chinchilla coat
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 5,107
- 10,968
Mr. Blue Anadai kuwa kutokana na ustaa aliokuwa nao, wasichana wengi walimtaka na yeye alichokifanya ni kuchagua amtakaye na kumpa mambo. Blue anasema enzi hizo alikuwa playboy haswaa!
Anasema yeye alikuwa hajui kutongoza mwanamke na wasichana walikuwa wanakuja kwake anachagua wa kuwa naye kisha anawaambia wenzake waliyekuja nae aondoke au mpenzi wake anakuja na rafiki yake kisha anamuambia wewe leo sikutaki namtaka rafiki yako leo wewe ondoka na anaondoka na kesho yake anarudi tena.
Ameongezea kuwa wasichana wengi walikuwa wakija na kujazana maskani yeye anachagua tu utafikiri walikuwa wanasubiria hela.