unaweza fikiri labda mashabiki hawamfahamu muhuisika....

Mr Blue ni mmoja ya wasanii ambao pengine wanaweza wasiwe wana sikika sana radioni au kutotoa nyimbo kila leo radioni lakini ukweli ni kwamba ana nguvu kubwa sana tena sana kuliko hata wasanii ambao kila leo husikika na nyimbo mpya radioni......

Nilipata wasaha kumshuhudia kwenye TV kwenye tamasha la komaa na mziki mnene yanayo andaliwa na E-fm kwakweli ni ukweli usiopingika kuwa Mr Blue ndiye msanii pekee wa bongo fleva anayeweza kupambana na wasanii wa singeli kwenye kuwapagawisha mashabiki kwenye matamasha......

Mr Blue ni msanii mwenye nguvu sana stageni kwakweli mwanzo nilikuwa nashangazwa na yeye kupewa show kila mara pamoja na kutokuwa na nyimbo mpya nyingi radioni au kutosikika sana radioni...... kwa jicho langu nimethibitisha ni msanii mkali sana stageni ukiwaacha wa singeli ambao kwakweli wanatoa upinzani mkubwa sana kwa wasanii wa bongo fleva.

Wasalaaam
Ni kweli jamaa yuko vizur, ana energy ya kutosha na anakubalika kwa mashabiki kitu kinachofanya show zake zivutie.
Ila huku mikoani sio wakumlinganisha na hao waimba singeli.
Hao waimba singeli hawapo katika level hizo unazojaribu kuwalinganisha labda huko Dar.

Ila jamaa jukwaa analiweza
 
maisha ni kupanda na kushuka
jana tulishuka cheki leo tunapanda
nimepata idea ya kusambaza kanda
nimepata show za kenya na uganda
burundi na rwanda
Twende pamoja twende tukasake chanda..
Mungu akijalia nazuia kibanda.. namiliki kiwanda..
Tuko pamoja si ungefunga mkanda..
!! Yote kwa sababu __ nipe tabasamu.

Blue ni hatari.. Ubishi pembeni.
 
Mada ni ya Mr. Blue kwanini unaleta wengine??
Kama humkubali si unapita kimya kimya tu halafu unaenda kuanzisha uzi wa kumsifia umpendaye.

Ndio maana wengi hufeli mtihani.
Huyo ni mgeni hili jukwaa anafikiri yeye ndio pekee ana mshabikia Diamond hahaha
 
Ni kweli jamaa yuko vizur, ana energy ya kutosha na anakubalika kwa mashabiki kitu kinachofanya show zake zivutie.
Ila huku mikoani sio wakumlinganisha na hao waimba singeli.
Hao waimba singeli hawapo katika level hizo unazojaribu kuwalinganisha labda huko Dar.

Ila jamaa jukwaa analiweza
Waimba singeli kwakweli wanajua kukonga nyoyo za mashabiki kama hutojali tuletee hapa clip hata mbili za E-FM huko mikoani kwenye mziki mnene au komaa concert....
Lakini speaking of Mr Blue ni level nyingine ndio maana nimesema hapo juu kuwa yeye ndiye anaweza kwenda nao sambamba
 
Alafu kumbe we jamaa ni shabiki limbukeni wa wavaa vikuku.

Maana hapa anazungumziwa byser wewe unaanza kuwaingiza wakina daimondi.
hahaha huyo jamaa ni wakumsamehe tuu hahah
 
Back
Top Bottom